Swali kwa Wizara ya Utumishi; Je ni haki kuajiri Watumishi wa Mikataba kwa muda mrefu bila kupandishwa mishahara?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,079
49,786
Niulize Swali Kwa Waziri wa Utumishi na Serikali Kwa Ujumla..

Kumezuka Utaratibu wa Serikali kuajiri Watumishi Kwa mikataba Kwa ajira rasmi kabisa na Mingi ya hiyo mikataba inakuwa ni renewable..

Imekuwa kawaida Sasa Mtumishi aliyeajiriwa Kwa Mkataba kukaa kwenye hiyo Ajira ambayo ni renewable Kwa Zaidi ya miaka 5 nk..

Cha kushangaza na kusikitisha licha ya hao Watumishi kufanya kazi zile zile wanazofanya Watumishi wa kudumu ila wamekuwa hawabadilishiwa salary zao hata baada ya Serikali kupandisha Mishahara ya ngazi zao na Wala hawapandi Madaraja kama Watumishi wa kudumu..

Sio sawa na sio Haki Kwa sababu kuwa muajiriwa wa Mkataba inakuaje tena iwe ndio njia ya kunyanyasa Watumishi wasio wa kudumu?

Unakuta mtu aliajiriwa na salary ya 200,000 ameendelea ku renew hiyo kazi Hadi anafikisha umri wa kustaafu bila ya salary yake kubadilika.Nadhani hii sio sawa.

Ni vyema Serikali ikaliangalia hili suala kwamba kama unaendelea kumhitaji huyo Mtumishi zaidi basi aendane na wengine wa kudumu Kwa sababu status yake Kwa kwamba usipomhitaji utamuachisha kazi..

Kuna Taasisi kama TanRoads,Tarura,Tanesco nk Wana utaratibu wa Ajira Serikali iangalie hili jambo upya maana Ajira za mkataba ziko rasmi kabisa Serikalini lakini Kwa nini noble job ya Serikali itumike kumnyanyasa mtumishi wa mkataba Kwa sababu tuu hana Ajira ya kudumu?

Mwisho ,huyu huyu mtumishi wa Mkataba anakatwa makato yote rasmi kama mtumishi wa kudumu na Cha ajabu wakisitishiwa Ajira zao , taratibu za malipo ya pension ni zile zile kama za Mtumishi wa kudumu.

Nitoe wito Kwa Serikali iwajali Watumishi wake wa Mikataba na wanapositishiwa mikataba ,malipo Yao ya pension wapewe yote Kwa mara Moja badala ya kuwa kwenye terms kama za Watumishi wa kudumu,ikibidi Fao la kujitoa au kupoteza kazi walipwe Chao.
 
Back
Top Bottom