Swali la haja kwenu wana MMU

RAGNAR LOTH

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
698
1,589
Dhana ya nzi kufia kwenye kidonda ni Utaahira/ Mapenzi / Uhaba wa vidume, wanawake/ Uvumilivu / Ushika dini kupindukia / Kutojiamini ama ni nini?

Ushawahi kukutana na familia/ uhusiano uliogubikwa na ugomvi na migogoro isiyoisha?

Yumkini mwanamume ndiye chanzo ama mwanamke ndiye chanzo cha maugomvi yasiyoisha kila siku lkn unakuta bado wako pamoja. Unakuta kidada kizuri kimejikondea kwa mawazo na manung'uniko yasiyoisha. Ama jamaa kaisha hadi tunamshangaa kijiweni kisa mikasa ya mahusiano. Kupenda kupo lkn sio kila kitu katika maisha, Mapenzi ni sehemu tu ya maisha, dhana ya maisha sio mapenzi pekee wanandugu.

Kwa mtazamo wangu : Jifunzeni kuyapa kisogo baadhi ya mambo ktk maisha, Jifunzeni kuanza upya ktk baadhi ya mambo, Mkubali kushindwa ktk baadhi ya mambo. Acheni kufunika nyota zetu zising'are kwa kukumbatia yanayokurudisheni nyuma kwa sababu tu neno mapenzi lilishakuepo

Wangapi waliamua kuacha yaende ? Hutakua wa kwanza ktk ulimwengu, wengi walishafanya. Waliachana na vizingiki wakaanza upya wakafika mbali ktk kila affair kwenye maisha yao.

Siwashawishi mvunje mahusiano yenu lkn ikibidi kufanya hivyo ongeeni na dhamiri zenu ziwasaidie kufanya maamuzi.

Mtalia sana, mtatembea sana kwa waganga kuwabadili wenzi wenu, mtasubiri sana wenzi wenu wabadilike, mtawawekea vikao 100 kidogo, If he/she is not to change you'll end up getting stuck in the dark of despair, sorrow, and pain till we burry you.

Learn to let some things go in life.
 
Ngoja wenye Uzoefu na changamoto waje.

Binafsi Niko Tanga line Sina hayo majanga.

Asante sana Tanga, Kwa kuwa sehemu ya Tanzania.
 
Tanga line ni mkoa. Ukioa huko hakuna stress.

Acha hizo porojo.

Kama umeoa huko nako, ukubali kufa maskini. Wanawake wa huko wanawaza kuvaa chupi gani yenye mvuto kwa mumewe hakuna thinking out of the box
 
Kama umeoa huko nako, ukubali kufa maskini. Wanawake wa huko wanawaza kuvaa chupi gani yenye mvuto kwa mumewe hakuna thinking out of the box

Kwanza, mimi siyo maskini naelekea kwenye mabilioniers.

Kwa hiyo utakuwa unakosea sana unapodhania hivyo ila ni akili yako labda na uliyekutana naye /uliokutana nao.

Japo, pichu nzuri ya mke ni sehemu ya kufanya ndoa kuwa nzuri na imara Btw, mimi humnunulia nyingi sana na nzuri. Kwa hiyo, ni kawaida kabisa.

Tanga, raha Aiseeeeeeeh.
 
Utakuwa unakosea sana unapodhania hivyo ila ni akili yako labda na uliyekutana naye /uliokutana nao.

Japo, pichu nzuri ya mke ni sehemu ya kufanya ndoa kuwa nzuri na imara Btw, mimi humnunulia nyingi sana na nzuri. Kwa hiyo, ni kawaida kabisa.

Tanga, raha Aiseeeeeeeh.

Hhahahah na wewe bwana akili yako ilishatekwa na hao watanga. Nimemaanisha zaidi ya nilichoandika, usinijudge kwa mfano wa chupi peke yake. Namaanisha wanawake wa pande zile kwenye kufikiri nje ya box kwa minajili ya utafutaji wako nyuma sio kwa kupenda, la hashaa ila ni kwa sababu ya mila na desturi zao. Huwezi kumlinganisha mtanga na mchaga( mkaskazini), au msukuma( kanda ya ziwani kule).Wale kutokana na mila zao wanakua ni watafutaji by nature
 
Ndiyo maana nikaandika kuwa, labda uliyekuwanaye au uliowahi kuwaona.

Siyo kweli kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza.
 
Kweli leo akili yako iko nzima wew jamaa... Nakujua vizuri sana usingeweza kuandika vitu kama hivi, kistaarabu namna hii... Hali yako imetengemaa leo..!!
 
Back
Top Bottom