Swali fikirishi: Ni nini walicho nacho wapinzani wahamao ambacho CCM hawana?

Ukianza kutumia logic and reasoning katika siasa za Africa na ccm hususani hapa Tz, utaumiza kichwa chako bure......hapa hamn itikadi au philosophy, kinacho fuatwa ni swala la kukurupuka na kufurahisha kiongozi mkuu....tabia hiyo hiyo itawasumbua mpaka chama kitapata mpasuko mkumbwa, kwa sababu "what goes round comes round" hamna mwana chama wa CCM wakwelikweli anae weza ku trust Mtatiro au Mtulia nawenzake,
Baada ya miaka 2 hawa wahamiaji watatupwa nje kama kopo la chooni ndipo watakapogundua walifanya kosa kubwa sana ila watakuwa wamechelewa. Time will tell.
 
Jibu ni kwamba CCM kuna vilaza kwa hiyo ili kupata viongozi bora inabidi mkuu asajili toka upinzani. Mfano mzuri ni wale waliotoswa na CCM mwaka 2015 wakahamia upinzani. Baada ya rigorous training waliyoipata wakiwa upinzani na ku graduate with flying colours CCM imewasajili upya kwa dau kubwa kama la Emmanuel Okwi!
 
Baada ya miaka 2 hawa wahamiaji watatupwa nje kama kopo la chooni ndipo watakapogundua walifanya kosa kubwa sana ila watakuwa wamechelewa. Time will tell.
Kwa upande wa kwanza
Kwa upande wa pili, mule ndani (green room) utatokea mtifuano wa wageni na wenyeji
Wanuka maziwa wanajua Ng'ombe mgeni verses Ng'ombe mwenyeji
 
Ni kama umekuwa katika mawazo yangu.!
Hawa watu wanaohamia CCM wana hamia kwa dhamiri kuu mbili..
1: kupata mahali ambapo maslahi yao yanaweza kutunzwa bila bugudha.. wakiamini kuwa Watanzania ni watu wa kusamehe hasa ukiwa na rangi ya kijani..

2.wanakuja huku kimkakati wakiamini kabisa njia pekee ya kuiangusha CCM ni kuwa ndani ya CCM yenyewe hivyo wanakuja kama virusi..ili wajizalishe kisha waipasue.!

Ushauri wangu kwa Wanaccm.
Hasa vitengo vinavyohusiana na uchunguzi.!
Hawa watu ni vema wakachunguzwa kwa muda wa kutosha mienendo yao matamshi yao na hata tabia zao! Kama tujuavyo kirusi huchukua muda kuanza kuleta madhara vivyo hivyo watu hawa hawapaswi kuchukuliwa tu kikawaida..

Hususani Julius Mtatiro.!
CCM halisa haina watu wenye nia njema na Taifa hili.
Mtu kama Polepole ni mtuwenye Historia ya kuitetea kwa nguvu zote Katiba ya Warioba lakini akaangushwa na wenzake waliofikiri ufisadi ni sehemu ya Chama na maisha yao.
Sasa amepewa Rungu na Dr. Bashiru chini wa Jemadari wa Vita ya ufisadi Mh. JPM. Ni wazi kuwa kuwakaribisha wale wenye uchungu na nchi hii popote walipo ni kuandaa Mazingira bora ya kupata Katiba bora wakati ukifika.
Kwa sasa maendeleo kwanza mana hilo halina ubishi. Baada ya maendeleo wataweka mazingizira mazuri ya kuyalinda na kuenzi utawala bora kwa kuleta Katiba bora.

Tumwamini mkuu wa nchi ana nia njema na watanzania wote.
Na ni vyema tukampa muda wa kutekeleza vipao mbele vyake kwa sasa kwa sasa.
 
K
Hilo swali kauliza Ephraem Kibonde ambalo naliona lina mantiki kubwa sana kwamba hao watu wanaotoka vyama vya upinzani kisha wakajiunga na ccm na kupitishwa moja kwa moja na ccm kugombea nyazifa walizoziacha huko watakako sasa ni kitu gani huko ccm hamna?

Pili ni mwanachama yupi wa ccm ambae anaweza kuhoji au kumkosoa moja kwa moja mwenyekiti wa ccm pindi akikosea ambae ni Raisi magufuli hivyo basi wakina mtatiro na mtulia wanaweza kumkosoa magufuli?

Maoni yangu sasa.

Binafsi naona kuna makubaliano fulani ya rushwa ya uongozi huwezi kujivua ubunge ukahamia chama b ukapitiliza moja kwa moja kuutaka ubunge ambao umeukimbia chama cha awali ambacho ulisimamia majukwaani kutetea itikadi na misingi yake zilizokupa ubunge au udiwani.

