Swali la kizushi kwa Dr Slaa, Mbowe, Mnyika, Mkumbo na Wanachadema

Mbona jibu ni rahisi jamani??? Kama wananchi wa zanzibar wameamua hivo chama chochote chenye staha kikishinda au kuwa cha pili kitashiriki kuunda serikali huko... ILA KWA STAHA ILEILE HAKITAJARIBU KULAZIMISHA KUUNGANA NA CHAMA TOFAUTI CHENYE HAKI KISHERIA/KANUNI ZA BUNGE KUUNDA KUB...
 
Shukran sana na hongera kwa kuweza kuusoma ujumbe/swali na kulielewa, lakini kwa bahati mbaya mie si mzanzibar na kama ningekuwa Mzanzibar basi ningechukua hilo jukumu.

Kuna swali tangu jana linaniumiza kichwa nalo ni hivi ni kweli CUF wana shirikiana kuendesha Serikali ya SMZ na CCM na huu ni uasi je kwa nini CDM kuendesha Halmashauri na CCM ambapo wamepata viti sawa si uasi? Sina jibu na najua hakuna wa kuweza kunijibu. Ushauri wangu ni kuwa vyama ambavyo ni vya upinzani lazima vishirikiane ili kuweza kuleta ushindani wa kweli ila hali ikiwa kama CDM wanavyotaka basi ndoto ya kufika kwenye Tanzania yenye neema itakuwa imekufa na kuzikwa rasmi.

Chadema waliishaizika! tunasema haya tunaonekana maadui au wazanzibar!!!! tumeni jazeni mapost yenu humu ya kulikoa taifa hili, ila kwa matendo ya CDM wamekataa kuiondoa CCM madarakani, huu ndio ukweli.
 
Umoja ni nguvu....needless to say it.

Lakini kwa mazingira haya ya kimahusiano na kutokuaminiana miongoni mwa opposition parties, umoja wa KWELI ni feasible?
I personally dont think so....I think utakuwa ni UMOJA wa kupendezesha kurasa za magazeti na screens za runinga tu, huku core yake ikibakia kuwa UNAFIKI.

Na unafiki ni time bomb!
 
Shukran sana na hongera kwa kuweza kuusoma ujumbe/swali na kulielewa, lakini kwa bahati mbaya mie si mzanzibar na kama ningekuwa Mzanzibar basi ningechukua hilo jukumu.

Kuna swali tangu jana linaniumiza kichwa nalo ni hivi ni kweli CUF wana shirikiana kuendesha Serikali ya SMZ na CCM na huu ni uasi je kwa nini CDM kuendesha Halmashauri na CCM ambapo wamepata viti sawa si uasi? Sina jibu na najua hakuna wa kuweza kunijibu. Ushauri wangu ni kuwa vyama ambavyo ni vya upinzani lazima vishirikiane ili kuweza kuleta ushindani wa kweli ila hali ikiwa kama CDM wanavyotaka basi ndoto ya kufika kwenye Tanzania yenye neema itakuwa imekufa na kuzikwa rasmi.

