Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
- Thread starter
- #41
Mkuu, ni lazima tukubaliane kuwa hiyo imekuwa silika ya watu katika siasa: kusifia watu wasiostahili kusifiwa au kuwapuuzia wengine waliostahili sehemu ya sifa hizo. Ndiyo maana nikasema, uongo ukishasemwa mara mbili haubadiliki na kuwa ukweli. Lazima tu tukubali kuwa suala la Richmond liliibuliwa na Dr. Slaa, akalipigania kwa nguvu zote. Hata pale Spika wa Bunge alipotafuta namna ya kulihafifisha, bado Dr. Slaa alisimama na kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua. Hivyohivyo katika suala la ESCROW, Kafulila ndiye aliyelipigania tangu mwanzo. Alitukanwa matusi mengi, na kama unakumbuka, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu alikaribia hata kumkunja Kafulila.It's never wrong bro, Ndivyo dunia nzima inavyoyachukulia maswala yote mazuri na mabaya. Osama hakuwa peke yake wala sio mwanzilishi wa Al Qaeda, Abraham Lincorn sio alokuwa na hoja ya Uhuru wa Marekani na wala hakuwa peke yake. Wewe si ajabu waendesha gari hapo unamjua aloivumbua? au unasifia Toyota yako! Na hata Uhuru wetu ulianza kuzungumziwa na wapiganaji wakiwa Barma lakini leo nani anawajua? na kibaya zaidi hata dhumuni la Uhuru wetu haswa hakuna mtu anayekumbuka!
Maana yangu ni hii, hatupaswi kuipuuza kazi iliyofanywa na Mwakyembe au Zitto katika skendo za Richmond na ESCROW. Nao walifanya kazi kubwa sana, istahiliyo heshima yake. Hata hivyo wao hawasimami kama wao, bali wanasimama kama wenyeviti wa kamati za Bunge, ambazo zina wajumbe kadhaa. Wanaposimama na kutaka kujizolea ujiko kuliko wale walioibua hoja, ni lazima tuwatilie mashaka kuwa wanatafuta sifa tu na ni wabnafsi. Leo katika suala la ESCROW tunapompuuzia Filikunjombe na kumpa sifa zote Zitto Kabwe, hatumtendei haki Filikunjombe na wanakamati wengine. Tena Filikunjombe ambaye aliwasulubu wenzake wa chama chake ndiye angepaswa aonekane shujaa zaidi. Vyovyote, sifa zaidi ziende kwa Kafulila, na sifa nyingine ziende kwa kamati ya PAC (na wala si Zitto).