T.B Joshua na Askofu Gwajima!

T.B Joshua na Askofu Gwajima!

Uko wapi ushahidi kuwa TB Joshua alitabiri ushindi wa Lowassa?
Hizo ni propaganda tu.

MBINU za Edward Lowassa kutaka kurejea kileleni katika ulingo wa kisiasa zimemnasa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo, imefahamika. Beatrice ambaye alikuwa akijitambulisha kuwa mmoja wa "wapambanaji dhidi ya ufisadi," waliopachikwa jina la "Mitume kumi na miwili," sasa anatajwa kuhamia rasmi mtandao wa Lowassa. Gazeti hili limepata ushahidi wa maandishi ya mkono wa Beatrice mwenyewe yanayoonyesha kuwa amekuwa mfuasi muhimu wa Lowassa kiasi cha kushawishi wengine kujiunga katika mtandao wake. Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alieleza mambo matatu katika ujumbe wake kwa Chana. Kwanza, kumshukuru Chana kwa kukubali kulinda kura zake. Pili, kumshawishi kumuunga mkono Lowassa. Tatu, kumweleza juu ya ulokole wake na "mtumishi aliyepakwa mafuta" kutoka Nigeria. Beatrice anamwambia Chana kuwa Lowassa ndiye kampeni meneja wake. Hii ilikuwa katika uchaguzi wa makamishina wa Bunge; nafasi aliyogombea na kushinda. "Mungu ni wa ajabu, (Lowassa) ameniombea kura pasipo maelezo. Ameandaa lunch na dinner (vyakula vya mchana na usiku) ambako amekuwa akiniombea kura. Ana njia za ajabu za kufanya mambo. Ahsante kwa kukubali kuhesabu kura," inasema sehemu ya ujumbe huo. Chana, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, ndiye alihesabu kura za Beatrice kwenye uchaguzi wa kutafuta makamishina wa Bunge. Ni kwenye ujumbe huo ambamo Beatrice anatoboa kuwa siri ya ushindi wake ni Lowassa aliyekuwa kampeni meneja wake. Katika kusisitiza hoja yake, Beatrice anasema, "Nimezungumza na TB Joshua wa Emmanuel TV Nigeria aliyenipa unabii kuwa rais ajaye Tanzania ni Edward Lowassa, nikamuambia haiwezekani kwani amechafuka sana." Anasema Joshua alimjibu, "…alikuwa amechafuka sasa amesafishwa kwani katubu. Akaniambia his past is over (maisha yake ya nyuma si kitu). Akaongeza kwa kusema, wewe Beatrice ningeangalia your past (maisha yako ya nyuma) pengine nisingekuombea kabisa. Akasema my past is over (hajali maisha yangu ya nyuma)," inasema sehemu ya ujumbe huo wa Beatrice. Hata hivyo, Beatrice hakueleza katika waraka wake kwa Chana maisha yake ya nyuma yalikuwa vipi. Wala hajaeleza alifanya nini, hadi kuamini kuwa kama Nabii Emmanuel angeyatazama, basi asingemuombea. Kuvuja kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya Lowassa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje. Mume wa Beatrice, William Shelukindo alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo iliongoza harakati za kuundwa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba tata wa Richmond. Ni taarifa ya kamati hiyo iliyosababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu, Februari 2008. Kwa mujibu wa watu waliokaribu na Beatrice na kwa ushuhuda wake mwenyewe, mwanasiasa huyo ameamua kujisalimisha kwa Lowassa kwa kile kinachoelezwa kuwa "Lowassa ndiye rais ajaye wa Tanzania." Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku kukiwa na juhudi kubwa zinazofanywa na Lowassa na kundi lake kutaka kujisafisha kwa lengo la kujitosa katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015. Miongoni mwa mikakati aliyojiwekea Lowassa na kundi lake ni kujitokeza katika maeneo yote muhimu na kutoa kauli ambazo zitafanya wananchi waanze kumkubali kuwa ni kiongozi anayefaa. Katika kutekeleza mkakati huo, Januari mwaka huu, Lowassa alijitokeza kuzungumzia vurugu zilizotokea mkoani Arusha zilizotokana na mvutano katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo kati ya CCM na CHADEMA. Katika mnyukano huo, watu watatu walipigwa risasi na polisi na kufariki dunia baada ya polisi kutumia nguvu isiyo ya kawaida kuzima maandamano ya CHADEMA. Kauli hiyo ya Lowassa ilikuwa tofauti na msimamo wa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtaka kuwasilisha maoni yake