Swala la umeme: Kwanini ham-protest? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swala la umeme: Kwanini ham-protest?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Natalia, Jul 27, 2011.

 1. N

  Natalia JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Inaelekea watu wanapenda giza.Ni kwa nini watu wanakubali kukaa gizani na hawalalamiki wala nini ,inaelekea mnapenda hiyo style .
   
 2. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Waziri muhusika alitakiwa ajiuzulu juu ya kukosekana kwa umeme,alipitisha rushwa kubwa sana kama bilioni kazaa hivi alingiza katika budget yake ili aje walipe wabunge kila mmoja milioni 50 kwa kupongzwa kupitishwa kwa budget yake.

  Napendekeza mimi kwa wananchi,katika mchakato unaokuja wa katiba,kuweke sheria juu ya walaji rushwa na wawanaochezea mali za umma,akipataka mtu mwenye hilo kosa apigwe kinyongo tu ili iwe funzo kwa viongozi wengine.

  Ubaya wa ulitumika hapa tz ni kwamba vyanzo vya umeme ni vichache na hivyo ndivyo vilivyoifanya nchi nzima kuwa giza,wakati ilitakiwa kila mkowa kuwe na vyanzo vyake vya umeme,kunapotoka athari isi athiri nchi nzima.

  Hwa viongozi wamesoma au wame cremu mabuku tu ? Mbona hawako waamini sana na hawajui wajibu wao,hawako creative sana,viongozi wanasingizia mabwawa ya maji yamekauka sasa nauliza.

  Hivi zile nchi za kiarabu jangwa tupu wanapata umeme wa majabali au umeme gani ? Mana hakuna mito kama tulio nayo tz ?
   
 3. N

  Natalia JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kIkwete amewaweka pembeni wasomi wote .yule mama Lugembe Rose yuko wapi . Haya nchi haina umeme watanzania hawalalamiki
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  yoyo, umeshamaliza kifungo?
   
 5. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Watanzania walio wengi hawawezi kuprotest wala kulalamika kwa kuwa si utamaduni wa kizazi kinachotumia umeme au wale tunaoweza kusema wenye uwezo wa kununua umeme kuwa ni kizazi cha watu wazima ambao wengi wao walilelewa kuto kuhoji wala kufuatliwa maswala muhimu kwa kuwa zama zao mtu aliyefuatilia mambo ambayo Serikali ilikuwa inayasimamia alionekana kama Mtu mkolofi na Mwenye chokochoko kwenye jamii.

  Ulikuwa ni Mfumo wa kumeza na kamwes si kuoji dhidi ya lolote lile linanaloendelea Serikalini na hivyo kuifanya Serikali kuwa haina changamoto toka kwa umma wake hivyo kuibuka kwa baadhi ya viongozi kuonekana ni Miungu watu.Kwa kuwa Maamuzi mengi ya Serikali miaka hiyo yalionekana kama ni kitu daima sahihi,na hata kama kilikosewa Raia wa kawaida hakuwa na haki kuuliza na kupata jibu la hicho amabcho hakuridhika nacho.

  Hivyo basi sehemu kubwa ya Wananchi ambao sasa ni watu wazima wakawa ni watu wa NDIO ZAIDI,kuliko kuhoji na kupata majibu pale ambako hawakulidhika na utendaji wa Seriakali.

  Leo hii wanachuo walioingia kwenye vyuo vyetu vikuu miaka ya 2005 ndio wamekuja na uelewa mapya ambao wanajaribu kuhoji na kutaka ufafanuzi pale ambako wanaona hawana ufafanuzi na taarifa sahihi kuwaridhisha kuhusu na hicho wanachotaka kujua.Kwa ujumla vijana wa sasa wana uthubutu wa kujaribu tofauti na wazazi wao ambao ndio wateja wa umeme wa Tanesco,ambao walilelewa kutokuhoji.
   
