Swali: Wanawake wanapendwa kwanza alafu ndio wanapenda?

Swali: Wanawake wanapendwa kwanza alafu ndio wanapenda?

shikwashikwa

Senior Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
188
Reaction score
46
Habari zenu wanajamvi,

Kuna kitu kinanitatanisha kidogo. Najua mko kwenye tafakuri nzito kuhusu hawa watangaza nia naombeni niwapumzishe kidogo Ili (kufrash mind). Mimi ni mwanaume rijali niko na mvuto wa wastani nimebahatika kupitia relationship nyingi kiasi na kila niliepita nae yupo na utofauti na mwenzie na wote walikuwa wananipenda.

Tatizo liko hapa;

Mimi kama mwanaume ninavigezo vyangu ninavyotaka toka kwa mwanamke (hapa nahisi kila mwanaume yupo hivyo) sasa napata shida kugundua mwanamke anatumia vigezo gani kumkubali mwanaume kwa mfano, niliwahi kuwa na uhusiano na binti mwembamba akaniambia anafurahi kuwa na mimi becouse sio mnene.

Tulipobwagana na mpenzi wangu wa zamani anatoka na jamaa mnene balaa, sasa naombeni mnisaidie hawa wanawake wanapendwa kwanza ndio wanapenda? Yaani wako automatic. Au kwao bora umekuja kama msaada twende tu mpaka tufikie lengo?

Naomba niwakilishe kwenu kwa ufafanuzi

Ahsante
 
Back
Top Bottom