Swali la w/end . . . !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali la w/end . . . !!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Aug 31, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Najua wengi mlio na familia mtakua mnapanga namna ya kuifurahia w/end yenu kwa wale mtakaopata muda wa kufanya hivyo.Wacha leo niwaulize swali hili;Hivi itakuaje pale umefika nyumbani akaja mwanao kisha akakuita kwa jina lako kisha akakusalimu bila kutamka baba au mama,mfano AshaDii au Dark City shikamoo,utachukia?Kama ni ndiyo,kwanini uchukie wakati hilo ni JINA LAKO?Si ndo utambulisho wako?Kama unadhani kutokukuheshimu,kwani heshima iko kwenye jina?Kabla hujaanza kuwaza kama akili yangu ina matatizo,hebu jiulize heshima hasa ni kitu gani na kama inahusiana na jina.Hebu leo tuache kufikiri kimazoea angalau kidogo!!Najua unaweza kushangaa sana,lakini huo mshangao wako ni kutokana na kuaminishwa na jamii kuwa heshima iko kwenye vitu au sifa kama vile,mheshimiwa,bosi,mama,baba,dada,kaka n.k.Hebu nipe mtazamo wako na usipate hasira na kutoa povu kisa mwanao leo kakuita jina lako na kukusalimu!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu nadhani umekichanganya kwenye hii mada pengine ndicho kinabeba muktadha mzima wa neno 'heshima'..Na kitu chenyewe ni Jamii na hayo unayoita mazoea. Mazoea hayaji tu kama mvua lazima yanakuwa na 'backed up' na maisha ya Jamii husika. Jamii ndio inayoamua nini kikisemwa kitakuwa tusi na nini kikisemwa kitakuwa heshima..Unaweza kwenda kinyume na jamii kwa siku moja lakini huwezi kuishi kwenye jamii ile ile kila siku huku wewe ukienda kinyume na jamii inavyosema na kufikiri.

  Mwanangu kuniita Jina langu inaweza kuwa 'heshima mbaya' kwa jamii ambazo zimeamua au zinaona hilo jambo ni dharau. Ni sawa tu shuleni kumuita mwalimu kwa jina lake ilhali wewe ni mwanafunzi wake. Lakini kama 'familia' mnaweza kuwa na utaratibu wenu ambao mmeamua kuufuata na kama mnaweza kuufanya bila kuathiri mitazamo ya wanajamii wengine basi inaweza kuwa sawa kwa mimi mwanangu kuniita tu 'wewe snowball nenda nyumbani unaitwa na mama'..
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  SnowBall,hivi unadhani tusi ni nini?Mpaka liwe "tusi " ni wewe ulione hivyo,na utaliona hivyo kutokana na tafsiri ya jamii,je ni tusi kweli?Chukulia kwa mfano kuna ukoo wa kichaga una jina linalofanana na kiungo cha uzazi cha kiume,hebu fikiri ni kwanini wanavyoitana hawajisikii "vibaya"?Utagundua hapa tatizo liko vichwani na sio kwenye hali halisi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Unajua ukisema tatizo liko vichwani na sio hali halisi utakuwa unakoroga mambo. Tafsiri ya maneno kuwa 'tusi' au 'salaam' huitoi wewe au mimi as individuals. Naomba hapa tukubaliane tu kwa sababu hata Ukisema neno flani kwa kichaga ni 'salaam' lakini kwa kiswahili ni 'tusi' unakuwa umechanganya mitazamo ya jamii mbili katika jambo moja.

  Wachaga ni kabila na ni jamii pia..ukiishi uchagani ni tofauti na kuishi unyamwezini..kuna mambo ambayo yanaweza kushabihiana in common na mengine yakapishana katika maana zake. Na hii ni kawaida sana na inatokea sehemu nyingi tu. Tatizo litakuja kama wachaga na wanyamwezi wataamua kuishi katika mazingira mamoja lazima watengeneze utamaduni ambao uta'compromise' tofauti zao na kujenga commonness..

