Swali kwa Mhe. Rais: Umesema kila Mbunge wa jimbo afanyie mikutano kwenye jimbo lake je Bashiri Ally na Hamphery Polepole ni wabunge wa jimbo gani?

Nitajie tu ukurasa unaonesha hivyo, ninayo hapa hapa mkuu!
Kwa ufupi hua ni hivi, hakuna raisi kutoka ccm aliyetekeleza ILANI ya uchaguzi kwenye kipindi chake cha kwanza cause yeye hua sio part ya team inayo andaa ILANI hiyo, Mkapa alilalamika hadharani mwaka 1997 kwamba ILANI ile ilikua haitekelezeki, haikuzungumzia chochote kuhusu barabara yeye akakomaa na mabarabara nk, mwaka 2006 JK nae aliilalamikia ILANi yake ya mwaka 2005 tena akiwa kanisani na hasa kuhusu ile kitu inaitwa Kadhi wa Waislamu na akasema kabisa yeye hakua member we team ilio andaa ilani ile so hata hi, mambo ya ndege, Stigles Gorge (sina hakika kama nimepatia spelling) na hayo mafly over sijui nini, hayapo mle.
Kwenye ilani ya CCM hakuna kujenga uwanja wa ndege chato, kununua ndege,kujenga flyover wala Stieglers Gorge..
 
kama kunakitu huwa simuelewi jiwe,ni kua kila ipodaiwa demokrasia yeye hukumbilia moja kwa moja kusema demokrasia sio maandamano.

kwamba yeye kuandamana tuu ndio tafsiri ya demokrasia?,yani eti analalamika kwamba akiruhusu mikutano anaogopa matusi na kejeli,utadhani chama chake hua hawatoi hizo kejeli kwa upinzani.

na hivi alichokisema bashite juu ya ukichaa wa lissu tena mbele ya jiwe zile kwake ndo siasa za kistaarabu anazo zitamani?
 
kama kunakitu huwa simuelewi jiwe,ni kua kila ipodaiwa demokrasia yeye hukumbilia moja kwa moja kusema demokrasia sio maandamano.

kwamba yeye kuandamana tuu ndio tafsiri ya demokrasia?,yani eti analalamika kwamba akiruhusu mikutano anaogopa matusi na kejeli,utadhani chama chake hua hawatoi hizo kejeli kwa upinzani.

na hivi alichokisema bashite juu ya ukichaa wa lissu tena mbele ya jiwe zile kwake ndo siasa za kistaarabu anazo zitamani?

Mkuu kumbe umeona, huwa analazimisha eti watu wakifanya mikutano watatukana. Analazimisha hilo neno kutukana na maandamano ili kutoa uhalali wa hayo makatazo yake mfu. Ki Ukweli hataki vyama vingine vifanye mikutano hasa cdm kwani anajua kina ushawishi hivyo ili kisiwe na nguvu ni kukinyima uwanja wa kukutana na watu.
 
Mod Naomba Msiunganishe Thread hii inaumuhimu wake maana nimaswali yanayoulizwa

Ndugu wadau leo kuna swali ambalo tunategemea majibu kutoka kwa Mhe Rais

Tumeona katimu Mkuu wa chama cha mapinduzi akitembea kila mkoa kwenye mikutano ya ndani na hadharani pamoja na katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi Hephrey Polepole lakini hakuna anayesema, kuwagusa wala kuwakemea. Watu wote na viongozi wote wapo kimya kama hakuna kinachoendelea.

Kwenye upande wa pili wa chama cha Upinzani Tanzania Chadema Katibu wake Mkuu Vicent Mashinji akiwa kwenye vikao vya ndani vya chama chake tumeona anavyokamatwa na polisi na kuzuiwa pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho kikubwa hapa nchini

Swali

1)Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Mwenezi wa ccm Polepole wao niwabunge wa Jimbo gani na Chama Gani? je Tunamuongopea Mungu au Binadamu? Je Tundu Antipas Mugwai Lissu akiambia Dunia kuwa hakuna Demokrasia Tanzania anakosa gani? Je umeshangamua kuwa Dunia sasa hivi nikijiji kila ukifanyacho kinaonekana nisawa na kila Ukipandacho ndio utakachovuna?

2) Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi, watendaji wa kata na watarafa hao wote niwanachama na viongozi wa ccm bahadhi je hawatoshi huko majimboni mpaka hao wawili polepole na Bashiru wazunguke je hizi si fujo kwenye majimbo yawapinzani?

Mfano uliyo hai: Tukumbuke Mbunge wa Jimbo hili ni Godbless J. Lema je hizi si fujo jimboni kwa Lema ambapo ccm wanaleta?

