Swali: Kuhusu uchongeshaji 'holela' wa mihuri

911

Platinum Member
Aug 22, 2008
852
499
Wasalaam wadau,
nimekaa nikajiuliza sana kuhusu suala la uchongaji wa mihuri unaofanyika hapa Tanzania.Ningeomba wenye ufahamu wanieleweshe kama kuna sheria inayodhibiti uchongaji huu ninaouita holela.Kwani kwa sasa unaweza ukaenda kwa mchonga mihuri ukamwambia kuwa nahitaji muhuri wenye maandishi unayoyataka nae akauchonga bila kukuuliza mara mbili.Sijui katika nchi nyingine jambo hili likoje.
Kilichoamsha ari yangu ya kufahamu haya ni kuwa ilipelekwa bank cheque ya organization flan bank(names withheld) kwa ajili
ya kutoa hela kwenye akaunti ya org hiyo,ila ktk cheque kulikuwa na muhuri wa staff wa hyo org ambaye ni top level manager.Bank wakakataa kutoa hela kwa madai kuwa anayetakiwa kutoa idhini ya kuchukua hela ni manager wa level flani(kwa madai kuwa ndie signatory).Kilichofanyika ni kuwa ukachongwa muhuri unaohtajika then mambo yakawa shwari.Ndipo nikajiuliza kuhusu suala hili la mihuri.
 
Mihuri haina tatizo, hiyo kampuni ichunge check zake kwa uangalifu zaidi.
 
Thanks Kang,
kwahiyo inamaana kama nkipata kuchomoa cheque moja katika cheque book tken naweza kuchonga muhuri na kwenda kuchukua hela.Kwangu mimi hii ni hatari sana...
 
Hapa ni Bongo, chochote kinawezekana, hii ni kutokana na serikali kutosimamia sheria zilizopo kikwelikweli, nina hakika sheria zippo, kutozijua sio excuse ya watu kufanya wanavyotaka.
 
hii ndo bongo kila kitu kinakwenda shaghala baghala ingaweje tuna sheria na taratibu nzuuuri kwenye makabrasha
 
Udhibiti unahitajika toka kwetu sote.

Suala jingine, Je umeshajiuliza vile vibanda vinavyojiita 'music recording centre' ambayo kazi yake ni kuburn kazi za wengine za miziki na video na watu yanauza hizi CD, VCD, DVD's, Cassette n.k waziwazi kila sehemu hasa katika vituo vya mabasi bila kuulizwa na yeyote juu ya hati milki?

Na vipi zile DVD's 'a kichina zinazotembezwa kwenye mabaa ambapo unawezakuta eti kijana anauza the latest movie, hata kabla haijazinduliwa! lakini ndo hivyo hizo picha zenye vichwa virefu kuliko miili au zenye ukungu tunajua zinapotoka, lakini kwa nini wanunuaji tusiwe wakali na kuzisusa na kuelimisha hawa vijana wajasiliamali kuwa wanaweza kufunguliwa mashitaka?
 
Back
Top Bottom