Swali: Yuko wapi Juma Duni Haji?(Ban Duni)

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Heshima Kwenu,
Kwa muda mrefu sasa simsikii kwenye medani za siasa aliyekuwa mgombea mwenza wa UKAWA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.Huyu ni Juma Duni Haji ambaye ana cheo cha makamu mwenyekiti kwenye Chama cha Wananchi CUF.Toka aliporejea kutoka UKAWA alikokuwa kwa matakwa ya makubaliano ya ushirikiamo, hajasikika tena. Yuko wapi Babu Duni?
 
Utamsikia wapi wakati alijichomeka kwenye tumbo la dudumizi fisadi lenye kuwafisadi.. Utamsikia vipi wakati alikubali kunaswa kwenye mtego wa kujiunga na kampeni za matusi na kuviringisha mikono. Akatibua reputation yake kwa kuukana uanachama wa CUF ili awe mgombea mwenza. Siasa za Zanzibar ni za msimamo wa wastani ambapo Kiongozi unatakiwa kupima upepo kabla ya kukurupuka na mahitaji ya muda mfupi. Kabla ya hapo akina Tundu lisu walikuwa wanawazodoa viongozi hawa na kujiunga kwa Duni kwenye chadema ilikuwa ni matusi kwa wahafidhina wa mjini magharibi na Pemba. Kwa ufupi mzee huyu ndio basi tena kapotea kwenye ramani za siasa za Zanzibar.
 
Kuna viongozi wa chama wala siwasikii katika media Ispokuwa nawaona kwenye ziara za mikutano ya majimbo kuboresha chama, angalia video zote za mikutano ya cuf Zanzibar utamuona babu Duni
 
Heshima Kwenu,
Kwa muda mrefu sasa simsikii kwenye medani za siasa aliyekuwa mgombea mwenza wa UKAWA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.Huyu ni Juma Duni Haji ambaye ana cheo cha makamu mwenyekiti kwenye Chama cha Wananchi CUF.Toka aliporejea kutoka UKAWA alikokuwa kwa matakwa ya makubaliano ya ushirikiamo, hajasikika tena. Yuko wapi Babu Duni?
Duni yupo amekuwa mwanachama wa kawaida tu.
Alijaribu kugombea u makamu mwenyekiti Cuf,akaenguliwa katiba ilimbana.Katiba yao inataka ukae miaka miwili ndio ugombee,wakati Duni ana miezi sita tu CUF!
 
Huitaji uliza kujua kuwa kilichomkuta, ni kifo cha mende kisiasa....."chali mbendembende"...
Ujue kubwa lingine ambalo halikuzungumzwa, ni kuwa Mh Duni hakujua sharti la kikatiba la chama chake, pindi unapojitoa ktk chama, na kurejea ukitarajia siku inayofuata ugombee uongoze ktk chama...kwenye uchaguzi, alipewa kumbusho la kikatiba, lililomuwesha sawia ka kofi mardadi usoni....alibaki akiona nyota nyota, ktk tamaa zake za umakamu uwenyekiti wa chama...
Ah! Bora katupumzisha...
 
Duni yupo amekuwa mwanachama wa kawaida tu.
Alijaribu kugombea u makamu mwenyekiti Cuf,akaenguliwa katiba ilimbana.Katiba yao inataka ukae miaka miwili ndio ugombee,wakati Duni ana miezi sita tu CUF!
Bwege...hata vipengele muhimu vya uchaguzi wa ndani ya chama, wakati nyeti wa uchaguzi alishindwa vifanyia rejea...
 
Back
Top Bottom