Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,092
- 43,265
Na. M. M. Mwanakijiji
Wanataka waendelee kututendea kama hawatupendi, lakini wanataka tuwatendee kama tunawapenda. Wamekuwa ni kama yule mwanamke mgomvi ila mrembo. Ukimuona kwa mbali na kwa karibu unaweza kujikuta unasema kama alivyosema Ice Cube na Chris Tucker kwenye ile filamu ya kuchekesha ya "Friday"... Walipojikuta wanamuona Miss Parker.. wakajikuta wameachia midomo wazi na kung'aka "Dayyyymmmnnn!!"
Hawa watu wamekuwa wakitembea kwa mikogo..wakienda wanajitingisha kwa mtindo wa Singida Dodoma. Wanajua tunawaona na tunajua wanatuona. Miendo yao na mapozi yao yana lengo moja nalo ni kutupagaza akili. Kuna watu wanajikuta wako kwenye mahusiano yenye sumu na hawajui watokeje; mwenza anaweza kuwa ni mgovi, mwenye visirani, na anaweza kuwa "abusive" kwa maneno na kwa matendo lakini kuachika haachiki. Akiwa kwa watu unaweza ukadhani na yeye ni mtu. Na mkiwa kwa watu anakufanya na wewe ni mtu. Lakini siri yake unaijua. Mwisho na wewe unajikuta unageuka kuwa mtu wa "kujifanyisha" - a pretender!
Pamoja na mwendo wao wa maringo wanaongeza na mavazi ya mitego, kama wawindaji. Sauti zao wanabana na macho wanarembua na vidole wameinua juu. Lakini haitoshi. Wanajua kulegeza sauti; sauti ambayo inakuta watu kwenye udhaifu wao; wakilegeza wanalegeza kweli kwa ile sauti ambayo wahenga waliita ya "kumtoa nyoka pangoni".. nyoka nyoka pori na bichwa lake hilo!
Wameongeza urembo na mapambo...Hereni na bangiri na lipstick 💄 za kung"ara na kumetameta. Wakikunja miguu mbele yako wanakupiga picha kama alivyofanya mwigizaji Sharon Stone katika filamu ya Basic Instincts; Wanataka mioyo ishtuke. Wanataka wasikie miluzi na sauti za psiii psiii!!
Kitu kimoja hawataki tukizungumzie, tukiwazie, wala kukifikiria juu yao. Kitu hicho hawataki tuwaambie watoto wetu, na hawataki tuwaimbie wana na mabinti zetu. Hawataki tuseme ubaya wao! Tusithubutu kuutaja, kuunyoshea kidole au hata kusema tunataka tuachane nao; tusithubutu! Wataongeza visa na mikasa mwisho wa siku tunasalimu amri. Tukitaka kuwaacha wanasema "kukosea ni ubinadamu"; Hawaombi msamaha; wanasema "kwani nani mkamilifu".
Hawasikii...wanasema ni lazima tuwapende..tuwatake ..na kila wanachosema tuwakubalie...Sasa, tunajiuliza kama ni wazuri hivyo kwanin wanajitahidi sana kujipara na kujishaua? Kuna mtu mmoja alisema kuwa wengine wanatumia vipodozi kufichua uzuri wao lakini wengine huvitumia kuficha ubaya wao. Kwani hujawahi kukutana na mtu kajipodoa hadi ukafikiria ni kitukuu cha shetani!? Yaani, mtu kajipara hadi akajiparua!
Inawezekana mwanamme akamuacha mwanamke mrembo kabisa (kwa kuonekana); mwanamke mwenye wowowo la umbo la kitunguu maji, na matiti ya matikiti maji, mwenye macho ya gololi ya rangi ya njiwa pori! Kila mtu anashangaa - anamuachaje huyu...
Kumbe aliyeonja mboga chunguni anajua ladha yake...au uchachu wake... uzuri wa chungu si utamu wa mboga....
Siku wakijua wameachika .... tutanuniwa sisi na tusipoangalia.....na tusipoangalia....
Tutauliwa sisi...