Swali: Wajumbe wa Nyumba Kumi-Kumi ni Watumishi wa Serikali au Chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali: Wajumbe wa Nyumba Kumi-Kumi ni Watumishi wa Serikali au Chama?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Nov 28, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Hili swali limekuwa likitesa mtima wange.

  Nikitaka kupata, mathalani huduma ya kibenki ninaambiwa 'leta barua ya serikali ya mtaa'. nikienda serikali ya mtaa naambiwa leta barua ya mjumbe wa nyumba kumi-kumi.

  nikienda kwa mjumbe wa nyumba kumi-kumi na kutizama kwenye paa la nyumba yake, ninaona kuna bendera ya chama cha mafisadi (CCM) inapepea. mbaya zaidi nikiingia ndani kueleza shida yangu naambiwa nilipe "Tsh. 1000 ya mhuri"

  lakini mimi ishu yangu ni ya serikali. ishu ya benki. sasa mambo ya CCM yanaingiaje?

  ndiyo maana nauliza.

  hawa watu. mabalozi wa nyumba 10-10. ni watumishi wa serikali au wa CCM?
   
 2. k

  kayumba JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hilo ni swali la msingi, hata mimi niliwahi kuambiwa niende kwa mjumbe kuchukua utambulisho lakini aligonga muhuri wa CCM. Nilidhani ule utambulisho usingekubaliwa lakin, kumbe huo ndio ulitakiwa. Hata ukinunua ki-plot wajumbe wanamihuri ya chama!
   
 3. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndio hao hao ndio waliotumika kununua shahada za kupigia kura...
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  hao ni watu muhimu sana wa kuwezesha uchakachuaji kwa upande wa ccm, sio waajiriwa wa serikali!
   
Loading...