Mohamed,
Jibu la swali lako lilishatolewa tangu mwanzo, sijaelewa unataka nini zaidi, ama lasivyo unataka upewe jibu unalolitaka wewe. Naanza kuamini kwamba katika hili unabisha ili tu uendeleze mjadala usiokuwa na tija kwa kuwa ukweli uko bayana.
Ushirikiano kati ya cdm na ccm kuendesha halmashauri ya manispaa kigoma ulikuja baada ya uchaguzi. Kwa maana kwamba baada ya uchaguzi vyama vyote viwili vilikuwa na idadi sawa ya madiwani.Kwahiyo walikubaliana kuendesha halmashauri kwa kupokezan, kila chama miaka miwili na nusu. Hakukuwepo na suala la mayor atoke cdm na naibu wake atoke ccm ama vise versa. Kila chama kilipomaliza ngwe yake kilikaa pembeni na chama chengine kikachukua usukani.
Lakini kwa zanzibar ni tofauti. Kulikuwa na makubaliano kabla ya uchaguzi. Katiba ilirekebishwa na ikaweka utaratibu wa kuunda serikali.
Sasahivi Rais wa smz anatoka ccm, makamu wa kwanza wa rais anatoka cuf, kwahiyo wanafanya kazi kwa pamoja ndani ya serikali moja. Maalim seif wa cuf hawajagawana vipindi vya kuongoza na Dr.shein wa ccm, wanapiga mzigo pamoja na wataendelea kuiongoza serikali moja hadi 2015.Kigoma hawakuongoza halamshauri kwa pamoja, waligawana vipindi, hilo nalo gumu kuliona?Yani huwezi kuiruhusu akili yako ikaona hiyo tofauti?
Kwa sababu kama sio matakwa ya katiba ya zanzibar bado ccm walikuwa wanaweza kuunda smz kama walivyofanya miaka yote. Dr.shein alimshinda maalim seif kwahiyo alistahili kuunda serikali, hawakupata idadi sawa ya kura, na ndio maana katiba imesema chama kitakachopata 5% basi kishirikishwe kuunda serikali, katiba haijasema chama kitakachopata 50%ndo kishirikishwe kuunda serikali.Kwahiyo suala la kigoma liko tofauti kabisa, vyama viwili vya cdm na ccm vililingana idadi ya wapiga kura 50% kwa 50%, yani hata busara ya kawaida haikusaidii kuliona hilo?
Suala la kushirikiana kwa vyama ni muhimu lakini sio lazima, kunakuwepo na ushirikiano kama kuna tija lakini kama hakuna tija, bora kila chama kipigane kivyake.Inajulikana jinsi ccm inavyohujumu vyama vya upinzani vyenye ushawishi mkubwa katika jamii yetu wala huitaji kulibishia kama unafuatilia vizuri siasa zetu za tanzania. Kwahiyo kama chama kinahisi kunaweza kutokea hujuma kwa kutoa nafasi ya ushirikiano na chama kingine ni lazima kichukue jukumu la kujihadhari na kitakuwa tayari kuusimamia uamuzi wao na hata kama kutakuwa na madhara basi kitabeba msalaba. Lazima mnafika mahali mnafanya uamuzi na kuwa tayari kuusimamia na mnakuwa tayari kubeba maslaba, vinginevyo tutabaki tunalilia muungano wa vyama usiokuwa na tija kwa wananchi na hata ustawi wa vyama vyenyewe.
 
Kaka bado wanachama wa CDM wanakwepa maswali??

Majibu yametolewa mengi sana hapa toka kwa watu mbalimbali, wanachadema na wasio wanachadema.
Lakini huyu muungwana inaonekana ana majibu yake mwenyewe anayotaka kuyasikia, kwahiyo muda wote anabisha tu hata palipo na facts yeye anabisha tu, labda anataka kuendelea kujaza page kwa kurudia maswli yale yale kwa majibu yale yale, na kwa staili hii mjadala mzima utapoteza mwelekeo na hakuna la mkujifunza litakalopatikana hapa.
 
Kwa ufupi na ufasaha kabisa hata huo ushirikiano wa CUF na CCM ulikuja si baada ya uchaguzi no ulikuja baada ya chaguzi tatu yaani ya 1995, 2000 na 2010. Na wala sina haja ya kuzozana na mtu ni kuwa wengine hawasomi yaliyopita wanaendeleza kuuliza yaliyokwisha kujibiwa ndio maana kuna kuwa kujirudia rudia hii imenifanya nivumilie kwa maana uelewa wako wewe ni tofauti na yule wangu ni tofauti na wako hivyo hivyo kwa kila mtu. Kila mmoja wetu ana uwezo wake wa kuchambua mambo. Kunyamaza wengine wanachukulia ni dharau lakini wewe unakemea eti unaendeleza mjadala. Nisamehe lakini elewa sina nia mbaya na wala simpigii mtu upatu hapa.
 