  Kwa hiyo inakuwa rahisi tu mchaga akizungumza kiswahili kuwasiliana na mnyamwezi lazima kuzingatia istilahi za kiswahili ambazo zinakuwa na connotation ambayo huyo anayeongea naye anaweza kumwelewa. Vinginevyo kama tutashindwa kuwa na common principles za kuendesha maisha..basi maisha yatakuwa magumu manake utaniambia tusi na mimi ntajua ni salaam..tutafika wapi????
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  yaani mwanangu aniite Kongosho???

  Kuna wakati ataniita hivyo for fun tukiwa tunataniana lakini sio wakati anani-address siriaz.

  Kila kundi la wanajamii wana jinsi ya kuonyesha heshima hizo, jinsi ya kumuita mtu ni mojawapo ya kuonesha heshima.

  Kuna wakati nilifanya kazi na mtu wa nchi fulani, siku ya kwanza nilitoka povu, kisa aliniita kwa kidole kinachofuata kidole gumba huku kijanga cha mkono kimetazama juu. Niliona ni dharau sana, lakini yeye akasema ndio wanavyoita kwao na hakumaanisha dharau.

  Kwa hiyo, nitajali mwanangu kuniita kwa jina maana heshima inajumuisha jinsi ya kumuita mtu kulingana na tamaduni za kundi husika.
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  SnowBall,wachaga ni jamii na waswahili je?Ni jamii nyingine?Hebu nijibu kwanza hili!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Kongosho bana,hauna tofauti na sisi wanajamii wengine.Tumeaminishwa heshima iko kwenye majina au vitu na sio kwenye utu.Upofu huu utatutesa sana maishani!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  huo utu wewe umeaminishwa na nani??

  Huoni upofu huo wa utu utakutesa?

  Unajua 'machiavellian principle'?

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 80
  Nakubaliana nawe mkuu snowball....unastahili kuitwa Great Thinker.
   
 10. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna kitu kama hiki. Mambo yote yanazunguka katika namna jamii inavyoyachukulia hususan mambo ya kijamii.
   
 11. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Yes wachaga ni jamii kamili kwa maana wana lugha zao, mila zao na tamaduni zao zinazoeleweka..Haliakdhalika waswahili ni jamii mtambuka inayojumuisha jamii ndogondogo na wachaga wakiwemo..Kwa hiyo wachaga wanapoishi kama waswahili lazima waishi kwa taratibu za kiswahili!!!
   
 12. S

  Smarty JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  Nitamwambia kuwa....,,Maadili ya dini hayaruhusu kuwaita wazazi wako kwa majina yao ya kuzaliwa...,,hapo nadhani ataelewa
   
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Unatumia muktadha upi kusema huu ni upofu??
  Tamaduni za zamani zitakufa tu pale utamaduni mpya utakapoibuka..ila huwezi kusema mazoea yaliyopo ni upofu!!!
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  What????An by the way,where were u?
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hiyo machiavellian itakuelezea vizuri, kwa hiyo kama ni upofu hata utu ni upofu wa mazoea tu.

  Kifupi wanaamini 'the end justify means'

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  SnowBall,nilitaka uone na kujiuliza inakuaje watu wale wale,lakini chini ya kivuli cha jamii wanaliona neno moja katika sura mbili tofauti.Yaani chini ya kivuli cha uchaga neno linakua halina shida,lakini mtu yuleyule kwa kivuli cha uswahili neno lile lile linaleta tabu?Kwani ukiamua kutokulipa tafsiri yoyote neno hilo itakuaje?Huoni tatizo lipo vichwani zaidi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Kwanini usifafanue?Maana hueleweki unaposema utu ni upofu!
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Ni pale tunaposhindwa kung'amua kuwa heshima ya binadam ni utu na sio sifa,kwani sifa mbaya au nzuri ni kutokana na jamii na haina lolote kwenye uhalisi!
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  machiavellian principle inasema morals consideration are irrelevant to matters of state.

  Kama hawa wanaona morals hazina maana kwa then hata utu ni upofu kama ilivyo heshima katika jinsi ya kuita mtu.


   
Loading...