SWALI: Kati ya Shetani na Adamu nani alikuwa wa kwanza kuwepo duniani

Adam alikutana na Lucifer bustani ya eden sio duniani, naomba tuelewane kwanza hadi hapo.


Na kuhusu nani alikuwa wa kwanza hapo bustanini au nani alianza kuwapo kabla ya mwenzake, Lucifer kabla hajawa shetani wa leo, alikuwa ni kiongozi wa malaika wote huko mbinguni. Alikuwa ni malaika mwenye cheo cha juu sana na mkuu wa majeshi ya malaika.

Baada ya kumzingua mshua ndio akanyang'anywa vyeo vyote na kutupiwa katika uvungu wa ardhi na kufungwa minyororo ambayo sasa hivi binadamu kupitia matendo yetu mnamsaidia kila siku kupata nguvu za kuikata hiyo minyororo na kurejea hapa ulimwenguni kufanya uharibifu wake live bila chenga.
 
Lucifer, ndiye anayeitwa Leo shetani baada ya Kufukuzwa mbinguni, alitupwa hapa duniani. Maandiko hayasemi ni muda UPI alitupwa hapa duniani.
Lucifer, ni malaika na malaika ni viumbe walioumbwa na MUNGU kwa kazi mbali mbali. Na kila malaika ana mamlaka na uwezo tofauti na malaika mwingine.
Lucifer ni mmoja wa malaika waliopewa uwezo au daraja la juu miongoni mwa malaika.
Malaika ni kiumbe asiyekuwa na mwili ni roho.
Mwanaadamu ameumbwa kwa daraja bora zaidi (Roho, Mwili na Nafsi).
Jini ni muunganiko wa malaika zaidi ya mmoja. Malaika wawili au zaidi Wanaweza kuunganisha nguvu zao na kuwa malaika mmoja hapo huwezi kuwaita malaika bali ni jini.
Ukiangalia habari ya yule Mtu aliyekuwa akiishi makaburini, Bwana YESU alimwuliza wewe ni nani?. Alijubu kuwa yeye ni jeshi, maana yake malaika wengi.
Na baada ya kuamriwa wamtoke waliomba waruhusiwe kuwavaa nguruwe waliokuwa kundi kubwa zaidi ya mia tatu. Kila nguruwe alivaliwa na malaika na kuangukia majini.
Jini linaitwa jini wakati malaika mmoja ameunganisha nguvu zake na malaika mwingine mmoja au zaidi ya mmoja.
Sifa kubwa ya malaika ni utii na hana machaguo yoyote yale,hivyo huyo shetani hakuwa malaika bali ni kiumbe tu kama viumbe vingine kama majini n k...
 
Kati ya Adam na shetani Wa kwanza kuishi duniani ni Ibilisi(shetani/sheitwan/satan).

Ushahidi ni Qur’an .

Sura ya 76 aya ya 1.

IMG_3935.jpg
 
HII THREAD IMEJAA UONGO SANA .

1. Shetani alikua mkuu wa majeshi ya malaika

2.Jini ni muunganiko wa malaika zaidi ya mmoja

3. Kuna malaika wema na waovu

4.Bustani ya eden ilikuwa inalindwa na malaika

4.shetani alikuwa malaika / mkuu wa malaika/malaika aliye asi

5.Ibilisi ana nguvu, uwezo , akili kushinda binadamu

6.Shetani alitaka kumpindua Mungu

7.Shetani alikuwa anamwimbia Mungu

8. Mungu amemuumba Adam kwa mfano wake

9.Mungu alimkabidhi shetani funguo za peponi

10. Shetani anajua siri karibu zote za Mungu

11.Adam alikuwa anaishi peponi

IMG_3842.jpg
 
Back
Top Bottom