Swahiba wa Mizengo Pinda ashinda Urais Namibia, walishiriki wote jopo la kuandika katiba ya Namibia

Sasa Pinda haoni aibu kuwa alishiriki kuwaandikia katiba nzuri Namibia kitu ambacho huwa anajisifia kila siku. Lakini, Akiwa kama Waziri Mkuu ameshindwa kuwa influence CCM kutuandikia katiba ya maana! Kwa ujumla kumlinganisha Hage na Pinda ni kama kulinganisha mafuta na maji !!
 
Nina langu jambo.

Kusema kwamba Pinda hafai urais. Pinda mwenyewe kasema alivyotaka kwenda kugombea ubunge Mkapa alimwambia you are not leadership material.

What more can I say?

Na hapohapo baadae akasema hivi, ""MIMI KAMA RAIS,NILIMTAKA MWINGINE TOFAUTI NA KIKWETE,LAKINI MWISHO WA SIKU WATU WAKAMPENDA MGOMBEA MWINGINE. IKIFIKA WAKATI,UNAPASWA KUTULIA ILI WAJUMBE/WAPIGA KURA WAONGEE"" **mwisho wa kunukuu**

Sasa hayo yalikuwa kwa J.K v/s SUMAYE 2005.

Kama aliyaongea hayo kwa Pinda,naamini alimaanisha kama nilivokuonesha kwenye quotation hapo juu.

Pinda angekuwa legelege,asingepasua miamba yote hiyo hadi hapo alipo.
 
Pinda alikuwa mzuri kipindi kile cha Mwalimu, lakini sasa hivi ni history. Hawezi kuongoza hata kijiji
 
Pinda inaonekana aliaminiwa na mwalimu

Ni kweli mkuu ukisoma historia ya maisha yake ya utumishi serikalini PINDA yuko vizuri Sana na aliaminiwa na Mwalimu mapema sana akiwa na miaka 27 hiyo ni kutokana na weledi na uaminifu wake katika utendaji wa kazi na majukumu mbalimbali aliyokuwa anapewa
 
Na hapohapo baadae akasema hivi, ""MIMI KAMA RAIS,NILIMTAKA MWINGINE TOFAUTI NA KIKWETE,LAKINI MWISHO WA SIKU WATU WAKAMPENDA MGOMBEA MWINGINE. IKIFIKA WAKATI,UNAPASWA KUTULIA ILI WAJUMBE/WAPIGA KURA WAONGEE"" **mwisho wa kunukuu**

Sasa hayo yalikuwa kwa J.K v/s SUMAYE 2005.

Kama aliyaongea hayo kwa Pinda,naamini alimaanisha kama nilivokuonesha kwenye quotation hapo juu.

Pinda angekuwa legelege,asingepasua miamba yote hiyo hadi hapo alipo.

Tanzania dhaifu Kikwete kaqezankuwa rais, lakininlegelege Pinda hawezi.

Ashukuru wamekosa kumnyoa juzi kwenye escrow. Sasa hivi baada ya upepo kupita aokote mbao na kuanza kujenga nyumba yake ya kisiasa upya.

Lofty ambitions for even higher offices while he can't handle his current one are misplaced.
 
Unachuki binfsi wewe! KIRANGA maana yake ni #SHETANI (kwa Kiha). Nadhani wewe ndiye na ndo maana unaongozwa na utashi wauongo.

UKAWA e.t.c walikuwamo ndani mle. Walilichakata suala hilo kwa makini na kweli.

Kwamba wewe ndiye imara kuliko hao?

UNALAKO JAMBO!

Mkuu unalipwa nini, mbona povu jingi?
 
Hage Geingob (phd) amechaguliwa kuwa Rais wa Namibia katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi November, 2014 akivaa viatu vya Hifikepunye Pohamba aliyemaliza muda wake. Dr Geingob alizaliwa mwaka 1941 na alishiriki katika vuguvugu la ukombozi wa taifa la Namibia hadi uhuru wake mwaka 1990.

Kufahamiana kwa Dr Hage na PINDA

Rais Hage alifahamiana na waziri mkuu wa Tanzania mh Mizengo Pinda wakati wa vuguvugu la uhuru wa Namibia. Ikumbukwe kuwa Tanzania ilisaidia sana nchi nyingi za kiafrika katika vita vya ukombozi. Waziri mkuu Pinda alikuwa miongoni mwa team maalum iliyoundwa na serikali ya Tanzania kwenda Namibia kusaidia kuandika katiba ya nchi hiyo pamoja na kuandaa mfumo wa uongozi wa serikali mpya ya Namibia baada ya vita vya ukombozi. Jopo lile liliundwa na ikulu ya Tanzania kwa mawazo na mchango mkubwa wa mwalimu na lilifanya kazi yake mwaka 1989-1990.

