El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 263
- 502
Mnamo mwaka 2011 nchini Kenya, ilipitishwa Sheria ya bunge iliyounda chombo au wakala wa kusimamia na kiratibu utendaji wa kazi wa Jeshi la polisi, INDEPENDENT POLICING OVERSIGHT AUTHORITY. (IPOA)
Na masukumo mkubwa wa kuanzisha chombo hiki ulitokana na historia ya muda mrefu ya kutaka kubadili dhana ya upolisi iliyokuwepo ya utumiaji wa nguvu zisizo na kiasi( unreasonable force), jeshi kujihusisha na uingiliaji wa mambo ya Kisiasa( political interference, na ukiukaji ulokuwa umekithiri wa haki za binadamu(wide spread violations of human rights).
Ndiposa kianzishwa chombo au wakala huo. Kazi zake pamoja na majukumu yake yaliyopelekea kupitishwa kwa wakala huu ni pamoja na:
1)kuchunguza vifo na majeraha makubwa yalosababoshwa na matendo ya polisi
( To investigate deaths and serious injuries caused by police actions.)
2)kuchunguza mwenendo mbaya wa polisi ( To invistigate police misconduct)
3)kusimamia, kufanya rejea na kukagua uchunguzi na matendo yanayofanywa na unit inayosimamia utendaji wa kila siku wa polisi ( To monitor, review and audit investigations and actions by the internal affairs unit of the police)
4) kufanya ukaguzi wa makazi na maeneo ya polisi (To conduct the inspection of police premises).
Kama nilivyoanza kusema au kuandika hapo juu huu ndo wakati muafaka nionao was sisi pia kuwa na chombo hiki.
Chombo hiki ni Cha kiraia na kinaundwa hasa na raia wenye taaluma tofauti ingawa pia uhusisha polisi wastaafu kama sehemu ya makamishina kwa ajili ya kutoa hints za kitaalamu ba hasa za upolisi wenyewe.
Kwa mtazamo was wengi, na ndivyo ilivyo, polisi wetu hapa wana madaraka yaliyopindukia na hawana usimamizi wowote wa Kila siku wa kazi zao.
Polisi wanakamata( arrest) wanapeleleza( investigation) na sehemu kubwa wao bado ndo waendesha mashitaka( prosecution)
Hivi hapa kweli kutakuwa na haki inayopaswa kutolewa?
Hapa jamvini kumejaa malalamiko ya watu juu ya vitendo mbalimbali vinavyoendelea ndani ya jeshi letu. Hivi wao wanawajibika Kwa nani wakati wanapofanya mambo yaliyo kinyume na kazi zao?
Ninajua Kuna mamlaka zao za nidhamu ktk majukumu yao lakini nani anamwajibisha nani wakati kazi na pengine hata hulka zao zimeshafanana kwa sababu ya nature ya kazi zao?
Nimeona juzi msajili wa vyama vya siasa akiomba kukutana na wakuu wa jeshi la polisi bila shaka kurekebisha( to regulate) yanayoendelea Sasa ambapo polisi wanavamia na kutawanya vikao vya ndani vya vyama jambo ambalo hawana jurisdiction ya kulifanya..
Sijui, kama nikisoma katikati ya mistari polisi wanaweza wasimsilize maana yeye hahusiku nao kisheria tena Wana uwezo hata wa kumkamata yeye kwenye kikao hicho wakitaka maana wao ndo kila kitu . Vipi kungekuwa na over sighting body huoni wangejua kwamba Wana mahali wanapowajika na kuchukuliwa hatua? There is no authority not under another authority"..
Haya mauaji yanayosababishwa na polisi, wanachunguza wenyewe, wanapeleleza wenyewe na kushitaki wao, KESI ya nyani unampa nyani mwenziwe,mwenye mahindi atapata haki yake?
Kuchunguza mienendo mibaya ya polisi. Nani amchunguze mwenzake na kweli hatua zichukuliwe? Ndiyo wanaweza kulindana wao ndani kwa ndani lakini ulinzi wa kweli uko nje.
Malalamiko ya wananchi juu ya mienendo na tabia mbaya za polisi yalipaswa yapelekwe siyo kwa OCD au hata RPC bali chombo huru ambacho polisi wanawajibika kwacho. Kulindana na kukingiana kifua ni kwingi kwa sababu kazi Yao ni moja na wakati mwingi wanafahamiana
Je unategemea nini hapo?
Nani anafuatilia utendaji wa kila siku wa central unit ya Polisi?
Ni kweli IGP abawajibika kwa waziri na kwa Rais. Lakini je nani anakutana naye mara kwa mara kumuhoji na hata kumuonyesha yeye na makamanda wake mahali wanapoacha taaluma Yao, unyanyanyasaji nk.
Waziri ni mwanasiasa, wakati mwingine unyanyasaji wa haki A watu na hasa za kisiasa no mtaji kwake . Nani atamwambia yeye na timu yake kwamba" you have gone beyond boundaries"na akaogopa?
Nawashauri serikali katika wimbi hili ambako polisi wanalaumiwa kila mahali na vilio ni vingi juu ya kukiukwa Kwa haki za binadamu na manyanyaso yanayodaiwa kutendwa na polisi, ni wakati sahihi sasa iwepo mamlaka ya kiraia kama ilivyo IPOA Kenya itajayosimamia haki za raia wenzao. Kuwaacha polisi watambe na kwa sababu ni chombo cha nguvu chenye madaraka makubwa ni kuwaumiza raia wa nchi husika na mwisho wa siku wataichukia serikali.
Mara zote husema madaraka yasiyodhibitiwa huharibu kabisa" absolute power corrupts absolutely" polisi wetu Wana absolute power wadhibitiwe.
Leo nimesikia kutupwa kwa KESI ya mbowe ambayo pamoja na mambo mengine alikuwa analakamika juu ya kukamatwa kwake kwamba haki zake zilikiukwa. Ukiacha technicalities na mambo ya mahakama, chombo kinachoaimamia polisi kama IPOA, kingepokea makakamiko hayo na kumwita IGP au afisa mhusika wa polisi kujibu maswali kama;.
Kwa nini kiongozi was hadhi ya mbowe anavamiwa na kukamatwa kama jambazi? Of course angeambiwa hiyo siyo professionalism
Kwa Nini kumfunga mtu kitambaa toka mwanza mpaka Dar! ( Kama ni kweli maana mambo mengine nasi tunayasoma tu) ? Wangefanya uchunguzi na hata kuwawajibisha polisi waliofanya hivyo, kupendekeza kuwashusha vyeo nk ingebidi.
Mahakama haiwezi ona mambo ya nature hiyo kabisa.
Ni wakati sasa tuwe na chombo kinacholeta checks and balances kati ya polisi na jamii na hasa kuwafanya polisi wawe disciplined na wawe na hofu Kwa maana ya reverence wanapotekeleza majukumu yao.
Hata hivyo bado tunawahitaji polisi na Jeshi lao maana ni watu wa muhimu kuwa nao.
Wasalaam