katika vikao vya chama badala ya kutumia vyombo vya habari. Kauli nyingine ya Lowassa ilihusu nyongeza ya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi, kutokana na kile alichoita mfumuko wa bei kuwa mkubwa. Bali wiki moja iliyopita, Naibu Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicholas Mganya alimtuhumu Lowassa kwa kutoa kauli hiyo akisema ana ajenda ya siri nyuma yake. Mgaya alisema TUCTA haihitaji msaada wa Lowassa katika kusimamia madai yao. Alisema "mbunge huyo wa Monduli inaonekana ana ajenda yake mgongoni." Hatua nyingine ya Lowassa katika kujikarabati kisiasa ni kugombea na kupata nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Lowassa amekuwa pia akihudhuria hafla nyingi, hasa za madhehebu ya Kikiristo (KKKT) ambao anaonekana akitoa maoni mbalimbali kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita ukumbi wa Dimaond Jubilee kwenye uzinduzi wea albamu ya moja ya kwaya za injili. Kwenye kusanyiko hilo, Beatrice naye alikuwepo. Lowassa alimtaka asome maoni ya gazeti la The Citizen juu ya ushirikina uliokithiri nchini; jambo ambalo Lowassa alizungumzia kwa urefu. MwanaHALISI lilipowasiliana na Beatrice ili kupata maoni yake juu ya ushwahiba wake mpya na Lowassa, mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: Mwandishi: Tusaidie maelezo kidogo juu ya ujumbe uliomwandikia Mheshimiwa Pindi Chana kumjulisha kuwa uliambiwa Edward Lowassa atakuwa rais. Ni kweli? Beatrice: Barua ameandika nani na umeipata wapi? Mwandishi: Hii barua fupi – memo ndani ya Bunge, uliposema Mheshimiwa Lowassa ambaye amesimamia vizuri kura zako za ukamishna wa Bunge. Beatrice: Sina taarifa hiyo. Wala siikumbuki. Unajua ndani ya Bunge tunaandikiana mambo mengi, tena mengine ya utani tu. Na mimi na Mheshimiwa Chana sote ni "walokole," tunafanyiana utani sana. Mwandishi: Kwani mheshimiwa Shelukindo, mkiwa ndani ya bunge kuna utani mwingi, kwamba huwa mnaandikiana utani sana? Beatrice: Kabisa, unajua tunaandika mambo mengi. Na kama unaandika kwa utani kwa mwenzako inabaki hivyo ni utani tu. Sasa tatizo hao wanaowaletea mambo haya wanatumia mambo haya kutafuta mipango yao ya kufikia mwaka 2015. Alisema, "Mimi najua hakuna anayenibeba ndugu yangu. Mimi ni very solid (ngangari), sibebeki. Nakwambia, mbona mimi nina nguvu nyingi mimi mwenyewe; sihitaji kubebwa. Najua wanajaribu kuonyesha tunabebwa, lakini huo ni ujinga wao wa kufikiri. Mwandishi: Mheshimiwa Shelukindo, kwani nyie waheshimiwa huwa mnatafutana (kufitiniana)? Beatrice: Hiyo inafanyika sana, watu wakishakuwa na mambo yao wanatumia wengine kutimiza dhamira zao. Lakini mimi ninafikiria wananchi. Nimeshaamua kwamba Beatrice nashughulikia shida za wananchi jimboni. Ninatafuta njia za kuwaondolea umasikini, njaa na mambo kama hayo. Sasa wengine wanatafuta tu pa kunishika. Mwandishi: Kwa hiyo Mh. Lowassa ndiye alikuwa kampeni meneja wako katika kutafuta ukamishna pale bungeni, au siyo Mheshimiwa? Beatrice: Lakini kama anafanya kazi ya kampeni vizuri; ni vizuri tu. Isipokuwa kila mtu anajichukulia mwenyewe alivyo. Mimi ni mtu wa kazi sihitaji kusimamiwa hivyo. Na hebu tujadili hili; unajua kaka nyinyi mnafanya kazi kubwa. Sasa hii kusikia, sijui MwanaHALISI hivi, sijui hivi, pengine kuna watu wanachomekea vitu vyao. Tunapenda kazi yenu. Mwandishi: Mheshimiwa nakushukuru sana. Beatrice: Karibu sana tutafanya kazi pamoja. Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, mume wa Beatrice, William Shellukindo, alikuwa na msimamo mkali dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ufisadi nchini na hiyo ndiyo inayoelezwa kuwa sababu ya kushindwa kwake ubunge katika mchakato wa ndani ya CCM. Shellukindo alikuwa mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga kwa zaidi ya miaka 20, alishindwa katika kura za maoni na January Makamba, mtoto wa katibu mkuu wa CCM anayetajwa kuwa mfuasi wa mtandao wa Lowassa. S0urce by Mwanahalisi – 9 March 2011
 
