Swali Makini kwa Wana JF Makini tu!

JATELO1

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,230
301
Wana JF,
Naomba kwa wale wenye ufahamu wanisaidie hili swali langu muhimu sana. JE KATIBA YETU YA TANZANIA INASEMAJE KUHUSU NAFASI NA MAJUKUMU YA FAMILIA YA RAIS WA NCHI YETU katika shughuli za Serikali. Nimeuliza hili swali kwasababu katika kipindi hiki cha Rais Kikwete, kumekuwa na safari nyingi sana za Mke wake-Salma (ndani na nje ya nchi) na mtoto wake Ridhiwani. Je, hizi ziara zote zinalipiwa na nani?

Kwani Mama Salma anapokwenda Mikoani amekuwa akipokelewa na uongozi wa Mkoa/Wilaya husika na mara nyingi anasomewa taarifa za kimaendeleo ya Mkoa au wilaya husika, sasa swali langu ni Je, nini nafasi ya First Lady katika katiba yetu. Pia hizi ziara za First Lady nazo zimekuwa nyingi sana, mara yuko huku leo kesho kule, Je gharama hizi zote zinalipwa katika bajeti ipi? Pia hata zile ahadi nyingi sana za pesa Taaslimu zinatoka katika bajeti ipi?

kuhusu Ridhiwani, pia naomba kufahamu jenini nafasi yake katika Katiba yetu, kwani utasikia mara ameitwa Magu kwenye Harambee, je zile ahadi anazotoa kama kununua tenki la maji pesa ni za kwake au? na je mualiko wake unakuwa kama wa Ridhiwani au kama mtoto wa Rais? Na kama mwaliko ni wa mtoto wa Rais, je gharama za safari na Pe rdierm zinalipwa na nani?
CHONDE CHONDE NAOMBA WENYE UELEWA KATIKA HAYO MAMBO AYAWEKE HAPA TUYAJADILI, Kwani hata Marais wote waliopita walikuwa na Familia zao lakini sina kumbukumbu kama nao familia zao zilikuwa na ziara kama hii Familia ya sasa, ndiyo maana NAULIZA, NINI NAFASI NA MAJUKUMU YA FIRST LADY NA WATOTO WA RAIS KATIKA KATIBA YETU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA?

C
 
Kwa kweli watoto, wake, wazazi, kaka, dada, ndugu na marafiki wa mfanyakazi yeyote katika nchi yetu hawana haki wala wajibu wowote unaohusiana na kazi ya mtu. Raisi si tofauti katika hili.

Vitu ambavyo wanaweza kufanya au kufanyiwa ni vile vinavyohusiana na kwamba kijamii raisi ataendelea kuishi na familia/jamii yake sawa na kabla hajawa raisi. Baba yake ataweza kumtembelea Ikulu. Mke wake ataweza kuwa naye nyumbani/chumbani anapoishi na kulala. Watakula pamoja, kusindikizana kama Raisi na hata mkewe (au mmewe ikiwa Raisi ni mwanamke) anasafari. Watoto watapewa huduma na Raisi sawa akiwa si Raisi. Ikiwa wanakwenda shule ya kutwa watapewa pesa ya dadadala na wanaweza kupelekwa na gari la baba au mama yao kwenda shule.

Wanafamilia ya raisi si sehemu ya Uraisi. Hawastahili kupata taarifa yoyote na wafanyakazi walio chini ya Raisi kama Waziri mkuu, mawaziri, maafisa nk. Mke wa Raisi akipewa taarifa ya mpishi wao kama chakula kimeiva ni sawa kwani kila familia yenye mhudumu wa nyumbani wanafamilia wanaweza kupewa taarifa, sio lazima baba tu.
 
Nashukuru kwa majibu yenu wanaJF, Lakini swali langu la msingi ni Je hizo gharama wanazotumia hasa katika ziara zao nyingi zinatoka kwenye bajeti ipi?
 
Nashukuru kwa majibu yenu wanaJF, Lakini swali langu la msingi ni Je hizo gharama wanazotumia hasa katika ziara zao nyingi zinatoka kwenye bajeti ipi?
bajeti ya hela yako mfukoni unayolipia kodi.
 
Kwa kuwa kipindi hiki nchi inaongozwa kisanii, basi lolote linawezekana,
Ila ktk katiba yetu chakavu, mke na watoto wa rais hawatambuliwi,
Gharama za shughuli zao mikoani wanapaswa kujilipia kutoka mifuko yao,
Lakini nimesema awali utashangaa kusikia gharama hizo zote zinalipwa na serikali, kinyume cha katiba
 
Back
Top Bottom