Swali la w/end:Kwani ni lazima upige makelele??

Swali la w/end:Kwani ni lazima upige makelele??

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Ni muda tu mfupi uliopita hapa "kijiweni" zimepita gari mbili zimepambwa huku honi zikipigwa nikajiuliza ni kitu gani hiki ndo jamaa yangu akaniambia ni harusi hiyo
'
Nikashangaa kisha nikajiuliza maswali
'
Hivi watu wakioana ni lazima wapite barabarani wakipiga makelele?
'
Ni kitu gani kinawafa watu wapige makelele kwenye misafara ya harusi?
'
Kuna mabilioni ya watu walishafunga ndoa sasa cha ajabu nini
'
Hivi kuoana ni jambo la ajabu kiasi hiki?
 
ni mzuka tu, na furaha iliyowajaa wapendwa wao kuona wakifunga ndoa. sioni tatizo katika hili.
 
ni mzuka tu, na furaha iliyowajaa wapendwa wao kuona wakifunga ndoa. sioni tatizo katika hili.

Furaha gani?Cha ajabu kipi mpaka upige makelele barabarani?
 
Kwani ni lazima kwa wapendanao wawapo kwenye mahaba yao chumbani wawili wapunguze sauti??
 
kuna tofauti ya kelele na furaha za shangwe, kwenye harusi hakuna kelele ila shangwe
Ni muda tu mfupi uliopita hapa "kijiweni" zimepita gari mbili zimepambwa huku honi zikipigwa nikajiuliza ni kitu gani hiki ndo jamaa yangu akaniambia ni harusi hiyo
'
Nikashangaa kisha nikajiuliza maswali
'
Hivi watu wakioana ni lazima wapite barabarani wakipiga makelele?
'
Ni kitu gani kinawafa watu wapige makelele kwenye misafara ya harusi?
'
Kuna mabilioni ya watu walishafunga ndoa sasa cha ajabu nini
'
Hivi kuoana ni jambo la ajabu kiasi hiki?
 
makoyo hebu nipe hizo tofauti!
 
Last edited by a moderator:
Furaha gani?Cha ajabu kipi mpaka upige makelele barabarani?
kama hujaolewa, siku ukiolewa utajua jinsi gani furaha unayokuwa nayo.unaweza kufanya kitu cha ajab mpaka ukashaanga siku ukionesha video ya harusi yako..,

ila kuna wengine wanakodisha matarumbeta na bendi ili kuikoleza harusi. acha wafurahi bhana, we kama wanakukera ziba masikio..
 
zimwimtu wanaoolewa halafu wakapiga makelele wana matatizo ya akili
'
Kwanini uoe/olewa ume kama mwendawazimu wa kupiga kelele hovyo?
'
Siku nikioa hata nzi alieko ndani mwangu hatajua achilia mbali watu wa barabarani!
 
Last edited by a moderator:
vipi mdau kwani ni lazima msafara wa msiba kukaa kimya? watu wengi wameshafariki ni nini cha ajabu?
 
Ni mbwembwe tu hizo mkuu za mafuraah na mshawasha! Na ndo maana kuna tofauti kati ya harusi na msiba! Aririririririririiiiii! Dada huyooo! Anaolewa!..
 
vipi mdau kwani ni lazima msafara wa msiba kukaa kimya? watu wengi wameshafariki ni nini cha ajabu?

Ulishawahi kufika mahali pana ONYO la kutokukaa kimya?Ni kipi kinachokera kati ya kelele na ukimya?
 
Ni mbwembwe tu hizo mkuu za mafuraah na mshawasha! Na ndo maana kuna tofauti kati ya harusi na msiba! Aririririririririiiiii! Dada huyooo! Anaolewa!..

Na ipi tofauti kati ya wehu na wenye akili timam?Kati ya mwehu na mwenye utimam wa akili ni yupi mwenye sifaya kupiga kelele?
 
Ulishawahi kufika mahali pana ONYO la kutokukaa kimya?Ni kipi kinachokera kati ya kelele na ukimya?[/QUOTE

inategemea na mahali na wakati. kelele zaweza kuwa nzuri au mbaya! kimya chaweza kuwa kizuri au kibaya! wewe umeoa au umeolewa? vipi harusi yako ikawa kimya toka church hadi ukumbini? utajisikiaje? au wasemea kelele za barabarani ila za ukumbini hazina shida?
 
Mi naona poa tu cz ni jambo la kheri na lenye furaha. Acha wafurahi cz ni siku yao.
 
anhaaa mi nilifikiri wanapiga kelel kweye ndoa,kumbe kwenye harusi!
 
Back
Top Bottom