Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Jamani wadau wenzangu,
Nina Swali rahisi sana kwa Mh. Zitto Kabwe. Jana baada ya taarifa kuwa Mahakama imetupilia kapuni kesi yake na kuipatia ushindi Chadema, Zitto aliandika hivi kwenye ukuta wake wa Facebook:
Swali lingine la mwisho, mbona hili suala la ESCROW linakuvimbisha kichwa kana kwamba wewe ndiye uliyeliibua? Katika hili swali langu la mwisho, nisieleweke kwamba nahafifisha kazi nzuri ambayo kamati ya PAC iliifanya, bali nieleweke kuwa ninatamani Kafulila apewe heshima inayomstahili katika sakata hilo. Yeye ndiye aliyeitwa ngedere, yeye ndiye aliyetishiwa kushitakiwa mahakamani, yeye ndiye aliyelipigania tangu mwanzo hadi mwisho. Krediti nyingi zingepaswa zimrudie yeye. Nikipata majibu ya maswali yangu haya mawili, moyo wangu utatulia kidogo.

Swali langu ni rahisi sana: Zitto unadhani ni nani hasa akuvurugaye? Je unadhani Chadema ndio waliochukia kazi yako katika ESCROW na ndio maana wakakufukuza uanachama? Je unadhani waliotuhumiwa katika ESCROW wametia mikono yao mahakamani na kusababisha mahakama ikunyime haki yako? Hapa unayemtuhumu kutumiwa na waathirika wa ESCROW ni Chadema au Mahakama?Kwa kazi ya ‪#‎TegetaEscrow‬ ilivyokuwa ingeshangaza waathirika kukaa bila kujaribu kunivuruga. Bahati mbaya sana sivurugiki.