swali kwa Wakristo

swali kwa Wakristo

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
2,101
Reaction score
5,442
Mfano mtu ameoa ana wake watano na wote kazaa nao, akaamua kuwa Mkristo hao wake zake inabidi awape taraka au? Maana si ndoa ya Kristo ni ya mke mmoja/
 
Katika hao wake mmoja wa ndo ndie atakae tambulika hasahasa ni yule wa kwanza wewe ulienza nae kufunga ndoa ila na yeye afuate dini yako
 
Nini kitatokea kwa hao wengine aliobaki?
 
Ukihamia kwa wakristo utafuata utaratibu wa kikristo (na kinyume chake pia)......huyo inabidi aanze upya, aibariki ndoa kikristo ili ampate mke halali mmoja wa ndoa ya kikristo, hao wengine atakuwa anazini nao kama ataendelea nao.
 
Hakuna kitakacho tokea ila anaetambulika kidini ni huyo wa kwanza ilieanza kufunga nae ndoa hata sisi wakristo kuna wenye wake zaidi ya wawili na kuendelea ila kidini anaetambulika ni yule wa kwanza tuj hao wengine ni kujishereheshea tuu na watoto wanahesabika wote kama umezaa nao.
Kwa mfano ukifa hua wanasema marehemu kaacha watoto labda kumi au kuendelea hata kama mke wa kwanza ulizaa na mmoja na wake wengine ukazaa nao watoto wengi
 
Sasa hao wake wengine ataendela kushirikiana nao kimwili au lah! na kama akiendelea atakuwa anafanya zinaa au hapana na kama ni ndiyo si kuwanyima haki hao wanawake
 
Ukihamia kwa wakristo utafuata utaratibu wa kikristo (na kinyume chake pia)......huyo inabidi aanze upya, aibariki ndoa kikristo ili ampate mke halali mmoja wa ndoa ya kikristo, hao wengine atakuwa anazini nao kama ataendelea nao.
Si kuwaonea mkuu kwa maana itakuwa kama kawazalisha then kawatosa
 
Sasa hao wake wengine ataendela kushirikiana nao kimwili au lah! na kama akiendelea atakuwa anafanya zinaa au hapana na kama ni ndiyo si kuwanyima haki hao wanawake
Hiyo inahesabika ni zinaa maana tayari mke wa ndoa unae
 
Hilo swali sio kwa wakristo bali ni kwa waislam ambao wanaruhusu ndoa za mitala..

Waulize je mtu akibadili dini hao wanawake wenginr inakuaje?
 
Mfano mtu ameoa ana wake watano na wote kazaa nao, akaamua kuwa Mkristo hao wake zake inabidi awape taraka au? Maana si ndoa ya Kristo ni ya mke mmoja/

Hakuna sheria kwenye ukristo inayozuia mtu asioe wake wengi isipokuwa kwa Padri au askofu. Hayo mengine ni mapokeo tuu ya watu. Oa kama unauwezo hata wafike mia ni wewe tuu
 
Hiyo inahesabika ni zinaa maana tayari mke wa ndoa unae
Hii Mimi nimeishudia kuna shehe alikua na wake wanne akaamua kuokoka akaacha na uislam. Na akaambiwa afunge ndoa Mpya ya kikristo akawapa talaka hawa watatu akaoa mmoja wa kwanza wake na mpaka leo yupo nae na hao wengine waliendelea na kudanga
 
Hilo swali sio kwa wakristo bali ni kwa waislam ambao wanaruhusu ndoa za mitala..

Waulize je mtu akibadili dini hao wanawake wenginr inakuaje?

Ukishabadili dini au kuritadi uislam hauna jukumu na ww isipokuwa kama utaleta fitina katika dini hukumu yako ni kuuliwa
 
Hilo swali sio kwa wakristo bali ni kwa waislam ambao wanaruhusu ndoa za mitala..

Waulize je mtu akibadili dini hao wanawake wenginr inakuaje?
Jaribu kuelewa swali.

1. Uislamu hakuna ndoa ya wake watano kama alivyouliza.

2. Pia swali liko sahihi..kwa maana anataka kujua hatima ya hizo ndoa endapo atabadili dini..hivyo jibu sahihi inabidi litoke kule kunakotarajiwa kuhamia.
 
kuna taratibu na amri.
wakristo kila dhehebu wana taratibu zao. ila amri ni zile zile 10.

sasa iko hivi ajitathmini yy mwenyewe, kwenye hizo amri 10, akiona anatosha ndio aje na taratibu za dhehebu husika.

kwa maana hamuwez kuwa kanisa kwa kutegemea amri 10 tu, hapana mtapanga na taratibu zingne
mfano~ muda wa ibada, namna ya kutoa zaka na kiasi, utovu wa nidhamu n.k ambazo zinaweza kupelekea hata kupewa adhabu au hata kusimamisha ushirika wako kwenye kanisa hilo licha ya kwamba unatimiza amri zote kumi

NB:hawezi kuwepo mtu wa kushika amri zote kumi aje ashindwe taratibu za dhehebu husika.
 
Hilo swali sio kwa wakristo bali ni kwa waislam ambao wanaruhusu ndoa za mitala..

Waulize je mtu akibadili dini hao wanawake wenginr inakuaje?
Akibadili dini kutoka kwenye Uislamu si atafuata taratibu na kanuni za hiyo dini aliyohamia? Kama hawaruhusu mke zaidi ya mmoja haliwezi kua ni suala litakalojibiwa na Uislam tena

Ama ungeuliza kama mtu ana wake watano na anataka kuingia kwenye Uislam na katika sheria za dini ya kiislam ndoa mwisho ni wake wanne tu itakuaje?

Uislamu hamung'unyi maneno itabidi amuache mke mmoja katika hao kama atavyochagua yeye mwenyewe(sio lazima kwamba abaki na yule wa mwanzo) na kisha abaki na wake wanne tu kwa wakati mmoja
 
Nitoke nje ya mada kidogo..

Kama unaruhusiwa kuoa zaidi ya mmoja kwanini upewe limit kuwa nne ndio mwisho?

Si bora uoe tu idadi unayotaka as long as ni zaidi ya mmoja!
 
Ni suala la sheria, taratibu na kanuni mkuu kama ambavyo dini zingine zinasema strict mmoja mpaka kufa

Kuhusu nini ilikua hekima ya kuruhusu hadi wake wanne kwa wakati mmoja kuna hoja zake kama ambavyo dini zisizoruhusu zaidi ya mke mmoja zina hoja zake
 
Katika hao wake mmoja wa ndo ndie atakae tambulika hasahasa ni yule wa kwanza wewe ulienza nae kufunga ndoa ila na yeye afuate dini yako
Si lazima afuate dini yako mkuu. Kanisa katoliki linaruhusu mpaka muislamu kumuoa mkataloki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom