Swali lisilojibiwa: Ndege ya Qatar iliwezaje kutua KIA?

Sina shaka kwamba ndege hiyo ilifuata taratibu za kuingia nchini, hivyo ilikuwa pale kihalali. Tatizo naloliona ni aliyetoa kibali hicho cha ndege kubwa ya kijeshi kama hiyo kuingia na kutua nchini alizingatia vigezo vipi? kwa kuwa alipaswa kutilia shaka maombi hayo na kuinyima kibali kama kweli anafanya kazi yake kwa kuzingatia sheria, utaratibu na common sense pia.Kwa kuwa mtoa kibali hakutumia common sense ana wajibu wa kutujibu watanzania kwa nini hakutumia common sense, na tuanzie hapo kuwakamata wahusika wote. Pili, wizara yetu ya mambo ya nje isikae kimya kama ilivyokaa kimya kuhusu suala hili, huu ni mgogoro wa kidiplomasia pia, hivyo lazima itoe kauli na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuhitaji twiga hao warudishwe nchini mara moja, na waarabu wote waliokodishwa viunga vya wanyama loliondo mikataba yao isitishwe mara moja na wote wafukuzwe nchini mara moja. Kama hatua zote hizi hazichukuliwi basi kwa kutumia common sense nitakuwa sina budi kuamini kwamba viongozi wajuu wa serikali ni wahusika wakubwa wa wizi huu, na wale ambao wamefikishwa mahakamani ni dagaa tu, kambale wapo nje huru.

Hebu tuache kumung'unya maneno, tatizo la Tanzania ni kuwa watu ambao wamechukua madaraka ya nchi ni wale ambao kama wangekuwa nchi nyingine yoyote duniani wangekuwa sio kada ya viongozi bali ni organized criminals ambao wengi wao wangekuwa jela na wapo kwenye list za watu hatari wa nchi hizo.

We are so unfortunate kwamba watu wa namna hiyo ndio viongozi katika nchi inayoitwa Tanzania. Tanzania tuna majambazi, wahujumu uchumi, wauaji ambao ndio walioshika dola.

I am still optimistic kwamba ipo siku wao au generations zao watalipa haya wanayowafanyia watanzania.
 
Hiyo ndio serikali ya CCM iliyojaa wezi wa raslimali za nchi,na hiyo kesi itapotelea hewani na hao wanyama harudi hata mmoja
 
Kila kitu kinajibika ila naona tunajadili newspaper article ambo ilikuwa poorly written

Hakuna basic facts na imekuwa kama mtego vile wa waandishi kutaka kupima akili za wana JF

Unless watu wa WANYAMAPORI na UTALIII na JESHI LA POLISI watoe statement lakini hii kujadili newspaper article iliyoandikwa na huyu mwandishi anayeoonekana kama vile anaandika news kwenye gazeti la Primary school is just beyond ridiculous

Hutaweza kututoa kwenye mada magamba wewe!
 
Huyo jamaa atakuwa ni mwalimu wa shule za uandishi wa habari!! ndo maana anacriticise!
Sijui alitaka facts gani?

Huyo sio mwalimu wa shule za uandishi wa habari, huyo ni mtetezi wa serikali ya magamba, most likely ni mneemeka wa uozo wa CCM.
 
Kama kawaida, Faru alipopigwa risasi na pembe kuondoka Serengeti waliokamatwa walikuwa maafisa wanyamapori wetu, hapa utaona maofisa wetu toka ngazi za juu serikalini wamehusika....Kisa.....mbona R1 anachukua, kila mtu sasa anachukua mali maana hazina mwenyewe...tuliowapa nchi wanakula kuku kwa pozi
 
je nikweli ndege ya jeshi iliagizwa nchini kwa nguvu ipi?mana huwezi tua katika nchi yoyote duniani na kutekeleza uhalifu pasipokuwepo mkono wa mwenye nchi. Je ni kweli wale watuhumiwa ndio hasa waliokula njama za kutorosha nyara izo pasipokuwepo watu wazito {vigogo} nyuma yao? Mi nadhani kuna siri ambayo ipo Nyuma ya hawa wanaotuhumiwa.
Wakati mwingine nashindwa kuamini kama hii figure ni halisi yaani dola 113,715 ndio watu wote hawa ,viongozi mbalimbali wa serikali na nafasi zao ,elimu yao,kuaminiwa kwao,wanaweza kufanya mesheni ya hela ndogo hivyo.shame on you.
 