 6. N

  Natalia JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 3,558
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kifungo cha nini nipo marekani nimeolewa na mzungu naishwa na kuvalishwa . Nafikiria jinsi gani nita weza kumtumia mzungu wangu kuja kuwauzia umeme
   
 7. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Tatizo la watanganyika wanasoma ma book tu na munashindwa kutumia akili zenu kuchambua mambo,sio umeme tu mambo mengi munashindw akuchambua na tatizo kubwa la watanganyika hamupendi ukweli,na ndio ikafika time muna lala giza.

  Vizazi vilivyo pita vya wazee aliki zao zilia duni sana,na ndoma enzi hizo walikuwa wakivaa ngozi hadi miaka 1960,wakati wazungu tayari washatengeneza nguo,hebu tuweni creative jamani,tuamkeni,tuwekeni uwazi .

  Leo mtanzania bara umwite mtanganyika anakasirika lakini nyinyi munatuita wapemba,wazenjii wazanzibari,sisi tunajifahari na tumeamka sasa hivi kwa kila kitu,ugao wa umeme uwewashinda ccm wameona kuimaliza zanzibar kwa bilioni 50 ili kuziba pengo la umeme,Waziri wa madini katumbua pesa huyo na familya yake kaona sasa wapi atazirudisha ni kuikaba zanzibar.

  Huyu waziri anafaa ajiuzulu,amkeni watanganyika ingieni barabarani ccm nchi imewachinda,viongozi wote wa ccm ni majambazi,ndio hawa ambao walikuowa wakipiga risasi kariakoo miaka ya 2005,sasa ndhi hao wabunge na mawaziri.

  HAHAHAHA ,amkeniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 8. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Niambie sisi Wazenji tunatumia akili gani wakati kila kitu tumelala tunawategemea machogo, umeme wenyewe watupa wao kwa upendeleo kama wake wadogo, upuuzi tu, hujui unacho ongea kaa kimya!
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  kaka mimi ni member kwenye viti virefu, sasa umeme huwa ukikatika tu watu hawaguni wala kulalamika kinachofuata huwa kila mtu alipo kuchukua position yake - yaani karibia midume mingi bega la kushoto linainamia usawa wa mgeni wake sambamba na mkono wa kushoto chini ya meza. sasa hapo mvua itanyesha kweli ijaze mabwawa? lol

  Kifupi wa TZ tulio wengi tunapenda giza hence your point proved!!.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ngoja kwanza bunge liishe!!
   
 11. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Tumekula ugali wa yanga hatukuprotest!!! Umeme tu tuingie street???
   
 12. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Wewe ulikuwepo wapi siku zote hizo,kwanza sio mzenji wewe na huwezi kuongea kitu hicho hata siku moja,zanzibar mpaka miaka ya 1964 tulikuwa na umeme wetu wa kujitegemea,tulikuwa na vyanzo vya umeme vya zanzibar kutoka zeco,Baada ya muungano nyerere alitumia technic ya kuuchukua umeme wetu,alichokifanya kutuletea umeme wake na kuchua magenerator ya zanzibar ambayo yalikuwa yakizalisha umeme.

  Zanzibar hadi miaka ya 1964 tulikuwa na tv ya rangi ambayo africa ni nchi ya mwanzo kumiliki,tulikuwa na lift katika majengo ya serikali ikiwemo hospital ya mnazi mmoja,kulikuwa na simu za mkononi huko wengereza kulikuwa hakuna unajua hilo wewe ?

  Zanzibar ilikuwa na pesa zakigeni kwa wakati huo katika bank ya dunia dola bilion 15,unafahamu wewe siri ya muungano au unasema tu wewe ? Unajua history ya zanzibar wewe ? ACHA UPUMBAVU WAKO,mzanzibari hasubutu kuongea kitu kama wewe .
   
 13. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Maskini sie tumeshalizoea giza letu.
  Tuacheni tukae nalo tu tusije tukalalamika alafu tukapigwa mabomu.
  Ama wenzetu hamuogopi polisi?
   
 14. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  wacha uzaifu wewe,kwanza nikuulize wewe mwanamme au mwanamke ? mbona umekuwa unaogopa ogopa,utakufa masikini wewe.
   
Loading...