Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,739
- 40,864
Hili ni swali ambalo linahitaji majibu. Seif Sharrif Hamad (pichani) amekuwa katika ulingo wa siasa za Zanzibar kwa miaka mingi sasa. Tangu akiwa Waziri Kiongozi na kuja kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Ameona mengi na bila ya shaka na ni kweli kabisa mtu hawezi kuandika historia ya Zanzibar kwa usahihi na kwa haki bila kumtaja Seif Hamad.
Lakini siasa za Zanzibar zimekuwa bora kwa sababu yake? Je, bila yeye siasa za Zanzibar zingechukua mweleko upi? Je, akiondoka kushiriki katika siasa hizo nani atachukua nafasi yake? Tunaweza kuona watakuwa bora kuliko yeye au watashindwa kuvaa viatu vyake?
NI swali ambalo pia linaweza kuulizwa kuhusiana na Seif na CUF; je bila yeye CUF itakuwa na mwelekeo gani? Je, ameifikisha alipotaka na watu walipotarajia?
Hili ni swali la ugomvi katika baadhi tu ya sehemu zake.