TB JOSHUA Hajawahi kumtabilia Lowasaa urausi mods ingilia kati huu ni uhuni na uzandiki!
 
TB JOSHUA Hajawahi kumtabilia Lowasaa uraisi mods ingilia kati huu ni uhuni na uzandiki!
 
TB joshua ni tapeli tu kama matapeli wengine sugu.Tofauti yake yeye anatumia jina la dini. Hebu rudini katika maandiko angalieni Biblia inasema nini kuhusu wanaojiita manabii siku za mwisho huku wakikataa kuishi kama Yesu alivyoaagiza. "Uza vyote wagawie maskini kisha unifuate". hapo manabii wengi hutoka nduki na visingizio kibao.

Mpelekee Lumbesa ya vipeperushi vya Ellen G. White mkuu aongoke.
 
Hiyo movie scripts? kama ndio, naomba kujua itatoka mtaani lini? :yawn:
 
Yesu hakumaanisha physical assets, alikuwa anamaanisha uache Yale yote matamu unayoyapenda kisha umfuate. Matamu ni Kama uzinzi, ulevi, anasa, na dhambi nyingine tuzitendazo.

Soma vizuri Marko 10:17-20: Yesu almwambia yule kijana azishike amri, usiue, usizini,usiibe, usishuhudie uongo.... Yule kijana akajibu kuwa hizo kazishika tangu utoto. Ndipo Yesu alipomwambia auze mali zake awape maskini atakuwa na hazina mbinguni, ndipo yule kijana aliondoka kwa masikitiko kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.

Hapo inazungumziwa mali alizonazo mtu, uzinzi ulishatajwa tangu mwanzo.Msipotoshe maandiko kwa makusudi yenu.
 
Chunga sana ulimi wako ndugu yangu. Haya ni maisha, huwezi jua kesho. Unaweza kuja kuumwa vibaya, huyo huyo unaemwita tapeli ndo akaja kukuponya. Hujui lolote kuhusu TB joshua, hivyo ni bora unyamaze.

Namtegemea Yesu kuniponya sio TB Joshua na manabii feki.
 
Chunga sana ulimi wako ndugu yangu. Haya ni maisha, huwezi jua kesho. Unaweza kuja kuumwa vibaya, huyo huyo unaemwita tapeli ndo akaja kukuponya. Hujui lolote kuhusu TB joshua, hivyo ni bora unyamaze.


Amka kutoka usingizini wewe!!

Yaani akili yako inamtegemea binadamu mwenzako kukuponya badala ya Mungu?! Na yeye huyo mtabiri wako akiumwa huponywa na nani?! Kwanini usubiri huyo mpiga ramli akuombee kwa Mungu? Wewe mwenyewe huwezi kumuomba Mungu? Au yeye yupo karibu zaidi na Mungu kuliko wewe?

