superstar

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,223
Supasta alipopata mkwanja
akaamua kuhamia Masaki na mke
na mwanae. Siku moja mwanae
alipokuwa anacheza na manati
akavunja kioo cha nyumba ya
jirani. Supastar na mkewe
wakaamua kumfuata mwenye
nyumba wakamuombe msamaha.
Walipogonga mlango akafukua
mbaba mmoja;
MBABA: karibuni
SUPASTA: Samahani sie
tumehamia karibuni nyumba ya
jirani, mwanetu kavunja kioo
chako kwa bahati mbaya,
tumekuja kuomba msamaha na
kuona kama tunaweza
kutengeneza
MBABA: Karibuni kwenye kiti
niwahadithie kitu. Kwanza mimi
nawashukuru nyinyi. Mimi ni
ZIMWI nilikuwa nimefungiwa kwa
zaidi ya miaka 200 kwenye
kichupa kilikuwa kwenye kile
chumba ambacho dirisha
limevunjwa, chupa nayo
imevunjika nami nimekuwa huru,
kwa hiyo kwa shukurani ombeni
chochote mtakacho nitawapa
SUPASTAA:Mi naomba niwe
bilionea mpaka nife
MBABA: Hilo jambo dogo sana
kwangu, umepata na kesho
utaamka tajiri
MKE WA SUPASTA: Mi nataka niwe
na nyumba kila nchi duniani na
niwe na biashara Dubai na China
na HongKong
MBABA:Umepata kuanzia kesho
hayo ni yako. Mimi nawashukuru
kwa uhuru wangu lakini nina
ombi dogo.
SUPASTAA: Sema tu
MBABA: Mi naomba nilale na mkeo
leo tu, unajua kifungo
nilichofungwa kilinizuia kila kitu.
Asubuhi ikifika hamtaniona tena,
itakuwa siri yetu
Supasta na mkewe wakajadili,
wakaona utajiri waliopata ni
mkubwa sana hilo jambo ni dogo
wakakubali sharti. Mke akalala
kwa Mbaba mpaka asubuhi.
Wakati mke akijitayarisha kurudi
kwake Mbaba akakohoa kidogo;
MBABA: We una miaka mingapi na
mumeo ana miaka mingapi??
MKE: Mume wangu 32 na mimi 30
MBABA: Sasa nyinyi wakubwa
wazima mpaka leo mnaamini stori
za MAZIMWI?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom