Swala la Muungano ni zito, si la kuchukulia masihara!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swala la Muungano ni zito, si la kuchukulia masihara!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Moseley, Apr 30, 2011.

 1. Moseley

  Moseley Senior Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
 2. k

  kabindi JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Muuungano haukuwekwa na Mungu! ni vema kwamba waasisi wetu walikuwa na nia njema maana umoja ni nguvu! LAKINI lazima na nilazima uwe kwa ridhaa ya WANANCHI! Pia hamuwezi kuungana na kuwa nchi moja ya Tanzania mkapata nchi mbili TANZANIA NA ZANZIBAR! Muungano gani huo?! WATANGANYIKA TUNAITAKA TANGANYIKA NA WAZANZIBARI TUNAITAKA ZANZIBARI! Then tukae chini tuangalie kama tunaendelea kupendana katika yale mambo 11 tuliyokubaliana na siyo 26/28 yaliyowekwa kinyemela.! Huwezi kulazimisha kufungamana na mtu! Kwani nchi zote duniani zina Muungano?!
   
 3. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Unasemwa ni muungano wa kipekee duniani unaoendana na kanuni za hisabati 1+1=2,kwa hiyo mathematically muungano huu uko sawa kabisa.But logically Big NO.Muungano unaabudiwa na viongozi,wanaukumbatia wanaubusu wanauacha ukiwa hoi.Wanawaacha raia wajaze wenyewe.
  Mimi huwa nasema katika makosa ambayo mwl aliyafanya ni lile lililosababisha waNigeria wamuondolee heshima yake na kubadirisha sehemu iliyokuwa inaitwa port nyerere na kuitwa port Harcout.Kubwa zaidi ni hili la Muungano ambao haukuwa wa kitaalam.Kwa sasa tumefikia mahali ambapo hatuwezi kwenda nyuma au mbele i.e hatuwezi huesema muungano tuuvunje au tuendelee nao.Sishauri muungano uvunjike lakini suala la serikali tatu liwepo.Haiingii akilini Tanganyika ipotee kwa gharama rahisi ya mambo 11 ya muungano hilo halikubariki.Kama na Zanzibar ingepotea hapo ingekuwa sawa kwa sababu tungepoteza wote.Serikali moja sio rahisi maana nawafahamu wazanzibar wanaona fahari na nchi yao na serikali tatu haiwezekani kwa sababu hiyo hoyo ya wazanzibar kuhisi kwamba wananyanyaswa.Watanganyika hawana hawako serius wala hawajivunii kuwa watanganyika.Neno tanganyika limekuwa na ukakasi sana midomoni wao.Wanabaki kujisifia kwa sifa za kijinga,eti sisi ndo tumewaoa kwa sababu ni nchi ndogo! Mmewaoa! acha mchunwe huku mkisema chini chine kwamba nduhu tabu bageshi!!
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Tunataka Muungano uzungumzwe! Ujadiliwe na uchambuliwe ili tujuwe tulipojikwaa ktk kipindi chote na turekebishe kasoro za muungano wetu. Tunataka muungano ambao utakuwa tunu kwa vizazi vyetu vijavyo, si muungano ulioshikiliwa na Chama, kikundi au upande mmoja wa muungano. Tunataka muungano utakaokuwa juu ya matakwa na majaaliwa vyama vya siasa na si muungano ulio chini ya matakwa na majaaliwa ya chama fulani. Hakuna Mtanganyika au Mzanzibari mwenye utimamu wa fikira aliye tayari kuona huu muungano ukivunjika ktk hali hii ya sasa. Sote tunataka tuujadili na kama ni kufa ufie ktk meza ya majadiliano. Wasiwasi tulionao wengi ni kuwa Serikali ya CCM inajuwa ugonjwa unaosumbua muungano wetu tangu na tangu ndo mana wameamua kuhangaika kujaribu kuutibu kimyakimya kwa kipindi bila mafanikio. Na sasa hali ya muungano imekuwa mahututi kiasi serikali imeingiwa na hofu na kiwewe hata kuona wale wanaotaka ugonjwa wa muungano uwekwe wazi tujadili sote namna ya kuutibu ni wendawazimu wanaostahili kupuuzwa. Serikali ya CCM inajidhihirisha ilivyo bingwa wa kupuuza sauti za walio wengi na kujiona yenyewe ndiyo muarobaini wa mambo hata yaliyo juu ya mipaka yake. Ole wao wanaotaka muungano uvunjike. Ole wao wanaojaribu kuzuia mijadala ya wazi juu ya muungano! MNAJARIBU KUFICHA NINI KTK MUUNGANO? ACHENI TUUJADILI KWA FAIDA YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR NA WATU WAKE, SI VYAMA AU KIKUNDI CHA WATU FULANI. Mungu ibariki TANGANYIKA, Mungu ibariki ZANZIBAR na AFRIKA!
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Wazo la nchi hizi kuungana halikuwa la Nyerere,haya yalikuwa ni moja ya masharti ya Uiengereza ya kutoa uhuru,Nyerere alikubali shingo upande kwa sababu alikuwa anautamani uhuru,hivyo uhuru wetu ulikua bandia ndo maana kuna wakati Nyerere aliwahi kusema kizazi kijacho kinatakiwa kiutafute uhuru wa kweli wa nchi za Afrika,uhuru wetu tulipewa kwa masharti kibao mojawapo ni muungano
   
