Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

Suphian Juma: Nimeng'atuka ACT Wazalendo

Suphian Juma

Senior Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
140
Reaction score
579
NIMENG'ATUKA ACT WAZALENDO-SUPHIAN.

Najua wengi mmeumia sana. Mmestaajabishwa mno na maamuzi ya Chama changu cha ACT wazalendo kukubali kuungana na Serikali ya Magufuli na Mwinyi tuliyoitangazia dunia imeunajisi Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2020.

Kitendo cha Chama kukubali kupeleka jina la Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na kuridhia kuapishwa wabunge wake; naelewa na naona wengi wananchi wenzangu si tu kimewakasirisha kupitiliza ila bali pia kimewatolea imani katika kuwaamini wanasiasa na vyama vya upinzani nchini.

Wengi tangu Jana Desemba 06, 2020 Chama kilipotangaza uamuzi wake huo kupitia Katibu Mkuu, rafiki yangu Ado Shaibu mmeendelea kuniuliza msimamo wangu mtandaoni, kwa simu hadi ana kwa ana kwa kuzingatia mimi kama mwanachama na Mtanzania ninayependa na kuheshimu Haki za Binadamu na Demokrasia, hivyo hakika nasema hampo peke yenu, Masikitiko yenu Watanzania wenzangu ni masikitiko yangu pia.

Uchaguzi ulikuwa batili, uongozi uliopatikana na unaoendelea kupatikana na uchaguzi huu ni batili pia. Haramu haijawahi kuwa halali. SIMPLE MATHEMATICS.

Kwangu mimi Suphian, ndoto yangu kuu ya kuona Taifa langu huru na lenye kufuata misingi ya Haki ni Lulu zaidi ya maslahi ya Chama cha siasa nilipo au yeyote ninayemwamini katika Siasa au nje ya siasa.

Kama nilivyoahidi wakati wa Sakata la Wabunge 19 wa CHADEMA, kwamba siwezi kumumunya maneno pale haki ikipindishwa hata kama na Chama changu, hivyo NATANGAZA: SIUNGI MKONO MAAMUZI YA CHAMA CHANGU.

Hivyo naomba dunia ijue kuanzia Leo Desemba 07, 2020 mimi Suphian Juma Nkuwi rasmi NANG'ATUKA UANACHAMA wa ACT wazalendo ili kusimama na HAKI, kusimama na familia za ndugu waliouawa, kutekwa, kufungwa na kuumizwa wakipigania Uchaguzi Huru, Haki na unaoaminika.

Asante Kiongozi wa ACT wazalendo na Kaka yangu, Zitto Kabwe na Chama kwa ujumla kwa malezi yenu ya KUSIMAMA NA HAKI mliyonipatia tangu mwaka 2015 nilipojiunga nanyi, nawatakia kila kheri.

Suphian Juma,
Aliyekuwa Mgombea Ubunge, ACT wazalendo 2020-2025 Singida Magharibi.

Desemba 07, 2020.

Juma.jpg
 
Kwa sasa upinzani halisi ni CHADEMA tu. Wanaishi katika kile wanachokisema na kukiamini.

CHADEMA wanasema kilichofanyika October, 2020 ni uchafuzi uliovuka mipaka yote ya kidemokrasia toka kuwepo kwa taifa la Tanzania. Na wamesimamia hicho hicho mpaka sasa.
 
Hongera kwa uamuzi makini; ila bado najiuliza hili linawezekana vipi mahali tulipoambiwa uamuzi ule umefikiwa na wanachama wote kwa asilimia zote?

Hili linathibitisha wanachama wameburuzwa kufikia uamuzi ule.
 
Mkuu unaleta UANAHARAKATI katika mbio za SIASA ?!!

Ninyi ndio mnaowachanganya wafuasi wenu kwa KUWADHANISHA ya kwamba MAMBO YENU siasani ni sawa na zile harakati za akina Ralph Abernathy, Fannie Lou Hamer, Desmond Tutu na wengineo...

Hivi mnashindwaje kuwa kama wanasiasa wa Kenya akina Raila Odinga, Kenyatta, Musalia Mudavadi Rutto na wengineo...?!!!

Ama hao ni "wanafiki"?!!
Ama hao si WANASIASA wa kweli bali "vibaraka na wachumia tumbo"?!!!

Leo hii mnataka mfanye LOBBYING ZA KIHARAKATI na si za KISIASA ndani ya VYAMA VYA SIASA.....

Boutrous Boutrous Ghali(former UN SG) alipata kusema "ONLY STUPID PEOPLE DO NOT CHANGE THEIR MINDS"

Endeleeni kusubiri UJIO wa VYAMA MALAIKA kutoka MBINGUNI.....


Kijana Muuza Al Kasus
Tandale
 
Angeshinda ubunge hata asingejitoa chama. Kweli njaaa mbaya na ina mambo mabaya sana
 
Kwa sasa upinzani halisi ni CHADEMA tu. Wanaishi katika kile wanachokisema na kukiamini.

CHADEMA wanasema kilichofanyika October, 2020 ni uchafuzi uliovuka mipaka yote ya kidemokrasia toka kuwepo kwa taifa la Tanzania. Na wamesimamia hicho hicho mpaka sasa.
Upo sahihi
Ila hata uchaguzi wa 2015 walikuja na ngonjera kama hizo na hatimaye walikwenda bungeni kuapishwa.
Tofauti kubwa aliojiktokeza kwa mwaka huu ni kukosekana kwa kundi kubwa la wabunge tu.
 
Back
Top Bottom