Swali: Tutahiri wanaume wote bure ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali: Tutahiri wanaume wote bure ?

Discussion in 'JF Doctor' started by TIMING, Apr 21, 2009.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wenzangu;

  Kwa kuwa kutahiri wanaume kumekubalika kwamba ni kinga dhidi ya vi-HIV; je kwanini taifa letu lisitahiri watu wake wote bure... yani bila kulipia gharama za theatre [surgery] kama ambavyo tunatoa dawa za bure, vitendanishi kondomu na vipimo vingine katika health facilities?

  Hamuoni kwamba wahaya, wasukuma, wanyakyusa, wabena na wakinga watapata ahueni?
   
 2. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wazo zuri lakini sidhani kama wasiotahiri ni kwa sababu ya gharama bali ni jadi yao.
  Hivyo naona zipigwe campaigns za watu kutahiriwa, na hasa watoto wadogo ili iwe kama chanjo kabla hata hawajaanza mambo flani.
   
 3. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #3
  Apr 22, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hapo itakuwa ngumu kwa baadhi ya kabila ambao kwao si jadi yao kukatwa hiyo kitu.
  Fikiria tu mwenyewe kuwa umpe ushauri Professor Sarungi kuwa mh. unatakiwa ukatwe! Au Professor Rwebangira wa United States of America!
   
 4. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo hao hawajatahiriwa ehe!
   
 5. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #5
  Apr 22, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hao ni mwiko kwao kutahiriwa, ni jambo baya sana kwa mjaluo au mhaya kutahiriwa! mwiko mkubwa! wanaogopa tohara kama ukoma, ila ukimwi sidhani kama wanaogopa!
   
 6. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwani mpaka karne hii bado wanaendelea na hii jadi???
  Je kuna utafiti wowote umefanya katika karne hii na kuthibitisha hii kauli yako???
  Husije ukaombwa vithibitisho ukawa huna mkuu. Ili ni angalizo .
   
 7. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #7
  Apr 22, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  mtu wa kawaida,kwani wewe jadi yako unaweza isaliti?? kwa sababu tu ya kubadili namba ya karne?
   
 8. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkuu mambo ya jadi ya kila jamii inabadilika kutokana na wakati. Ndio maana ukiangalia vizazi vya kale hawakuwa wanavaa nguo kama za vizazi vya sasa.
  Ndio maana katika bandiko langu hapo juu nimekuuliza je umefanya utafiti wa kina na kuja na hii hitimisho ya mtazamo wako kuhusu jamii hz??
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Inategemea uko wapi lakini kwetu huku ngudu nimekutana na wataalam wa afya wa wilaya wanasema hata kale ka-elfu kadhaa ka kutahiri wao hawana na wanataka kaondoke ili kila mwenye govi aliondoe kwasababu hawana hako ka-bajeti kadogo

  gharama ina-range from 5,000 to 50,000
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  harro binti izee; hawajakatwa
   
 11. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  we una uhakika gani lkn? Mie naona kama unawatia aibu wenzako! lol
   
 12. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  WABUNGE wa kiume wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambao bado hawajatahiriwa, wametakiwa kutekeleza zoezi hilo mapema, ili kusaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi kwa kuwa tohara kwa wanaume ndiyo njia mojawapo ya kupunguza maambukizi mapya.

  Mbunge wa Dimani, Hafidh Ali Tahir (CCM), alitoa wito huo bungeni, alipokuwa akiuliza swali la nyongeza bungeni na kudai kuwa, viongozi wanapaswa kuongoza kwa mifano, hivyo kabla ya kuhamasisha wananchi, ni vema zoezi hilo lianzie kwa wabunge.

  Alisema iwapo wabunge watatekeleza zoezi hilo, watakuwa mfano mzuri ambao utaigwa, na kutolea mfano wa Rais Jakaya Kikwete aliyeonyesha mfano wa kupima ukimwi kwa lengo la kuhamasisha upimaji kwa hiari na kwamba zoezi hilo lilifanikiwa.

  Sanjari na swali hilo, mbunge huyo pia aliitaka serikali kuwachukulia hatua kali wale wote ambao wanaambukiza virusi vya ukimwi kwa makusudi na kusababisha kuendelea kuwapo kwa maambukizi mapya.

  Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda, alitoa wito kwa wanaume wote ambao wanaguswa na kitendo hicho kufanya tohara, ili kupunguza maambukizi hayo kwa kuwa suna kwa wanaume, inasaidia kupunguza maambukizi ya ukimwi.

  Kuhusu kuwachukulia hatua za kisheria wote ambao wanaambukiza virusi vya ukimwi kwa makusudi, Dk. Kigoda alisema tayari Bunge limeshapitisha sheria ambayo itawabana wanaofanya hivyo.

  Akijibu swali la msingi la mbunge huyo, Dk. Kigoda alisema kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanyika Afrika Kusini, Kenya na Uganda hivi karibuni, imethibitika kuwa tohara kwa wanaume inapunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya ukimwi (VVU).