Changamoto zimeisha ktk jamii yetu hadi mtu uamue kuungana na fulani? Hapa linakuja suala la ubunifu

Hivi zanzibar ambayo inaongozwa na ccm kila kona maendeleo yake yanafukuzana na Qatar?

Kwa nini ukihama usiwe mwanachama wa kawaida na kutulia kwa nini ugombee tena waliopo huko hawafai?

Ni kiongozi yupi wa africa ambae yupo tayari kuachia madaraka kwa jambo fulani linalomfurahisha? Maswali ni mengi sana.
KWELI KABISA HAIWEZEKANI MTU ANA HAMA THEN ANAPEWA TENA KUGOMBEA NA KUWAACHA WALE WANAOPIGANIA CHAMA USIKU NA MCHANA. KWELI KABISA NAONA JINSI TUNAVYOTENGENEZA MPASUKO NDANI YA CHAMA CHETU. NAKUMBUKA CHADEMA WALIMPOKEA LOWASA NA KESHO WAKAMTANGAZA KUWA MGOMBEA NINI KINACHOENDELEA HUKO CHADEMA KWA SASA? NASI CCM TUSISABABISHE MAMBO HAYO KWA MAKUSUDI YETU TUWATUMIE WANACHAMA WETU KUGOMBEA NA SI KUWAPOKEA HAO WATU THEN KESHO TUNAWAPA UBUNGE.
LET'S BE CAREFULLY ABOUT IT
 
Pesa ni sabuni ya roho,hao wahamiaji ni wazi wamepata uhakika wa mlo kwa kipindi kirefu bila bugudha kutoka kweye mamlaka INRETURN wakimbizi haramu wameongeza wigo wa CCM kupitisha miswaada kwa zaidi ya 75% na hiyo katiba nadhani ndio TARGET.
 
Huwa nawaza hao ccm wanajisikiaje mpinzani ameingia tu na kupewa tiketi ya kugombea ubunge tena

Watakuwa wanaumia sana ccm kutoa sauti ndio hawawezi yajayo yanasikitisha sana yetu macho sie
Wala hata usiwaze, hii ni namna ya kuimaliza chadema, kwanza kuinyang'anya watu muhim pili kuipunguzia nguvu ya hela maana ruzuku itapungua kama sio kuisha kabisa, na kama tujuavyo chadema inaishi kwa ruzuku.

Athari ya hii movement ni kuwa chadema haitokuwa na nguvu ya kupambana kwa sababu watakuwa na uhaba mkubwa wa hela maana kiasi kidogo walichonacho kinatumiwa kwenye chaguzi za marudio.

Ccm ita dominate kampeni za 2020, Chadema itadondoshwa vibaya.

Hawa aliohama wanaachiwa miaka yao miwili wamalizie, ifikapo 2020 wengi wao wataondolewa kwa kura za maoni. Hivyo ama itabidi watulie wasubirie huruma ya uteuzi baada ya uchaguzi au warudi haraka upizani kuwaangukia na kuomba wapewe nafasi tena.

Hii Ndio siasa ya kiafrika, kwenye siasa jiangalie wewe kwanza kisha Chama baadae Sana waliokuchagua.
 
K

KWELI KABISA HAIWEZEKANI MTU ANA HAMA THEN ANAPEWA TENA KUGOMBEA NA KUWAACHA WALE WANAOPIGANIA CHAMA USIKU NA MCHANA. KWELI KABISA NAONA JINSI TUNAVYOTENGENEZA MPASUKO NDANI YA CHAMA CHETU. NAKUMBUKA CHADEMA WALIMPOKEA LOWASA NA KESHO WAKAMTANGAZA KUWA MGOMBEA NINI KINACHOENDELEA HUKO CHADEMA KWA SASA? NASI CCM TUSISABABISHE MAMBO HAYO KWA MAKUSUDI YETU TUWATUMIE WANACHAMA WETU KUGOMBEA NA SI KUWAPOKEA HAO WATU THEN KESHO TUNAWAPA UBUNGE.
LET'S BE CAREFULLY ABOUT IT
Chadema ni chama kichanga sana katika medani za kisiasa hata wanachama wabobezi ni wachache mno ni aibu kubwa chama cha mapinduzi ccm kuiga upuuzi wa chadema ccm ni chama kikongwe barani africa toka majeshini hadi vyuoni wamejaa watu wenye damu za ccm leo kikaanze kushoboka na mapandikizi?
 