USITAFUTE HESHIMA KWA KUUZA DHARAU. Ili nisionekane nimeuza dharau nakuachia wewe huu mjadala kwa yeyetote atakae uliza umjibu majibu yako unayoyajua wewe.

I am done
 
Take it easy mzalendo.
Ukizira namna hii ina maana labda hata hukuwa umefanya anticipative analysis of the eventualities za kuanzisha thread yenye topic ya aina hii.

Sisi kule mtaani kwetu uswahilini tunasemaga "umelikoroga, ulinywe"!
 
Kwa ufupi na ufasaha kabisa hata huo ushirikiano wa CUF na CCM ulikuja si baada ya uchaguzi no ulikuja baada ya chaguzi tatu yaani ya 1995, 2000 na 2010. Na wala sina haja ya kuzozana na mtu ni kuwa wengine hawasomi yaliyopita wanaendeleza kuuliza yaliyokwisha kujibiwa ndio maana kuna kuwa kujirudia rudia hii imenifanya nivumilie kwa maana uelewa wako wewe ni tofauti na yule wangu ni tofauti na wako hivyo hivyo kwa kila mtu. Kila mmoja wetu ana uwezo wake wa kuchambua mambo. Kunyamaza wengine wanachukulia ni dharau lakini wewe unakemea eti unaendeleza mjadala. Nisamehe lakini elewa sina nia mbaya na wala simpigii mtu upatu hapa.

Mohamed,ninakusoma vizuri sana.
Nadhani tunapishana sehemu ndogo sana, pamoja na ukweli kwamba uelewa wa mtu na mtu unatofautiana lakini kuna kiwango fulani lazima frequency zinalingana.
Ni kweli muafaka wa zanzibar ulikuja baada ya chaguzi tatu, kwahiyo baada ya kuona mivutano na minyukano iliyokuwepo kwa vipindi vyote huko kabla ndo mahasimu wawili wakuu wa siasa za zanzibar wakaamua kukubaliana kabla ya uchaguzi wa nne kwamba waendesheje nchi baada ya uchaguzi, ndipo ikazaliwa SUK zanzibar. Kwahiyo hiyo baada ya uchaguzi wa 2010 tayari utaratibu ulishaelezwa na katiba ni kipi cha kufanya na ndipo maalim seif na dr.shein wakaunda serikali ya pamoja.

Sasa tofauti na kigoma, hata kama walikubaliana baada ya uchaguzi wa 2005 na kwa mantiki yako ya baada ya chaguzi tatu ukirefer zanzibar, hakukuwepo na makubaliano kabla ya uchaguzi wa 2005 namna ya kuendesha halmashauri hiyo pamoja na kwamba tangu 1995 walikuwa wanafanya uchaguzi na cdm na ccm wanakabana koo kweli kweli.Hapa hakukuwa na katiba wala sheria iliyotoa mwongozo. Na hata baada ya vyama vya cdm na ccm kukubaliana namna ya kuiendesha halmashauri ya kigoma hawakubadili katiba, sheria wala kanuni za serikali za mitaa ili waendelee kushirikiana. Utaona kwamba walikubaliana kila chama kiongoze kwa miaka miwili na nusu. Na ulipowadia uchaguzi mwingine kila mtu ametafuta ushindi akijua kwamba mshindi ndiye atakayeongoza halmashauri. Kwakuwa hawajalingana kura mwaka huu basi cdm amechukua halamashauri.Kwahiyo unaona ukweli ni kwamba muundo wa uendeshaji wa halamashauri ya manispaa ya kigoma 2005-2010 ni tofauti kabisa na muundo wa SUK ya zanzibar. Nadhani hushindwi kuiona hiyo tofauti na kiungwana tunakubaliana tunaendelea na mengine ambayo hayajajibiwa kama bado yapo.
Kutofautiana kimtazamo ni suala la kawaida lakini baada ya kuchanga mawazo hapa na pale mwishowe ukweli unabainika na kuheshimiwa.Kwahiyo hakuna kuzozana, tunajadiliana hadi inafika mahali tunauona ukweli kutokea kwenye angle moja.
 