 6. k

  kabindi JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bwana Eiyer! uhuru upi unaouzungmzia? Tanganyika imepata uhuru wake 1961 na 1964 ni Muungano. Na baada ya hapo wananchi wake waliendelea kukosa uhuru kutoka mikononi mwa Nyerere na Karume! ndio maana ukumuuliza mtu mwenye akili sasa hivi kuhusu uhuru atakwambia heri ya ukoloni kuliko hivi sasa?! ndiyo maana tunataka katiba mpya tuwe huru!. Hebu fikiria, kabla na mara tu baada ya uhuru; miundo mbinu kwa maana ya Hospital, Shule, Maji na Viwanda vilikuwa vikifanya kazi!! wakati huo wataalamu walikuwa wachache, pia Sayansi na Technologia ilikuwa duni. Leo hii tuna wataalamu wa kumwaga, vyuo vikuu vingi, Sayansi na technologia ipo juu lakini, Viwanda vimekufa, miundombinu ni duni, nishati matatizo! mambo ya ajabu sana!!!
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kuna mahali nilichangia,kulikuwa na mjadala unaoshabihiana na huu.Let us go for federalism,let shun off whining unnecessarily and boldly let us move foward

  Nimekuwa nikisizitiza Umuhimu wa Federalism kwa nchi kama yetu.Kati yetu na zanzibar imekuwa kama ni one state against the other.It's like one state hijacked the rights and privileges of another state by conspirancy

  Reading the above made me think deeply on the composition of Tanzania and the different challenges posed to us as a people. Tanzania has seemingly stagnated due to the fact that we have refused to base our togetherness as a nation on the strengths of our differences as a group of diverse nations. As evidenced in the practice of Union style practiced by countries similar in composition to Tanzania as Switzerland through cantonments (loose federation,though) and United Kingdom, we can not grow in our present contraption where there is gross concentration of power and duties in an all-powerful central government instead of an ideal situation where we should have powerful states/regions with a strong enough central government to cater for areas of common need such as National security i.e the Armed forces, Intelligence agencies and para-military forces excluding the police; and Foreign affairs. States/Regions should be made to cater for the needs of their peoples and pay tax/duties to the central government Only by so doing can we really develop our people and make governance less attractive to purposeless administrators/leaders. We are a people abundantly blessed by nature with more resources than most of the so-called developed economies in the world.

  Under the present system that aims at getting all the peoples in Tanzaniato the goal of development at the same time and hour, we are consistently doomed to continuously wander with no concrete achievements to write home about. True Federalism would solve problems like Tanganyika-Zanzibar leadership clashes and unproductive debates, local government creation since their funding would be from the state governments and as such problems of increased funding from the Union account leading to suspicion among the different States/regions in Tanzania would be eliminated. This would also reduce the problem of illiteracy as states would be compelled to develop their people as individuals to be able to compete with other states as a means of avoiding being left behind and also to harness their resources as best as they can, whether mineral resources, manpower, Intellect, industry etc.

  So,Zanzibar's case itakuwa solved as kutakuwa na states nyingi kama Zanzibar. Tanganyika na Zanzibar ya Leo itagawanywa vipande vipannde na ku-create several states,but in the process we must ensure that,tribalism and religion-ism should be avoided
   
Loading...