Wote wanaohamia CCM na kupewa tena nafasi ya ubunge, wajue kuwa mwisho wao ni 2020, maana kutakuwa na mchakato wa kumpata mgombea mmoja, na ndio hapo wafia chama watakapoonyesha hasira zao na kuwapiga chini kikatili.

Watajuta kiujua CCM.
 
Ndugu wanabodi kutokana na hii hama hama ya baadhi ya viongozi wa upinzani(wabunge,madiwani na wanachama)pamoja na kupewa nafasi za kutetea nafasi zao za ubunge,udiwani na vyeo lazima wakumbuke kuwa mwaka 2020 wakati wa uchaguzi na wakati wa kupitisha wagombea wao watajikuta ni WAHAMIAJI HARAMU,kwasababu hawana historia wala misingi ya chama cha mapinduzi,hivyo kwa kuwa kura za maoni zitafanyika hawana nafasi za kujitetea.

Hii ni kwa sababu kwa sasa wanapewa nafasi kwa kuwa ni mkakati wa kudhoofisha upinzani na ndiyo maana hata kanuni kwa mjibu wa katiba ya ccm juu ya uteuzi wa nafasi zilizoachwa wazi haufuatwi yaani kuwa mwanachama kwa muda wa miaka mitano ili uaminiwe

Tutegemee wanasiasa watakaobaki bila mwelekeo .Nmemshangaa rais kusema eti wameguswa na juhudi za maendeleo,hivi kuguswa lazima uhame,inainekana asivyo mwanasiasa na wala hajui siasa ila siasa za kina afiki.

Tusubiri 2020 WAHAMIAJI HARAMU CCM.
 
Kazi kubwa ya CCM ni kudhoofisha upinzani,na kazi kubwa ya upinzani ni kuhakikisha CCM wanatembelea ringi,hapa chama chenye nguvu ndio kitakachosurvive
 
Ukianza kutumia logic and reasoning katika siasa za Africa na ccm hususani hapa Tz, utaumiza kichwa chako bure......hapa hamn itikadi au philosophy, kinacho fuatwa ni swala la kukurupuka na kufurahisha kiongozi mkuu....tabia hiyo hiyo itawasumbua mpaka chama kitapata mpasuko mkumbwa, kwa sababu "what goes round comes round" hamna mwana chama wa CCM wakwelikweli anae weza ku trust Mtatiro au Mtulia nawenzake,
Mimi pia huwa najiuliza ivi kweli mtatiro atakaa meza moja na wale vibopa wa ccm na akawa trusted? Hata kama Jiwe anawakubali ila kuna watu wenye nguvu ndani ya chama wataweka ngumu
 
Mimi pia huwa najiuliza ivi kweli mtatiro atakaa meza moja na wale vibopa wa ccm na akawa trusted? Hata kama Jiwe anawakubali ila kuna watu wenye nguvu ndani ya chama wataweka ngumu
Huyu kijana nikama ameharibu feture political career yake hamna mtu wa kumuamini akiwa CCM hata huku upizani amekua kama "political prositute" bora wale ambao walikua wanaponda CCM kwakuongee tu, yeye alikua anaandika Gazetini na makala yapo ataifuta je.
 
Ndo hapo sasa.Labda magu amewaahidi kuwa atatawala milele kama alivyodai hivyo anauhakika wa kukaa kwenye nafasi yake hadi mwisho.
 
nimemsikia anasema miiaka 2 sio.mingi nazani kunawatu wataliwa kichwa kwenye kula za maoni 2020 hasa hawa warowezi kama watara
 
ila hawata mzidi muhamiaji haramu mkuu ndani ya CHADEMA mzee lowasa
 
Hapo ndoujue kwamba siasa za vyama hapa Tz bado ni premature, yani mwenyekiti ni mzito anamaamuzi kuliko chama chote kila mtu anamogopa kupishana kauli nae..chukua mfano wa ANC Zuma aliondolewa na Chama, Mbeki kaondolewa na Chama ZANUPF wamemuondowa Mugabe.... sasa niwakati muafaka CCM wainge vyama vikonge vinavyo fanya, wasiendelea kuogopa kinyago walicho chonga wenyewe.....wasaidie wananchi kusema "No" enough is enough uwezo huo wanao.
Thubutuuuuuu!!!!!?
 
Mkuu jibu lipo wazi-Hamia huku nakupa ubunge wako, nakulipia madeni yako yote ya bank na TRA halafu na kulipa PESA YA UHAMISHO.

Mwisho kabisa nitakapoliamsha dude la kufia madarakani hakika na wewe utafia madarakani.
Aya ya mwisho mkuu 100%
 
Back
Top Bottom