Taarifa kamili: Chanzo vifo waliokula KASA Micheweni Pemba hiki hapa

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99

WATU watatu wamekufa na wengine zaiidi ya 28 wamelaza katika Hospitali ya wilaya Micheweni wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kula samaki aina ya KASA katika shehiya ya Msuka.

Akizungumuzia tukio hilo daktari wa Wilaya ya Micheweni Mkubwa Habibu amesema kuwa tayari wagonjwa waliofika wanapatiwa matibabu huku akibainisha changamoto ikiwa kukosa ushirikiano pamoja na taarifa sahihi kutoka kwa waathirika wa tukio hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema kuwa mpaka sasa hajapata idadi ya wananchi ambao wametumia samaki huyo.

Aidha amewataka wananchi waliotumia samaki huyo kuweza kujisalimisha katika kituo cha afya ili waweze kupatiwa matibabu.

Naye Seif Mzee Khamis mzazi wa watoto wawili waliofariki kutokana na tukio hilo amesema yupo tayari kutoa ushirikiano ili kuweza kunusuru maisha ya wengine.
 
Kasa sio samaki ni jamii ya kobe maji.
images%20(8).jpg
 
Naanzaje kununua kobe jamani?.pole zao ni bahati mbaya labda walimeza kitu kibaya hao kasa
 
WATU watatu wamekufa na wengine zaiidi ya 28 wamelaza katika Hospitali ya wilaya Micheweni wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kula samaki aina ya KASA katika shehiya ya Msuka.

Akizungumuzia tukio hilo daktari wa Wilaya ya Micheweni Mkubwa Habibu amesema kuwa tayari wagonjwa waliofika wanapatiwa matibabu huku akibainisha changamoto ikiwa kukosa ushirikiano pamoja na taarifa sahihi kutoka kwa waathirika wa tukio hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema kuwa mpaka sasa hajapata idadi ya wananchi ambao wametumia samaki huyo.

Aidha amewataka wananchi waliotumia samaki huyo kuweza kujisalimisha katika kituo cha afya ili waweze kupatiwa matibabu.

Naye Seif Mzee Khamis mzazi wa watoto wawili waliofariki kutokana na tukio hilo amesema yupo tayari kutoa ushirikiano ili kuweza kunusuru maisha ya wengine.

We tapeli kama wale wa ile hela tuma namba hii, hicho chanzo mbona hakipo.
 
Daah kwa sura yake ilivyo watu wana roho ngum jmn au ni uroho tu sasa huyo kasa m namuita kobe wa majin walikulaje watu thelathin mbona nashangaa
 
WATU watatu wamekufa na wengine zaiidi ya 28 wamelaza katika Hospitali ya wilaya Micheweni wakiendelea kupatiwa matibabu baada ya kula samaki aina ya KASA katika shehiya ya Msuka.

Akizungumuzia tukio hilo daktari wa Wilaya ya Micheweni Mkubwa Habibu amesema kuwa tayari wagonjwa waliofika wanapatiwa matibabu huku akibainisha changamoto ikiwa kukosa ushirikiano pamoja na taarifa sahihi kutoka kwa waathirika wa tukio hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amesema kuwa mpaka sasa hajapata idadi ya wananchi ambao wametumia samaki huyo.

Aidha amewataka wananchi waliotumia samaki huyo kuweza kujisalimisha katika kituo cha afya ili waweze kupatiwa matibabu.

Naye Seif Mzee Khamis mzazi wa watoto wawili waliofariki kutokana na tukio hilo amesema yupo tayari kutoa ushirikiano ili kuweza kunusuru maisha ya wengine.

Huyo kasa alikuwa mkubwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom