2013
JF-Expert Member
- Aug 2, 2011
- 11,358
- 6,060
Upo uwezekano hali ya Syria isitulie kama inavyotarajiwa. Kwasababu makundi yenye nguvu zaidi ndio yameonekana kupoteza kwenye hivi Vita. Hivyo lazima hayata kubaliana na matokeo.
Kwanza hivi ni Vita vya Kidini na Kiuchumi. Hizo ndio engines mbili zinazofanikisha kuona Waarabu wakifunguana butcher kila siku bila kujisikia vibaya.
Saudi Arabia ikionekana kama master mind wa hii Chessboard.
Tatizo la Pale Arabuni ni la Udini, Uchumi, nguvu ya Ushawishi
Udini kwasababu Mataifa ya ki Sunni yakiongozwa na Saudia kupitia umoja wao yanataka kuondosha tawala za waShia katika.mashariki ya kati.
Kama tujuavyo Syria inaongozwa na mShia. Wakati Iraq na Iran, ni dola za waShia wengi.
Mataifa ya Ki Sunni hayapendi hii hali iwe hivi. Yanataka kubadili hizi regime ili waSunni ndio watawale.
Mataifa ya Ulaya ni kama yanalipwa kufanya kazi hii. Wazungu wanapata Msukumo kwasababu za ki -Uchumi. Ambapo master mind atakua ni Saudia na kikosi chake cha Arab League.
Saddam Hussein alikua Msunni aliyetawala Iraq kwa mkono wa Chuma. Baada ya kuanguka utawala wa Iraq, Ilitawaliwa na washia walionyanyaswa na Saddam.
Baada ya hapa, Kukaibuka Arab Springs dhidi ya mataifa yaliokua chini ya madikteta, kuanzia kule Tunisia, Libya na Egypt.
Arab Spring haikuishia hapo ilienda hadi Syria.
Kwakua waarabu wamezoea Kutawaliwa badala ya kuongozwa. Kazi hii ya kulitifuatifua inakua nyepesi.
SYRIA.
Maandamano ya Syria yalipelekea machafuko kwa baadhi ya watu kushika Silaha. Matokeo yake Serikali ya ki Shia ya Bashar Al Assad ikawa inatupia lawama ksa waSunni kua ndio wanaoleta machafuko. Hii ikapelekea Uadui zaidi kati ya aShia na waSunni kuuana.
Waasi Wakaandaa mpango wa kuangusha Serikali ya kishia ya Syria ilio chini ya kiongozi Assad(Ambaye ni Mshia).
Mataifa ya kiarabu walikua wameunda Islamic states(IS), Ambapo Ilikuja na majina mbalimbali kama njia ya kujiimarisha zaidi. Iliitwa Islamic States of Levante (ISIL na ISIS) na mwishowe IS).
Islamic States ikaanza pale Iraq huku ikijitanua na kupewa ufadhili na mataifa yenye utajiri wa mafuta kama Qatar na Yemen.
Japo Agenda yao waliibadili hapo baadaye lakini haikuathiri nguvu yao ya kujitanua.
IS walieneza propaganda kua wanaunda Dola kuu ya Kiislamu ulimwenguni. Ajenda ilionunulika kirahisi na wengi. Mpaka makundi yenye nguvu ya wakati huo kama Alqaeda,Taliban na Nusra fronts yakapoteza wingi wa wafuasi ambao waliamu kujiunga na IS.
Kuhusu Syria, yalianza maandamano.
Kisha yakaletwa Madai kua Bashar kaua raia wake kwa sumu. Ajenda hii ililetwa ili kumshawishi USA aingie Vitani. Manake hakua na maslahi pale
Hivyo inaonyesha waundaji wake ni UK na France, Wakaunda Waasi(ARAB/MILITIA) ili kuung'oa utawala wa Syria. Lililoitwa Syria Defence force(SDR).
Turkey ilisapoti harakati hizi ikilenga Kudhibiti nguvu ya waasi wa kikurdi. Ambao walikua wanataka kuunda taifa lao.
UK na France zikamshinikiza US aingie.
Enzi ya Obama. Obama alikataa. Kwakua hakutaka US ijihusishe na vita yoyote. Alitaka iwe kama China.
Hata hivyo, Mwishowe akakubali kuingia nusunusu, alikataa kupeleka jeshi, akawa akishambulia maeneo muhimu yalioshikiliwa na Syria, kwa ndege za kivita. Na kuwasapoti waasi kwa kuwapa Silaha.
Turkey iliunga mkono harakati hizo.
Wakati huo IS walikua wana gain grounds katika viunga vya Syria na wakimbizi wengi wanakimbilia ulaya kupata asylum.
Kule Arabuni kuna jamii ya wakurdi wanapatikana katika nchi za TURKEY, IRAQ,SYRIA na IRAN.
Wakurdi wa Syria waliamua kupambana na serikali ya Syria, wakiwa na lengo la kuunda Taifa lao.
USA
Kama ilivyo ada US haina maislahi yoyote pale Syria. Lakini France na UK wana Interest pale.
Trump anafahamika ni rafiki wa Putin.
Mara Trump alipoingia akaamua kuwaunga mkono Wa kurdi wa Syria ili wamng'oe Assad.
Jambo hili halimpendezi Turkey, ambaye anahofu kuibuka kwa machafuko ya wakurdi wa nchini kwake, ikiwa tu wakurdi wa sehemu zingine wangepata Nguvu. Vilevile jambo hili halizipendezi mataifa mengine kama Iraq na Iran.
Ujerumani chini ya Merkel iliwahi kuonya kuhusu Hatari hiyo huko Nyuma. Wakati US inashirikiana nao kuung'oa utawala wa Saddam.
RUSSIA
Russia ana mkataba wa kuilinda Syria.
Anapambana kulinda utawala wa Syria chini ya Bashar Al Sadr.
Turkey na Russia wameboresha uhusiano wao
Ulikua umezorota baada ya Ndege ya Russia kudunguliwa na Turkey. Lengo ni ili wawadhibiti waKurdi wa Syria na walioko Turkey.Turkey ambaye ni mwanachama wa NATO.
Russia alitofautiana na USA kuhusu Tafsiri ya Magaidi nchini Syria.Ambapo wote kwa pamoja walikua wakidai wanapigana Vita dhidi ya magaidi.
Tafsiri ya Magaidi kwa Mujibu wa USA;-
Inahusisha Serikali ya Syria (Bashar Al Assad), IS na Vikundi vya Iran.
Wakati kwa upande wa Russia magaidi ni;- Wakurdi, Syria Democratic Forces(SDF) na IS kwa pamoja.
Russia ndio imekua msimamizi mkuu wa kutatua huu mgogoro kijeshi kuliko mataifa ya magharibi. Na hii imefanya Ushindi uwe upande wake.
IRAN
Iran ambayo inapalilia vita nchini Yemen, pia inaunga mkono utawala wa kiShia wa Syria(Assad) haiko tayari kuona unang'olewa na waSunni, nayo ikajiingiza Syria, ikichukua wapiganaji kutoka Afghanistan, Lebanon kwa Hezbollah na Iran na kutumia mabilioni ya dola kufadhili vita hivyo.
Iran inapambana kuhakikisha waKurdi wa Syria hawafanikiwi kuunda taifa lao.
ISRAEL
Israel ikihofia Adui yake Hezbollah na Iran, ikajiingiza ili kushambulia meli zenye silaha zinazo safirishwa kutoka Iran kupelekwa kwenye vikundi vya Hezbollah, Ili kuwezesha vita vya Syria na kutishia usalama wa Israeli.
Mapambano haya ndio yalimuweka Israel kiurafiki karibu na ufalme wa Saudia na nchi za ki Sunni. Hata Saudia kuamua kuruhusu anga lake kutumiwa na ndege za kijeshi za Israel.
Hivyo pale Syria pakawa na makundi 4. makubwa yakipigana:-
1. Waasi wa Syria( Arabu militia) ama Syria Democratic Forces.
2. WaKurdi
3. Islamic States.
4. kikosi cha waIran, Afghanistani, Hezbollah kikipigana sambamba na Jeshi la Syria dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na mataifa ya magharibi.
Waasi wakiungwa mkono na mataifa ya magharibi na Saudi Arabia ili waunde dola ya kiSunni katika Syria. Hawa wengi vita kwao ni Ibada.
WaKurdi dhidi ya serikali ya Syria, Iran, Russia na Turkey. Ili waunde taifa la waKurdi.
Wao Islamic States ikipigana ''solely dhidi ya makundi yote hayo, Ili kutanua Dola kuu ya kiislamu mashariki ya kati. IS ni wa Sunni extremists. Japo hawa pia walikua wakipata msaada Qatar na Yemen hapo kabla haujakatwa.
MAKUNDI YENYE USHIRIKA;
1. Iran ikiunga mkono serikali ya Ki Shia ya Syria(Assad), Russia na Iran zinapokutana. Kama upande mmoja.
2. Waasi, USA, Saudi Arabia, Israel, WaKurdi wakiwa upande mmoja. France, UK, Qatar, etc.
Vita hii imedumu muda mrefu wa miaka 7 na imekua vigumu kumng'oa Bashar Assad, kwasababu anapata backup kutokea Moscow.
Russia imeapa kumlinda Asad kwa gharama yoyote.
Mpaka ilipofika ni kwamba waasi wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi wamepoteza eneo la Douma ambalo ndilo walibakiwa nalo.
Na kwakua US hana Maslahi na ile vita, Na ukichukulia kua Trump ni rafiki wa Putin. UK na France zimejaribu kutafuta sababu ya
Kumrudisha US pale Syria ili kumuondoa Assad.
Ndipo ilipokuja sababu za mataifa ya West kutaka kumpiga Assad kwa kuwaua raia wa Syria kwa sumu.
Na kabla hili halijatokea, ilianza tukio la jasusi wa Russia Skripal kuwekewa sumu kule UK.
Wakaanza na vikwazo. Hata hivyo Russia imeonyesha kukataa kuhusika na matukio yote hayo mawili.
MAMBO YA KUCHUNGUZA
Uchunguzi huru unashindikana kwa sababu US hataki. Anaamini Russia wataharibu uchunguzi wakishiriki. USA wanataka wachunguze wenyewe.
Mambo ya kipekee;-
Trump anaaminika ni rafiki sana na Putin.
Hii imepelekea hata nchini kwake iwe vigumu kuaminika.
UN wanataka hii vita isije ikachochea vita kubwa kati ya Russia na US.
Hii ndio iko mezani kwa sasa.
UKWELI USIOSEMWA
USA NA UK Hazijui mahali hizo silaha za sumu zilipo fichwa huko Syria. Kama zingejua mapema, zingeshashambulia kabla hata mauaji haya hayajatokea. Hivyo tishio la Trump kushambulia Syria ni la kisiasa zaidi, lenye lengo la kuongeza shinikizo. Labda mpaka wapate Uhakika ni wapi hasa silaha hizo zimefichwa.
Lakini UK na France zinataka Washambulie.
German imekataa kushambulia, kwasababu ya utegemezi wake kwa Russia. Imeona iunge mkono US, UK na France lakini haitashiriki.