Swali la fasihi msaada tafadhal

dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
2,038
3,124
Habari wana lugha

Fasihi haitokani na ombwe bali ni matokeo ya uzoefu wa mwandishi..Ni kwa vipi kauli hii imeridhiwa na waandishi wa tamthiliya mbili ulizozisoma..

Naomba kufahamisha Maana Ya Neno Ombwe Lilivyotumika katika swali hilo?
Na je swali lina hitaji nn?
 
Mimi ni mwalimu wa kiswahili,ilo swali linajibiwa kwa kuangalia mambo yote yanayomzunguka mwandishi akiwa kama maana jamii kifupi unajadili dhamira kwenye vitabu husika
 
Mimi ni mwalimu wa kiswahili,ilo swali linajibiwa kwa kuangalia mambo yote yanayomzunguka mwandishi akiwa kama maana jamii kifupi unajadili dhamira kwenye vitabu husika

Asante mkuu
 
Ombwe ni nihil. Nothing. Kutokuweko na kitu. Kwa maana nyingine unaambiwa kuwa fasihi haitokei katika nothing/ombwe/utupu bali kwa namna moja au nyingine inatokana na mambo ambayo mwandishi ameyaona na kuyashuhudia katika maisha yake na jamii inayomzunguka kisiasa, kijamii, kitamaduni. Ndiyo maana ukisoma kazi ya kifasihi utajua tu kuwa hii ni fasihi ya Kimarekani, Kicuba, Kikenya, Kitanzania n.k. kwa sababu mwandishi ameathirika na Jamii yake na athari hizi lazima zijitokeze katika kazi zake za kifasihi. Hebu jiulize, kwa mfano, kitabu hiki kingekuwaje kama kingeandikwa na mwandishi kutoka Rwanda au Ushelisheli?

Tafuta hizo tamthilia na elezea jinsi zinavyoakisi hali halisi ya jamii inayomzunguka mwandishi. Na wakati mwingine athari hizi zinaweza kuonekana katika vitu vya kawaida tu kimazingira mf. Vitabu vingi vya Kezilahabi utakutana na dhana ya duara kwa sababu anatoka kisiwani Ukerewe ambacho kimezungukwa na Ziwa kubwa...

Umepata angalau fununu?
 
Ombwe kwa Kiingereza ni "Vacuum". Ni kweli kuwa fasihi haitokani ombe(kitu tupu/hewa) bali inatokana na mambo kadhaa yanayomsukuma Mwandishi kuiandikia jamii yake ili kuielimisha, kuionya na kuiasa, kuiadibu, kuifurahisha nk. Mwandishi hupata habari kwenye magazeti, kuona, misibani, matembezini, vilabuni nk. na kupata kung'amua mengi kama vile yaliyo kwenye KILIO CHETU; Athari za mapenzi, Tiba kwa wenye UKIMWI, Athari za marafiki, Dhana potofu. Hivyo basi, hilo swali linahitaji DHAMIRA.
 
Ombwe kwa Kiingereza ni "Vacuum". Ni kweli kuwa fasihi haitokani na ombwe(kitu tupu/hewa) bali inatokana na mambo kadhaa yanayomsukuma Mwandishi kuiandikia jamii yake ili kuielimisha, kuionya na kuiasa, kuiadibu, kuifurahisha nk. Mwandishi hupata habari kwenye magazeti, kuona, misibani, matembezini, vilabuni nk. na kupata kung'amua mengi kama vile yaliyo kwenye KILIO CHETU; Athari za mapenzi, Tiba kwa wenye UKIMWI, Athari za marafiki, Dhana potofu. Hivyo basi, hilo swali linahitaji DHAMIRA.
 
Back
Top Bottom