  Dk. Kigoda alisema kutokana na ukweli huo, serikali inaandaa mkakati maalum wa kuhamasisha tohara kwa wanaume kote nchini kwa kutumia huduma zilizopo, ikiwa ni pamoja na kutumia sehemu za huduma za afya na za kiutamaduni.

  Alisema msisitizo utalenga kutahadharisha watu kuwa tohara peke yake haitoshi kudhibiti ukimwi, bali ni lazima itumike sambamba na njia nyingine ikiwamo kuacha ngono, uaminifu katika ndoa na matumizi ya mipira ya kiume (kondomu). Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alitaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kuhamasisha wanaume wengi nchini kutahiriwa ili kupunguza kasi ya kuenea kwa VVU
   
 13. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Dah! ama kweli ukstaajabu ya Azizi wa Kipawa utayaona ya Mwagito wa Msewe, eti kumbe enh! kutahir ni lazma waume ili kuzuia ngoma! asemae wa Dimani, ati kwamba asotahiriwa yu karibu sana na Msalaa? yaweza kuwa kweli nami cshangai kwani siye Mozaya alipochapa maji 2kapita na 2lipofika tu Sayuni kisu kilipita, eti tukawa safi na wapya! usafi na upya huu ulitupa mengi sanaa! kila mmoja alitutakaa si unajua tena kichwa wazi tena safii! haya watahiri?
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Spear, tatizo ni namna watu walivyoelewa hoja... kinachopiganiwa hapa ni kwamba tohara iwe sera!!! si ya kidini au mila kama baadhi wanavyotaka kuiweka bali ni kwa ajili ya afya zaidi

  It is evident kwamba kuna faida ya kukata kwa wanaume, kama ilivyo hasara ya kukeketwa kwa wanawake na kama tunataka tufanikiwe, hili jambo lije kisera zaidi

  Pretty, Its not about shame or fame!!! Its about serving the purpose
   
 15. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hivi mpaka leo hatujafahamu chanzo kikubwa cha maabukizi ya VVU?

  Hivi watu wa bara EUROPA wana-tahiri (hapa namaanisha kuondoa ngozi ya mbele ya uu.me)?

  Chacha Wa Mwita - Waganda hawatairi pia lakini walijua sababu ya maambukizi na waka-"reverse trend"

  Endelea kufanya zinaa saaaaaaana kwa kuwa umetahiri utanusurika!
   
 16. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapa sipati picha, mimi naamini serikali na wanaharakati mbalimbali huwa wanahamasisha wananchi kwamba wasifanye wasifanye ngono kabisa kwa wale ambao hawajawa na wenza wao wanaotambulika katika utaratibu rasmi, au wawe na mpenzi mmoja ambaye (pamoja na yeye) amepima VVU, au watumie kondom kwa wale wanaopenda mseto na mwisho kutumia damu salama. Sasa linapokuja suala la kutahiriwa wanaume kama sehemu ya vita dhidi ya maambukizi ya VVU inanijia taswira kwamba tumeanza kuhamasisha nyama kwa nyama.

  Je ikiwa mimi nimewowa (hapo nimeongea Kihaya kwasababu hawa jamaa ni shemeji zangu) na mke wangu analifurahia sana govi langu pale tunapofanya tendo la ndoa, harafu ikitokea nikachapa nje ya ndowa nikatumia zana, nitatahiri kwa kwa ajili ya nini? Huo si ndo mwanzo wa kumkosa mke wangu kipenzi?. Mimi nadhani indekuwa vema wanawake ambao walishawahi kufanya mapenzi na wanaume wenye govi wakajitokeza na kutoa uzoefu wao juu ya ladha ya kufanya ngono na mwanamume mwenye govi ikoje, au kama hakuna ladha. Angalizo masuala ya kwamba jamaa haoshi yasihusishe kwani hilo ni suala jingine.
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135

  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  Nimetoka patupu hapa ama kiswahili kigumu.
   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naunga hoja mkono Ndg. DN ila watumie staili ya Wamaasai katika kutahiri otherwise walipie huduma hiyo muhimu kwa wanaume
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Tujitahidi tutahiri jamani ndugu zangu wanaume
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Hilo ni jambo zuri sana la Kutahiri ingawa kwa Sisi Waislam tumelishafanya siku nyingi mimi nilivyozaliwa tu baada ya siku 40 tangu kuzaliwa nimekatwa Govi langu sasa kwa wenzetu Wakristo jambo hilo la kutahiri kwao litakuwa gumu ingawa Bwana Yesu Mwenyewe alishatahiriwa zamani sasa itakuwaje kwa wenzetu Wakristo au Msio Tahiri? fanyaeni kabla ya Serikali kuchukuwa Uamuzi kwa nguvu kumtahiri kila mmoja wetu kazi hapo ipo jamani na wale wasiotahiri kwa Wakristo wanakuwa hawamfuati Bwana Yesu Wanamfuata Mtume Paulo.
   
Loading...