Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,383
Nimegundua unamuongelea usiyemfahamu vizuri.
Wewe unaabudu usichokijua
Nimegundua unamuongelea usiyemfahamu vizuri.
Utafiti nje ya Biblia ni kujilisha upepoFahamu kwamba Yesu huponya kupitia watu wake hapa duniani, ungewahi kumfatilia Prophet TB Joshua hata kwa nusu saa tu ungejua anatumia jina la Yesu. Tatizo tunakimbilia tu kuwataja kuwa ni manabii feki bila hata utafiti mdogo
Umenena mkuu. mwenye hekima atakuelewa.Sisi sote tumetumwa na Mungu kumuabudu yeye na si kumtegemea Binadamu mwenzetu ambaye hata yeye yupo chini ya uangalizi wa Mungu.
Nilishawauliza mna video clip ya utabiri wa Lowassa? Msitulishe maneno na propaganda zilizoganda
Yesu hakumaanisha physical assets, alikuwa anamaanisha uache Yale yote matamu unayoyapenda kisha umfuate. Matamu ni Kama uzinzi, ulevi, anasa, na dhambi nyingine tuzitendazo.
Yesu hakumaanisha physical assets, alikuwa anamaanisha uache Yale yote matamu unayoyapenda kisha umfuate. Matamu ni Kama uzinzi, ulevi, anasa, na dhambi nyingine tuzitendazo.
Soma vizuri Marko 10:17-20: Yesu almwambia yule kijana azishike amri, usiue, usizini,usiibe, usishuhudie uongo.... Yule kijana akajibu kuwa hizo kazishika tangu utoto. Ndipo Yesu alipomwambia auze mali zake awape maskini atakuwa na hazina mbinguni, ndipo yule kijana aliondoka kwa masikitiko kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.
Hapo inazungumziwa mali alizonazo mtu, uzinzi ulishatajwa tangu mwanzo.Msipotoshe maandiko kwa makusudi yenu.
Mtailetea laana nchi kwa kuwanena vibaya watumishi wa Mungu aliye hai
Yesu alimwambia auze mali kumwonyesha unafiki wake kuwa ameshika amri zote. Kiukweli Yesu alikuwa anamwonyesha amevunja amri ya Kwanza kwa uchache: Usiwe na miungu mingine. Mali alikuwa mungu wake, no wonder baada ya kuambiwa amuuze mungu wake akasikitika na kutokomea...!