Swali; IMESHINDIKANA KUMUENZI NYERERE wa hapa TZ ITAWEZEKANA MANDELA?

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,463
0
Katika mambo aliyokemea kwa nguvu zote enzi za uhai wake mwl. Nyerere ni RUSHWA ambayo kwa sasa ni kama imeshindikana kutokomezwa hapa TZ. Kama hali ni hiyo itawezekana vipi kumuenzi Nelson Mandela wa Afrika kusini kwa kutolipiza visasi na mambo mengine mema aliyoyaacha?
 

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,463
0
Hapa TZ ni ndoto kuwaenzi waasisi wetu mara nyingi tunawaenzi kwa maneno tu.
 

Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
1,677
1,195
Rushwa haikemewi wala kupayuka payuka kuwa rushwa ni mbaya. Yeye nyerere angeweka kifungu katika katiba kuwa raisi lazima ashitakiwe kwa kutumia vibaya madaraka ya uraisi hapo pasingekuwa na rushwa kabisaa. sasa yeyey alianza kukemea, hivyo kila raisi ajaye nyuma yake naye hukemea, hukemea, hukemea mpaka leo inabaki kukemewa tuu na viongozi.

Nchi zote ikiwamo Israel na marekani ambazo maraisi wake hushitakiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake, hazina rushwa kabisaa, kwa nini nyerere hakuiga hilo?

Yeye nyerere alijua fika kuwa kifungu hichi kitamhukumu yeye wa kwanza, kwa kufuta kiingereza mashuleni bila ridhaa ya wananchi, kupeleka watu operesheni vijiji vya ujamaa bila hiari yao,kuwakama kamata watu unemployed na kuwasweka jela miezi mitatu mitatu, kutumia vibaya pesa za umma kwa shughuli za chama tuu na kuleta palestiniai day sherehe ya kutukana wayahudi.

weka kifungu kimhukumucho raisi , halafu uone kama kutakuwa na rushwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom