Mwanamena
JF-Expert Member
- Feb 4, 2020
- 1,107
- 1,343
Mkuu, iko hivi, kwanza fahamu kuwa Benki nazo huwa zinakopa.Na kama unasema benki wanategemea pesa za wateja ambazo zinazunguka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
yaani kwa mfano mimi napeleka pesa zangu benki unakopeshwa wewe then unarudisha kwa riba kisha anakopeshwa mwingine na chain inaendelea.
Sasa wanaposema benki imefilisika hizo pesa zinazozunguka zinakuwa zimepotelea wapi?
Sent using Jamii Forums mobile app
Pili benki zinafanya biashara ya kukopesha fedha.
Tatu Benki zina matumizi ya kila siku, ambayo hayazalishi fedha yoyote.(expenditures)
Nne Huwa inatokea wateja kutoweka Sana hela benki husika. Matumizi wakati huo yanaendelea kumbuka.
Kumbuka pia hela ulizoweka benki wewe, Ni Kama umewakopesha.
Hela zinaenda wapi Sasa?
Maingizo ya benki (income) huwa inakuwa ndogo kuliko matumizi, kwanini?
Walioikopa wameshindwa kuilipa benki husika, hata wakiuza Mali za wakopaji hazifidii Deni lote kwa sababu ya Bei husika ya Mali, iliyowekewa dhamana, sokoni. Pia Mara nyingine dhamana huwa haziuziki kabisa, unaweza kudhani watu wameroga.
Hapohapo Waliyoikopesha benki nao wanaidai, benki inavyolipa madeni yake kule hela mnazoweka ndizo zinatumika.
Hapo benki inakuwa Haina hela zenu. Imeenda kulipia Deni. Hapo ndipo utakuta benki Haina watu na ukienda kuchukua hela unaambiwa cash hatuna.
Sometime hazitoshi inabidi ifilisiwe na wakopeshaji wenye dhamana.(Secured creditors)
Wakati wa kuanza kulipa tunaanza Kodi za Serikali.
Kumbuka wewe Ni Kama uliikopesha benki, Ila huna dhamana yoyote.
Imekula kwako tayari.
Kuna mengi hayo Ni machache tu Mkuu.
Sent using Jamii Forums mobile app