Swahiba wa Mizengo Pinda ashinda Urais Namibia, walishiriki wote jopo la kuandika katiba ya Namibia

Na mimi nasema kwa #kaliba ya watu kama wewe hakuna kiongozi asiyefaa. Kila mtu ni malaika na hata ashuke shetani mtamsifu tu. Ni nyie mnahitaji maombi. Maisha ya Albino yalipokuwa hatarini Pinda aliishia kumwaga machozi na hadi leo miaka saba baadaye bado usalama wa Albino ni wa mashaka. Wakati wa sakata la EPA, Pinda, kama Waziri Mkuu na kiongozi wa serikali bungeni alitamka maneno yanayofanana na haya, watuhumiwa wa EPA wana nguvu, wakikamatwa nchi itayumba...mafisadi wakichukuliwa hatua nchi itayumba, KWELI?
KBOSCO, ni kweli hakuna binadamu aliyekamilika 100% lakini pia zingatia kuwa binadamu hutofautiana katika mafanikio kulingana na malengo tuliyojiwekea na kwa kiasi gani tumeweza kuyafikia. Kama Pinda aliikuta nchi katika hali hiyo unayodai, amefanya jitihada gani kutunusuru hapo na amefanikiwa kwa kiwango gani kama Waziri Mkuu. Huo unaouita mchango wa Pinda je umeweza kuleta mabadiliko yoyote katika kulitoa nchi huko ilikokwishawekwa kwenye RADA ya unyonyaji wa akina LOWASSA etc? Ukiweza kunitajia hatua moja tuliyoweza kupiga kutokana na uwepo kwa Pinda kama Waziri Mkuu na kiongozi wa serikali bungeni niko tayari kumpa pongezi.
Granted tukubali kuwa alikuta kila kitu kiko #mateka na wahuni washamaliza biashara, je hao wahuni ameweza kuwatokomeza au wameendelea kustawi notwithstanding his presence. Kama hakuna mabadiliko yoyote yanayoonekana kwa wazi kabisa yameletwa kwa uwepo wa Pinda hicho cheo kwa nini alikikubali? Kuna msemo kuwa kama huwawezi kuwashinda ungana nao, je Pinda naye kaamua kuungana nao?

Utanisamehe lakini kwa kiwango kidogo ninachofahamu, hakuna kipindi ambacho ubadhirifu kwenye halmashauri na serikali za mitaa imeshamiri kama kipindi cha Pinda. Ripoti za CAG kila mwaka toka ameingia Pinda zimeonesha kwa kiasi gani wananchi wamezidi kuumia kwa kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii kutokana na udokozi na wizi wa pesa kwenye sehemu husika. Yawezekana Pinda kweli anaguswa na shida za Watanzania (hususan wa vijijini) kama unavyodai lakini zaidi ya kumwaga machozi, sikumbuki mchango wowote wa Pinda kushughulikia matatizo hayo.
KBOSCO, nakuapia sina chuki binafsi na Pinda ila nakuomba uwe mkweli kwa nafsi yako ukiri kile kinachokusukuma kumtetea, kafanikiwa nini katika uongozi wake? Hata pale Bunge lilipoazimia wafujaji kama Jairo wachukuliwe hatua, Pinda hakuweza kupata hata ujasiri wa kuwakemea wahusika zaidi ya kulialia akimsubiri bosi wake arudi. Katika historia ya nchi hii hakujawahi kutokea Waziri Mkuu asiye na meno zaidi ya Peter Kayanza Mizengo Pinda.

Umeeleza mengi mno.

Lakini nashukuru mwishoni umenifanyia wepesi. """KWA SUALA HILI,HAKIKA NINGALIKUWA RAIS,LEO HII HII ( #Jairo )LAZIMA ANGEWAJIBISHWA MARAMOJA"""

Nadhani unaweza kuona namna hata J.K alivokuwa kibri na kumuwekea mazingira magumu. J.K aliporudi,Pinda alimweleza namna bunge lilivyoghadhabishwa na habari ya Jairo. Akamsihi amtimue,but since JAIRO was there for the interests of JKs,Pinda had nothing to bend the direction.

Issue ya albino,alitaka kuanzisha utaratibu mzuri tu wakuwabana watuhumiwa(kama si kuwatisha). Ni nyie haohao mlompeleka Mahakamani. Aliguswa mno na issues hizo coz hata yeye mwenyewe kwanza ana vijana(ALBINO) kama 50 hivi anawatunza. Lakini wanaharakati kina MAG3 waliguswa zaid na wauaji wale,wakawatetea!

Mambo ni mengi sana. Walau kwa machache hayo,utakuwa ushapata kitu flani kizuri juu ya Pinda. Na wewe sasa utueleze Mh.Lowasa kafanya lipi lakusifiwa!
 
Fitina mwiko acha fitina mkuu. Pinda hajabadilika, hajawahi kuwa na kashfa wala doa miaka yake yote ya utumishi. Pinda amekomaa na kushiba maadili ya mwalimu Nyerere.

Mwalimu alisema "sito ona haya kumuonea haya mwizi, mzembe na mzururaji" Je Pinda kwa kipindi alichokaa madarakani amefanya nini kuhusu wezi wa mali ya umma? Tuliona Sokoine alivyokuwa, Pinda alikuwepo Ikulu kipindi kile, Je tunaweza fananisha utendaji wao wa kazi? Pinda hafai kabisaaaaa, hajui ukubwa wa madaraka yake.
 
Mbona katiba yetu inayopendekezwa ni nzuri mkuu? Acha mawazo ya wasaka vyeo wa UKAWA wanaowaza serikali 3 tu. Katiba imezungumza masuala mengi mtambuka, haki za makundi mbalimbali, wakulima, wafugaji, vijana, kina mama, n.k. Sioni tatizo

Katiba isiyoweza kuwawajibisha viongozi wabadhirifu hiyo kweli ni katiba. Not at this age! These people have failed us ............ l can't believe there is someone who's embracing the same people!!
 
Mmmh Pinda Yule aliyesema ningekuwa Mimi rais ningemfukuza mara moja. Mmmh sakata la madaktari lilimyumbisha sana. Pinda mwanasiasa msafi sema akikumbwa na misukosuko hasimami strong.
 
Back
Top Bottom