Dr Hage Geingob awa Waziri Mkuu wa Namibia 1990

Baada ya kukamilika kwa kazi ya kamati ya kina Pinda ya kuweka mfumo wa uongozi na katiba ya Namibia, Hage Geingob, Rais wa sasa wa Namibia aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Namibia. Nafasi hii aliitumikia hadi mwaka 2002 .

Rais Hage awa makamu wa Rais wa SWAPO

Mwaka 2007, Rais Dr Hage alichaguliwa kuwa makamu wa Rais wa chama tawala SWAPO, chama ambacho kimekua madarakani tangu uhuru. SWAPO ndicho chama cha ukombozi wa Namibia.

Dr Hage Geingob awa Waziri Mkuu wa Namibia kwa mara nyingine

Mwaka 2012, wakati mh Mizengo Kayanza Peter Pinda akiwa waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wake wa nne (2008-2012), rafiki yake wa muda mrefu Dr Hage Geingob nae aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Namibia.

Dr Hage achaguliwa kuwa Rais wa Namibia November, 2014

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu Dr Hage Geingob alichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamuhuri ya Namibia. Hage ameingia ikulu ya Namibia akitokea ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo. Rafiki yake waziri mkuu Pinda anatajwa kutangaza nia ya kugombea urais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2015.

Inasemekana Pinda na Hage bado ni marafiki wanaoendelea kuwasiliana kwa karibu. Wafuasi wa waasisi wa ukombozi wa bara la Africa wameendelea kuwa na nguvu katika uongozi hasa mataifa yaliyo kusini mwa Afrika.
Kila la kheri Mizengo Pinda , nyota njema huonekana asubuhi.
Unajua watu bado hawamjui vizuri Pinda ila nadhani taratibu watamjua,watu wengi wanamjua tu kwa kazi yake ya Usalama wa Taifa lakini bado hawamjui nini alifanyia Taifa katika Utumishi wake toka Enzi hizo mpaka sasa ,lakini ngoja niwafahamishe kitu kingine alichofanyia Taifa wakati wa vita vya Tanzania na Uganda ni mmoja wa Maafisa walioteuliwa katika kushilikiana na Jeshi katika kuhakikisha Iddy Amini anapigwa .pinda Ana sifaa ya pekee na ni mzalendo kwel kweli
 
Kumbe mtu akisaidia kuandika Katiba basi anaukaribia Urais! Chenge ajiandae hapa kwetu.
 
Mkuu Arch mchango wa Pinda katika ukombozi na ujenzi wa taifa la Namibia

Unamkuza bure tu ............. kwenye lile kundi lililokwenda Namibia, Pinda alikuwa mtu mdogo sana ............. wala hastahili hiyo sifa unazomtafutia. Jamaa alikuwa ni msaidizi wa akina Warioba na Bomani. Hao ndiyo walikuwa kwenye mission! Halafu kudai ana mchango kwenye ukombozi ni upotoshaji mkubwa sana ........... alipokwenda Namibia ilikuwa ni wakati UN imepeleka watu kusaidia. Nchi kama Kenya ilipeleka jeshi.
 
Kolimba Jr,
Hapa mnachofanya ni ku exaggerate mchango wa Mizengo Pinda kwa Namibia.

Ninavyoelewa mimi Jaji Mark Bomani na Prof.Keto Mshigheni ndiyo waTz wanaoenziwa huko Namibia kutokana utumishi wao kwa taifa hilo.

Jaji Bomani ana mchango mkubwa ktk uandishi wa katiba ya Namibia.

Prof.Keto Mshigheni alishiriki kuanzisha chuo kikuu cha Namibia.
Jengo la maabara ya marine biology univ of Namibia limepewa jina la Keto Mshigheni kwa kutambua mchango wake ktk chuo hicho.

Hizi hadithi za Pinda na Namibia hazina tofauti na jinsi Al Gore ambaye wakati wa uchaguzi ali exaggerate mchango wake ktk masuala ya internet huko Marekani.
Tunko, Kiranga
 
Last edited by a moderator:

These little itinerant hangers on never cease to amaze me.
 
Last edited by a moderator:
Hage Geingob (phd) amechaguliwa kuwa Rais wa Namibia katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi November, 2014 akivaa viatu vya Hifikepunye Pohamba aliyemaliza muda wake. Dr Geingob alizaliwa mwaka 1941 na alishiriki katika vuguvugu la ukombozi wa taifa la Namibia hadi uhuru wake mwaka 1990.

Kufahamiana kwa Dr Hage na PINDA

Rais Hage alifahamiana na waziri mkuu wa Tanzania mh Mizengo Pinda wakati wa vuguvugu la uhuru wa Namibia. Ikumbukwe kuwa Tanzania ilisaidia sana nchi nyingi za kiafrika katika vita vya ukombozi. Waziri mkuu Pinda alikuwa miongoni mwa team maalum iliyoundwa na serikali ya Tanzania kwenda Namibia kusaidia kuandika katiba ya nchi hiyo pamoja na kuandaa mfumo wa uongozi wa serikali mpya ya Namibia baada ya vita vya ukombozi. Jopo lile liliundwa na ikulu ya Tanzania kwa mawazo na mchango mkubwa wa mwalimu na lilifanya kazi yake mwaka 1989-1990.

Dr Hage Geingob awa Waziri Mkuu wa Namibia 1990

Baada ya kukamilika kwa kazi ya kamati ya kina Pinda ya kuweka mfumo wa uongozi na katiba ya Namibia, Hage Geingob, Rais wa sasa wa Namibia aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Namibia. Nafasi hii aliitumikia hadi mwaka 2002 .

Rais Hage awa makamu wa Rais wa SWAPO

Mwaka 2007, Rais Dr Hage alichaguliwa kuwa makamu wa Rais wa chama tawala SWAPO, chama ambacho kimekua madarakani tangu uhuru. SWAPO ndicho chama cha ukombozi wa Namibia.

Dr Hage Geingob awa Waziri Mkuu wa Namibia kwa mara nyingine

Mwaka 2012, wakati mh Mizengo Kayanza Peter Pinda akiwa waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wake wa nne (2008-2012), rafiki yake wa muda mrefu Dr Hage Geingob nae aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Namibia.

Dr Hage achaguliwa kuwa Rais wa Namibia November, 2014

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu Dr Hage Geingob alichaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamuhuri ya Namibia. Hage ameingia ikulu ya Namibia akitokea ofisi ya waziri mkuu wa nchi hiyo. Rafiki yake waziri mkuu Pinda anatajwa kutangaza nia ya kugombea urais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2015.

Inasemekana Pinda na Hage bado ni marafiki wanaoendelea kuwasiliana kwa karibu. Wafuasi wa waasisi wa ukombozi wa bara la Africa wameendelea kuwa na nguvu katika uongozi hasa mataifa yaliyo kusini mwa Afrika.
Kila la kheri Mizengo Pinda , nyota njema huonekana asubuhi.
je. katiba ya Namibia inafanana na hii ya pinda na sitta
au. ndio team pinda kazini
mmnatuboa sana na hizi mbio za urais na ufisadi ccm wakati mmetuponza ssaa hospitali hazina madawa nyinyi mnapigania ikulu ili mkalindane
 
Kuna watu hatuna haki ya kudai kama wana uwezo au hawana kwa sababu hawajawahi kupewa nafasi ili tuweze kuwapima lakini kwa Peter Kayanza Mizengo Pinda ni tofauti. Huyu jamaa kapewa nafasi aweze kutuonesha uwezo wake na hadi leo miaka zaidi ya sita toka ateuliwe hajaonesha uwezo wowote ule...sana sana ameonesha udhaifu wa hali ya juu ambao haukutegemewa. Pinda astaafu tu na ashukuru kufikia hapo alipo na kama tungekuwa na uongozi makini unaofuata misingi ya sheria na utawala bora, Pinda hangedumu kata kwa mwaka moja. Lakini ndio hivyo tena kwa viwango tulivyojiwekea haishangazi hata kidogo kwani si ajabu hata hii leo kuwakuta watu ambao wangependa kuona Kikwete anaongezewa kipindi kingine cha miaka mitano. Huo ndio ukweli; tumegota "at the very bottom" na haiwezekani kushuka zaidi.
 
Back
Top Bottom