Swali tata kwenye mapenzi

AkiliMingi AM

Member
Jul 5, 2020
88
58
Jamaa yangu aliwahi nipa story yake na demu wake, kwamba alikua anamuamini sana na demu ndie alikua akimtoa out mara mingi sana kuliko yeye, na anamnunulia vitu vya gharama kubwa mpaka alikua anaogopa.

Siku moja aliamua kwenda kwenye gheto la demu wake kwa kumstukiza mida ya saa mbili usiku, alipo fika alikuta demu yupo kajipumzisha ila kitanda kimevurugika haswaa yani si kawaida. jamaa akauliza mbona kitanda kiko rafu ivi demu akamwambia alikua amejilaza hapo tangu asubuhi ajaamka.

Muda wa kulala ulipofika jamaa si akaamua ale tunda lake demu akawa anamkazia, jamaa alipo jisumbua sana kufosi demu akamuuliza "ivi kama mwanamke wako akilala na mwanaume mwingine alafu akakupa tunda utajuwa ?" jamaa akamjibu ndio lazima nijue maana ntahisi utofauti, baada ya kujibu ivo dk 5 demu akasema anamaumivu ya kichwa anataka apumzike, basi jamaa akaamua kumuacha maana anampenda sana hakutaka kumkera.

Ivi kama ni wewe unasikia mwanamke wako anakuuliza swali hilo alafu anakunyima ghafla utafanyaje? unge mshauri nini mdau??
 
Kwani wakati akiletewa zawadi za gharama kuliko uwezo wa demu mbona hakuuliza?
Demu anampenda jamaa yako, ila pia anazitaka hela za sponsor.
 
Ilaa Bongo kina Uchebe wengi sanaa sema hawapigii ngumi tuu...!! Umarioo kazi sanaaa...
 
Kwani wakati akiletewa zawadi za gharama kuliko uwezo wa demu mbona hakuuliza?
Demu anampenda jamaa yako, ila pia anazitaka hela za sponsor.
Wanaoishi maisha ya hivi ni vijana wasiokuwa na hope na kesho yao..!! Ambao maisha yamekaza kweli but its not a Man nature kabisaaa
 
Wanaoishi maisha ya hivi ni vijana wasiokuwa na hope na kesho yao..!! Ambao maisha yamekaza kweli but its not a Man nature kabisaaa
Kwangu mimi zawadi ataleta na akizingua uchebe. Vijana wanashindwa kudictate terms. Wanazingua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom