Swali kwenu warembo kuhusu nywele

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Hivi warembo mbona mnapenda urembo wa nywele bandia? Hamjui kuwa wanaume wengi tunapenda urembo wa nywele hasa asilia? Na je huyu msichana ana nywele asilia ama bandia na nitagunduaje nywele badia ama asilia?

attachment.php
 

Attachments

  • DSC_0599.JPG
    DSC_0599.JPG
    74.7 KB · Views: 1,073
Nywele bandia zinajulikana tu,kwanza si natural(hope unaelewa coz na ww unanywele),pili ukimshika mtu kichwani utaona kuna milima na mabonde kama kashonea weaving utajua lkn pia nowdaiz wana bond,mtu aliebond ni ngum kujua sema tu utaona nywele ndefu lkn laini sana tofauti na nywele asilia.Kwamfano zangu hapo ni natural you can tel frm the bandia ones.
 
Hivi warembo mbona mnapenda urembo wa nywele bandia? Hamjui kuwa wanaume wengi tunapenda urembo wa nywele hasa asilia? Na je huyu msichana ana nywele asilia ama bandia na nitagunduaje nywele badia ama asilia?

attachment.php
sasa hata tofauti yake huijui unalalama nini?
 
Huyu ana nywele za bandia maana zake za asili zinaonekana zilipoishia.
 
El Toro, Urembo kwa mwanamke ni kitu namba moja kabisa, ni sifa ya pekee kwa mwanamke kuwa mrembo, hii inajumuisha ngozi, mavazi na hizo nyewele unazosema, So kuweka nywele za bandia ni sehemu ya urembo, maana wengine wanaufinyu wa nywele kabisa vichwani, wanaongezea (wiving, raster or wigs) kuongeza urembo na mvuto..
Na vile vile utashi wa wanaume unatofautiana... KUna wanaopenda nywele zozote iwe za bandia au natural ilimradi dada aonekane smart.. na wapo kweli wanaopenda natural hair( nafikiri wewe ndo mmoja wapo)
So kiufupi, nywele ni sehemu ya urembo na fashion pia kwa wakina dada/mama
Kumtambua inahitaji:
1- ufahamu nature ya nywele zake, kama ana kipilipili then unamuona na long hair obviously atakuwa ameweka bandia
2- ukimshika kichwani ndani ya nywele ana matuta matuta ya kushonea
3. Uwingi wa nywele zenyewe, mara nyingi hizi za bandia zinakuwa nyingi, ndefu na zenye kushine (ingawa wasioweza kuzitunza na zile za bei rahisi utafikiri mkia wa ng'ombe


Kwa ufupi
 
....tafuta na angalia documentary ya Chris Rock inayoitwa "Good Hair" utapata picha nzuri sana ya biashara nzima ya nywele za bandia............
 
Dada zetu waache kuhangaika na nywele bandia jaribuni kuwa natural tu mbona flaviana matata huwa ypo bomba tu na kpara chake, i realy like real the African queen
 
kuna tofauti kati ya uzuri na urembo. uzuri ni kipawa cha Mungu lakini urembo ni sanaa. kusema kila kitu katika sanaa ya urembo ni kibaya na/au kinabore siyo fair, na pia kusema weaving/rasta peke yake katika sanaa ya urembo ndivyo vinavyoudhi/kubore na ukkaacha vingine nayo siyo fair. kila mtu na taste yake, nawajua wanaume wengi tu wanaofurahia urembo aina kwa aina ikiwamo huo wa weaving/rasta. binafsi huwa naweka na kutoa inategemeana siku hiyo najisikia kufanya nini. haya mambo ni ya fashion tu huja na kupita
 
MJ you are right,

Lakini kwa wengi wetu nywele bandia kwa kweli zinatupa shida sana. I personally, naheshimu urembo na haki ya mtu kufanya apendavyo awe mrembo. Lakini kwa nywele bandia niko biased I dont appreciate them. Though again, ni vema kuheshimu haki ya mhusika. I aint married, but that I bet would be my one of those small things I am likely to ask my partner to deal with... Basi ukishindwa kuvumilia..weka hata rasta basi..? harafu ukute sasa ndo mtu kaweka that called (wigi) kama la mh. fulani mkulu wa bunge...It just puts you off....

I have loooong admired mama/Prof. Tibaijuka and her hair do! Its just incredible.....I hope warembo wetu humu watajifunza kidogo..
 
binafsi mimi ni conservative yaani sipendi mawigi ya wanawake kabisa, hata yale yenye mwonekano wa afro hair, nayaona bado hayajaweza kufidia nywele za asili. sipendi wanavyokuwa artificial, .hawako real kabisa kwenye sekta nzima ya urembo. kiukweli utafiti wangu unaonyesha wanawake wanavutiwa na wanaume mwenye urembo wa asili kama ambavyo wanaume wengi tunavyopenda kuuona urembo wa asili wa mwanamke kwani ni hapo tunapojaribu kukisia hata aina ya mtoto na sura yake itakavyokuwa iwapo tutazaa na mwanamke huyo. lakini cha ajabu wao wanatabia ya kujichakachua mpaka wanachukiza. nachukia nywele za kununua, pia siamini kama kuna wanaume wanazipenda labda nionavyo mimi ni kuwa wanaume wanaweza kutumia gia hiyo kumsifia mdada wakati wanamtongoza tu.binafsi nimeona ukichunguza vizuri harusi nyingi zinazofanyika wanawake huwa hawapendezi kabisa lakini wanaume wanaonekana watanashati. pia nywele zinazowekwa black ikazidi inaondoa ile natural color ya nywele kiasi inaonekana haina mvuto tena na artificial in looking. nachukia napoona mwanamke hawezi kuegemea ukuta kwa hofu anachafua ukuta kwa nywele zake kisa ni kalkiti zenye lundo la mafuta yasioeleweka yamepakwa ulinda nywele.
 
duh!urembo sio kitu kibaya,bt inategemea na huo urembo,coz kuna wadada wengine kiukweli dah!wanazidisha!
..km mi cpendi nywele bandia kabisa n i don use to!
...styl ziko nyingi sana mbona za kufanya uonekane mrembo bila hata kuweka hayo madude kichwani?basi suka rasta!
 
Ndio imekuwa fashion kwa sasa dunia nzima ata mastaa wengi wa nje zile si nywele zao..nilibahatika kuwa personal butler wa beyonce na rihana kwa wakati tofauti hapa dubai...bila hizi make up na nywele bandia wanawezakupita sehemu yoyote bila ata kujulikana ni picha na shooting ndio zinazowaweka juu lakini face to face without make up ni kawaida sanaa
 
Back
Top Bottom