Think outside the box and wake up!!
 
TB Joshua ni moja ya matapeli wale wa kinageria .... yuroba tribe... hawa jamaa ni wasanii sana... alimpa moyo mzee wa watu akajua kuwa i kweli ataukwaa upresidaa.... watanzania tukasema "NO..NO..NO...NO..." hahaha yaani TB joshua ukimuangalia usoni amekaa kisanii kabisa... nasikia kaja kuchukua ile pete yake aliyompa lowassa
 
Mbona sijawahi kuona popote TB Joshua akitabiri hayo? Nachojua mimi Team Nyumbu walizusha hiyo wakidhani inawapa kick..

Mwenye ushahidi wowote wa utabiri huo na aweke hapa
 
TB joshua ni tapeli tu kama matapeli wengine sugu.Tofauti yake yeye anatumia jina la dini. Hebu rudini katika maandiko angalieni Biblia inasema nini kuhusu wanaojiita manabii siku za mwisho huku wakikataa kuishi kama Yesu alivyoaagiza. "Uza vyote wagawie maskini kisha unifuate". hapo manabii wengi hutoka nduki na visingizio kibao.

Nimegundua unamuongelea usiyemfahamu vizuri.
 
Namtegemea Yesu kuniponya sio TB Joshua na manabii feki.

Fahamu kwamba Yesu huponya kupitia watu wake hapa duniani, ungewahi kumfatilia Prophet TB Joshua hata kwa nusu saa tu ungejua anatumia jina la Yesu. Tatizo tunakimbilia tu kuwataja kuwa ni manabii feki bila hata utafiti mdogo
 
Soma vizuri Marko 10:17-20: Yesu almwambia yule kijana azishike amri, usiue, usizini,usiibe, usishuhudie uongo.... Yule kijana akajibu kuwa hizo kazishika tangu utoto. Ndipo Yesu alipomwambia auze mali zake awape maskini atakuwa na hazina mbinguni, ndipo yule kijana aliondoka kwa masikitiko kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.

Hapo inazungumziwa mali alizonazo mtu, uzinzi ulishatajwa tangu mwanzo.Msipotoshe maandiko kwa makusudi yenu.
Yesu alimwambia auze mali kumwonyesha unafiki wake kuwa ameshika amri zote. Kiukweli Yesu alikuwa anamwonyesha amevunja amri ya Kwanza kwa uchache: Usiwe na miungu mingine. Mali alikuwa mungu wake, no wonder baada ya kuambiwa amuuze mungu wake akasikitika na kutokomea...!
 
Mwamakula, ni vizuri post yako ikaambatana na vithibitisho ili kuweka mada sawa. vinginevyo Moderator mnalazimika kutunza heshima ya Jukwaa hili. Udaku umekuwa mwingi sana JF now days!
 
Last edited by a moderator:
Amka kutoka usingizini wewe!!

Yaani akili yako inamtegemea binadamu mwenzako kukuponya badala ya Mungu?! Na yeye huyo mtabiri wako akiumwa huponywa na nani?! Kwanini usubiri huyo mpiga ramli akuombee kwa Mungu? Wewe mwenyewe huwezi kumuomba Mungu? Au yeye yupo karibu zaidi na Mungu kuliko wewe?

Think outside the box and wake up!!

You are the to wake up, hata hivyo fahamu kuwa mambo ya Kiroho hujulikana kwa jinsi ya Rohoni na si mwilini.
 
TB mwizi na tapeli kala ela za mamvi na urais hajaupata
 
Nendeni zenu yule ni mtumishi Wa mungu na katumwa na mungu
 
Nendeni zenu yule ni mtumishi Wa mungu na katumwa na mungu

Sisi sote tumetumwa na Mungu kumuabudu yeye na si kumtegemea Binadamu mwenzetu ambaye hata yeye yupo chini ya uangalizi wa Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom