Swali: Wajumbe wa Nyumba Kumi-Kumi ni Watumishi wa Serikali au Chama?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Hili swali limekuwa likitesa mtima wange.

Nikitaka kupata, mathalani huduma ya kibenki ninaambiwa 'leta barua ya serikali ya mtaa'. nikienda serikali ya mtaa naambiwa leta barua ya mjumbe wa nyumba kumi-kumi.

nikienda kwa mjumbe wa nyumba kumi-kumi na kutizama kwenye paa la nyumba yake, ninaona kuna bendera ya chama cha mafisadi (CCM) inapepea. mbaya zaidi nikiingia ndani kueleza shida yangu naambiwa nilipe "Tsh. 1000 ya mhuri"

lakini mimi ishu yangu ni ya serikali. ishu ya benki. sasa mambo ya CCM yanaingiaje?

ndiyo maana nauliza.

hawa watu. mabalozi wa nyumba 10-10. ni watumishi wa serikali au wa CCM?
 
Hilo ni swali la msingi, hata mimi niliwahi kuambiwa niende kwa mjumbe kuchukua utambulisho lakini aligonga muhuri wa CCM. Nilidhani ule utambulisho usingekubaliwa lakin, kumbe huo ndio ulitakiwa. Hata ukinunua ki-plot wajumbe wanamihuri ya chama!
 
hao ni watu muhimu sana wa kuwezesha uchakachuaji kwa upande wa ccm, sio waajiriwa wa serikali!
 
Back
Top Bottom