USITAFUTE HESHIMA KWA KUUZA DHARAU. Ili nisionekane nimeuza dharau nakuachia wewe huu mjadala kwa yeyetote atakae uliza umjibu majibu yako unayoyajua wewe.

I am done

Mohamed, umeanza mjadala vizuri lakini sasa unataka kuumaliza vibaya.
Pamoja na kwamba ninajibu majibu ninayoyajua mimi lakini kila mmoja anajibu majibu anayoyajua yeye.
Hizi tofauti za majibu yetu ndizo zinaleta changamoto kwenye vicha vyetu, lakini hatimaye tunafika mahala tunapata majibu ya kweli na tunakubaliana pasipo kujali kwamba yametoka kwa nani, manake hapa ni kueleweshana na kujadiliana kwa hoja na sio kutafuta mshindi.

Kama hiyo maneno imekukwaza, ninasikitika kwa hilo kwakuwa sijakulenga wewe lakini usikate tamaa, we endelea kujadiliana na wananchi hapa kwa amani na upendo.
 
KAMA ULIVYO SEMA KIONGOZI MASWALI YAKO YA KIZUSHI, NA WEWE MWENYEWE MZUSHI

Upande wa ZNZ kuna mengi, kwanza ni dhana takatifu iliyojengeka kwamba wa ZNZ wanakandamizwa, binafsi yangu naona tena kuwepo kwa ZNZ ni kikwazo kimojawapo kwa CDM kushika utawala mapema, kuna irudisha nyumba CDM kwanza hakuna haja ya kuweka concentration ya hali ya juu mahali ambapo mnapokewa kwa kiac kidogo sana, nanyi mnatafuta kushika dola, ki mcjakato ikibidi mipango hiyo ije mara tu baada yakuwa CDM imeshika dola, kwa sasa wakihangaika na ZNZ ambayo haitaki mahesabu makuuubwa ya formular upokezi wake c mkubwa.
 
Madhumuni ya vyama vyetu sio kuwatumikia wananchi? kama ndio sioni ubaya kunyang'anyana fito wakati wote wanajenga nyumba moja! TAFAKARI....

Well, sasa kwanini tunataka vyama vingi wakati tunaweza kuungana kuwatumikia wananchi?!!!!
 
Nadhani hapo nisema maneno machache yatakayo kujibu maswali yako yote, je CDM ina wabunge wangapi znz? ina wawakilishi wangapi znz? ikiwa ina uwakilishi ndani ya visiwa vya unguja na pemba na CDM ikawekwa pembeni basi walichokifanya CCM na CUF ni ushenzi wa kisasa na uchoyo wa posho za vikao.

Tuje bara, CUF ina wabunge wawili mmoja ni mlemavu wa ngozi hii inamaana gani? CUF ina uwakilishi ndani ya Tanzania bara!!!! sidhani kama inahitaji mtu awe na degree kulitambua hili.

Sijui una maana CUF inauwakilishi gani bara!, mimi nijuavyo CUF ina wabunge zaidi ya 10 hata kama wanatoka Zanzibar, lakini wana uwakilishi ndani ya bunge na maamuzi yao yanawagusa sana Wabara zaidi kuliko Wazanzibar.
Hata kama Chadema haipo Zanzibar, ninachosema ni kuwa CUF wamekuwa wanafanya mambo yao bila kuwashirikisha wenzao, ni wabinafsi. Vikao vya Makamba na Seif vilikuwa Dar, Seif alipoombwa kuwashirikisha hata Jahazi asilia japo, aligoma. Mohamed, kushirikiana na mtu usiyejua kuwa ni ndege au mnyama ni hatari sana. Aduihatari si mwenye silaha bali Mnafiki.
Nimekuuliza swali hujajibu, hivi kwanini CUF waligombea kuunda opposition camp hata kama walijua fika kuwa chadema ndio wenye majority in opposition? Sasa wanataka kurudi kushirikiana na Chadema kwa lipi. Fafanua tafadhali
 
Back
Top Bottom