Taaluma ya polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taaluma ya polisi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by wikama, Sep 17, 2012.

 1. w

  wikama Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ivi karibuni jeshi la polisi limeanzisha Diploma in Police science je hii itasaidia kuweka polisi kwenye perfomance nzuri au wameanzisha kwa nia ipi ? Polisi ina wasomi wengi lakn sio wataluma hiyo na kwenye utendaji kuna uoga mwingi hakuna anaejiamini toka IGP - PC ndo maana unakuta migongano mingi kutoa maamuzi kwa kuwa hawana uhakika na wanachokifanya penye kufuata sheria wanatoa amri matokeo yake mauaji. Wadau mnaonaje taaluma iyo kuanzishwa ?
   
 2. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  itasaidia ila wasifundishe siasa bali wafundishwa bomu la machozi linaweza kuua mtu!!! itasaidia...elimu kwa wote!!! teh teh teh....
   
 3. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  taaluma ni nzuri, na haitofautini na taaluma nyingine za social science kwa mawazo yangu.

  Kinachoboa katika utendaji wa kipolisi, ni pale tu jeshi linapokuwa na uhusiano na siasa. IJP huteuliwa na mwanasiasa. Unapoteuliwa na mwanasiasa, lazima kuna expectation kadhaa anazozitarajia kutoka kwako. Ni katika kutimiza expectation ya bosi aliyekuteua basi unaingilia haki za watu wengine hivyo unaharibu.

  Kwa upande mwingine, makamishina wote file zao ziko kwa mkuu wa kaya. Mkuu wa kaya anaamua nani awe kamanda nani awe mkuu wa kitengo fulani. Katika kutekeleza hilo, makamishina wamejikuta wakitekeleza hadi amri za bosi, kwa wanandamu tuliowengi, tunaamini kuwa tupo ili tule vizuri, na kwa kuwa mkuu wa kaya anakuwezesha kula vizuri, utalinda sana lindo lako hatimaye UNAWAKAMHANDA WATU wengine wanaodai uwajibikaji wa serikali ya bosi wako.

  Viongozi waandamizi kuanzia ASP hadi SSP, nao kwa upande mwingine wanaendekeza yaleyale kwa kuamini kuwa wanapokuwa wamemsaidia mkuu wa kaya na chama chake katika nafasi nzuri, basi kuupata u commisioner inakuwa ni rahisi na kupata madara mengine ya kipolis.

  Kujibu swali lako, Taaluma ya POLICE SCIENCE na taaluma nyingine ndani ya jeshi kama sheria, sociology, ualimu na nyingine nyingi zitakuwa na maana iwapo tu:-

  (a) Tutaweza kutenganisha siasa na utendaji wa umma. Hii ni kusema kuwa kama ni viongozi wa polisi watokane na sifa zilizoainishwa au waachiwe polisi wenyewe kuwapigia kura.
  (b) Viongozi wa wizara nao wataajiriwa kwa sifa zao ni wala si kwa nasaba walizonazo na watawala. hapa namzungumzia mkurugenzi na waziri wake.

  Yote haya yatafanikiwa iwapo wananchi watayadai katika katiba mpya na yakasimamiwa.
   
 4. w

  wikama Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani taaluma iyo ni njema kama itatumiwa lakini uongozi jeshi la polisi haufuati elimu ila ukiwa na refa mambo shwari ndo mana wasomi wanachukiwa na hawataki ushauri.
   
 5. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,888
  Likes Received: 564
  Trophy Points: 280
  Ivi wakuu, taaluma na AMRI vinaendana?! Mbona mi nnaona kama kuna ukinzani hapa? Sawa mi sipingi hii ishu kuanzishwa, lkn itakuwa sawa na 'kutandika godoro kwenye banda la nguruwe' ukitaka alale kwa usafi!
  Hii kwa kweli ni ngumu sana kuleta mabadiliko kwa sababu hautaapply ulichosoma bali utaendelea kufuata AMRI!
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,230
  Trophy Points: 280
  Upolisi ni kazi ya watu wavivu kufikiria, wenye kutii amri tu kutoka juu na kuzitekeleza bila kujali madhara yatakayo tokana na amri hiyo
   
 7. S

  Suma mziwanda kageye JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inawezakua science ya virungu.
   
 8. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,897
  Likes Received: 4,750
  Trophy Points: 280
  Umetisha sana jembe
   
Loading...