Ndugu Denis Zakariah Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha akisikiliza kero za wafanyabiashara wa soko la kilombero leo .Hapa kazi tu.
View attachment 1003365
Naogopa watanisema na sina ngozi ngumu kama aloshawahi kusema Mwakyembe kwa wanasiasa wawe nayo.
 
Ni udikteta tu, hamna lolote. Sasa tukirudi nyuma mbona katiba haisemi hayo ya kuzuia mikutano ya hadhara hadi sijui siku ya uchaguzi.

Je, vyama visivyo na madiwani au wabunge wao watapataje wanachama wapya au watauzaje chama chao. Haya ndio miongoni mwa mambo yanayomfanya Magufuli asiende hata hapo Kenya tu kwa kuogopa maswali ya waandishi wa habari.
 
Dr Bashiru na Polepole ni wajibu wao kuzunguka,kwa sababu chama chao ndio kinaongoza serikali,ni lazima wahakikishe ilani ya chama inatekelezwa kama chama kilivyoahidi,sasa Mashinji azunguke anakagua nn kwa mfano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa waungwana hawana majukumu ya kitaifa. Wanasahau kuwa Bashiru ni msaidizi mkuu wa Rais katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama, ambayo ndio inayosimamia uendeshaji mzima wa nchi.
 
Naamini wewe Mwanahabari Huru ni mtu makini tena uko vizuri katika uchambuzi wa masuala ya kisiasa. Lakini nikushangae kama hutambui kuwa Serikali iliyoko madarakani ni ya CCM na hivyo basi viongozi wake kutembelea sehemu mbalimbali za nchi ni kuhakikisha kuwa inatekeleza kwa ukamilifu Ilani yake ya Uchaguzi.

Vivyo hivyo, viongozi wakuu wa vyama vyenye wawakilishi wanawajibika kutembelea maeneo yao kuhakikisha pia kuwa wateule wao wanatekeleza ipasavyo ahadi zao. Kama hawafanyi hivyo, ni udhaifu mkubwa wa uongozi kisiasa. Ila tunawaona muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii au na vyombo vya habari wakiitukana Serikali. Naamini ni kwa sababu hizi ndiyo maana viongozi wateule wao hukiama chama kwa kuwa wanafanya kazi katika hali ya ukiwa.

ITAWAGHARIMU SIKU YA SIKU
Kama katiba inaruhusu Mtanzania kwenda popote pale na kufanya chochote mradi havunji Sheria,vizuri Sheria ikaheshimika sio kauli za mtu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuambia hawa ni viongozi wa kisiasa katika chama kinachoongoza serikali.

Hivyo wanawajibu wa kuzunguka nchi
nzima kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuziwasilisha kwa mwenyekiti na kupanga mikakati ya kuzitatua.

Kwakuwa watatuzi ni viongozi ambao ni wanachamawao, hivyo wanao wajibu wa kufuatilia kama wanatekeleza ahadi walizo toa kwa wananchi kupitia ilani za chaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
vyama vya upinzani vipi kwa mujibu wa sheria na katiba je kwenye katiba niwapi kuna kipengele kuwa vyama pinzani wasifanye siasa mpaka uchaguzi ukikaribia?
 
Hawa waungwana hawana majukumu ya kitaifa. Wanasahau kuwa Bashiru ni msaidizi mkuu wa Rais katika kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama, ambayo ndio inayosimamia uendeshaji mzima wa nchi.
vyama vya upinzani vipi kwa mujibu wa sheria na katiba je kwenye katiba niwapi kuna kipengele kuwa vyama pinzani wasifanye siasa mpaka uchaguzi ukikaribia?
 
Huo ndio ukweli,chama ndio kiliomba ridhaa kwa wananchi,na ilani ilitengenezwa kabla hata mgombea wa urais hajapatikana,hivyo ni wajibu wa chama kuhakikisha inasimamia utekelezaji wake,kwa sababu ni chama ndio kitarudi kwa wananchi kujibu ahadi ilizoziahidi,nimejitahidi kutumia lugha nyepesi unielewe.

Sent using Jamii Forums mobile app

Unanukuu sheria ya vyama vya siasa au unanukuu maneno ya JIWE? Nijibu kwana hapa ndio tuendelee.
 
nani kakwambia wasifanye siasa? kinachozuiliwa ni uzurulaji.
lakini Bashiru na Polepole wao wazurure? Nchi hii inafuata misingi ya Sheria na katiba ni wapi kwenye sheria na katiba kunamnyima mwanasiasa kufanya siasa naomba unuku kipengele hicho
 
2) Mkuu wa wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi, watendaji wa kata na watarafa hao wote niwanachama na viongozi wa ccm bahadhi je hawatoshi huko majimboni mpaka hao wawili polepole na Bashiru wazunguke je hizi si fujo kwenye majimbo yawapinzani?

Hao niliowa bold siyo wanachama. ni Watendaji wa serikali.
 
Back
Top Bottom