its just a start,tanzanian you have to be prepared to move out from that country,nadhani mpaka siku muambiwe haya jameni taifa lote limeuzwa na nyinyi mmenunuliwa so ama muhame au mtaishi under control(ukoloni mamboleo) ndio mutaamka usingizini. Rais alienda doha akavalishwa bling bling kama obama sasa kila analoambiwa hewala,na si ndo huko alisema anaweza kuwapa waaarabu ardhi kwa miaka 99? Sasa hapo mnashangaa nini? Labda hao waarabu wamechukua wanyama toka kwenye ardhi waliyopewa na m k w e r e kwa miaka 99. Kama mnabisha kaanzisheni kesi kama ile ya dowans kisha muishie kulipa faini. Mwenzenu nimewahi kuchukua uraia wa malawi kabla mambo hayajawa mabaya zaidi
 
Kama CCM wakipewa muda zaidi kuitawala nchii hii, Tanzania itakuwa mufilisi! Wakubwa wooote walijua ujio wa dege hili na sababu ya kuja kwake. Wakatoa baraka zao.

Na huyo mhindi wa pakistani achunguzwe nyumba yake! Tuanzie hapo.

Usalama wa taifa wamegawanyika: Wazawa(wazalendo), wa mafisadi, na wale wa Mwang'onda. Hawa wazalendo wamezidiwa. Haya makundi mawili yanashirikiana kwa karibu mno.

wakubwa wangejua hilo mambo yangeenda vizuri na wala wewe hungesikia hiyo habari. mind you habari imetoka baada ya hao jamaa kukamatwa na kupelekwa mahakamani
 
Kikwete and ccm is just more than a joke. Hivi hizi hasira tulizonazo hatuwezi kuzifanyia kazi na tuwe creative kufanya mapinduzi ya haraka haraka? Kweli nimefikia wakati nimepita kiwango cha kuchoka na sijui nitumie maneno gani leo au kesho kuhusu watu kama kikwete, usalama wa taifa, jeshi la polisi na hata hawa vibwengo wanachama wa ccm Tanzania. Is Tanzania the worse nation in the world? Kwanini kikwete alimkamata Mbowe na kumpeleka Arusha kwa ndege ya jeshi na kumchukulia hizi costs na security ya ajabu wakati wahujumu Taifa letu wanafanya wanavyotaka? Hivi kikwete anatudharau kiasi gani? Nitarud tena siku nyingine na sasa niende kujiandaa na jamaa zangu na mipango mingine ya kuwaondoa ccm serikalini.

Ushahuri kwa jeshi la polisi na wananchi wengine serikalini chagueni kusaidia Taifa na sio utajiri wa haraka haraka kuliumiza Taifa, Kwa kifupi kataeni orders za kikwete na mafisadi period...
 
Hata kama ndege ilikuwa na kibali ninajiuliza ndege ya kijeshi itue tu bila vyombo vya ulinzi na usalama kujua! sasa kuna sababu gani ya kumkamata lady Jaydee akiwa kwenye mavazi yanayofanana na kombati. Ndege ya JWTZ inaweza kupeleka mahindi Kenya bila ya diplomatic procedure!! Nwy

Kuna ndege ilianguka Arusha na jeshi likasema halikuwa na taarifa, watu walipo hoji wakaambiwa tume ya kijeshi imeundwa hadi leo hatujui matokeo. Kuna kitu kinaitwa meremeta tulipohoji tukaambiwa ni masuala nyeti ya usalama. Kuna mabomu mbagala/Gombs tulipopiga kelele waliohusika wamejiundia tume licha ile ya kwanza. Sijui hili tutaambiwa nini .
Halafu kuna mpakistani ana nyumba yenye uzio mrefu, mhh inanikumbusha Abotabad

Hakuna shoka linalokata bila mpini, Qatar sidhani wanatatizo kwetu, si BAE walivunja hazina wakaondoka na makasha ya pesa kwa kushirikiana na mwanasheria mkuu, sasa hapa tunashangaa nini kama wanyama wanaoishi porini wakibebwa tu.
Ninaposoma habari kama hii natamani ningekuwa mchina, maana watu wangechezea shaba na bili kwa familia.
Wataminywa zile sehemu nyeti askari pori na wapagazi kama sehemu ya kafara lakini mikono iliyoshika deal, ah! haiandikiki kwa herufi ndogo.
 
Siku nyingine wataingiza nchini wapiganaji wakujitoa mhanga na silaha mabomu na mazagazaga mengine,wanaweza hata kuiangamiza nchi ikiwa mtindo huu utaendelea,haiingii akilini sehemu kama KIA kwenye maafisa usalama lukuki tukio kama hili limetokea,inawezekana hata wao walishiriki katika uchafu huu.
 
Kwa kuleta hii kesi mahakamani, serikali imekiri kuwa kuna ndege iliingia nchini aidha kwa kufuata sheria au kinyume cha sheria.

Lakini ingekuwa ni ndege ya kiraia hilo lingekuwa kashfa tosha lakini kuwa ni ndege ya kijeshi ni kashfa mabayo kama waandishi wetu wangekuwa na ujasiri wangetaka maelezo toka JWTZ.. muone watu wanavyoweza kujiuma uma meno!! Hii ni kashfa kubwa kweli ambayo Dr. Hussein Mwinyi anatakiwa aitolee maelezo.

Hussein Mwinyi huwa anajisikiaje kila balaa kwenye nchi hii yanamuhusu lakini anatulia bilia kuwajibika?Au ndo ubashiri kwamba anaandaliwa kugombea urais?Atakuwa Rais wa bora liende kama sasa!
 
Duu hii michango hapa jamvini inazidi kunitia kichefuchefu kwani watu wanatoa vitu vya ukweli ambavyo watanzania tunafanyiwa na viongozi wetu kama vile sisi wote ni mazuzu.ENOUGH IS ENOUGH somebody must GO NOW!!!!!!!!!!!
 
Si waibe halafu walie hapa hapa nchini...lazima wapeleke huko nje yanchi?? nimeshangazwa na vibwengo fulani hapa wanauliza maswali ya kipuuzi kweli, yaani nchi yako inaibwa rasilimali wewe unaongea ujinga
 
Kwanini unadhani hivyo? hivi hujui kuwa kuna ndege zimewahi kabisa kuwa documented kuingia na kutoka nchini bila vyombo vyetu kujua?

nakubaliana na wewe kabisa inawezekana jeshi hawakuwa na taarifa. mimi kila nikikumbuka yale mabomu ya gongo la mboto ndiyo nachoka kabisa na hilo jeshi, kwa jinsi yalivyoaanza yale mabomu hakuna aliyejua kwamba yalikuwa yakilipukia kambini, ingewezekana kuwa tunalipuliwa, kilichonichosha mimi inakuwaje kanali mzima wa jeshi hakupata taarifa ya hayo mabomu mpaka asubuhi alipohamka, mimi sijui huko nchi zilizoendele kanali ana nafasi hipi, lakini hapa kwetu tanzania kanali wa jeshi ni mtu mkubwa sana na ilipaswa hawe na taarifa ya yale mabomu toka yalipoanza. so sishangai jeshi kutokuwa na taarifa ya mdege wa jeshi uliokuja kuiba wanyama
 
Back
Top Bottom