Jibu ni kwamba utakaaje tena uswahilini nawe umeshanyaka mikoko, si watakuibia, au kukupasulia windscreen!Wana JF nilisikia dogo mmoja wa bongofleva redioni kwamba ameshakuwa superstar sasa hawezi kuishi tena uswazi, nisaidieni superstar ni mtu wa aina gani?
Wadau mbona mmemshambulia sana bwana mdogo?
Labda dogo hakuwa straight kwenye hoja yake, ingawa na mimi niliguswa kidogo na kusikia kwamba eti msanii wa bongofleva aliyejinyakulia tuzo nyingi kuliko msanii yeyote yule kwenye 2010 Kilimanjaro Music Awards anayejulikana kama Diamond Platinum anaishi Tandika.
Kweli Celebrity unaishi Tandika???????
Thanks Mkuu kwa kuliona hilo... kwanza lazima tujue supa staa ni nani? unaweza kuwa celebrity na usiwe supa staa au unaweza kuwa popular tu lakini si supa staaCelebrity anatakiwa aishi wapi mkuu? Masaki? Oysterbay? Upanga? au wapi?
Duh! Unaimbia Dar Modern Taarab au Melody?asanteni sana kwa kunikaribisha vyema japo sikupiga hodi, si unajua watoto wa uswazi milango shuka hutabisha vipi hodi nawe bubu!!
Du we mkail milango shuka kweli hodi utabishaje sasaasanteni sana kwa kunikaribisha vyema japo sikupiga hodi, si unajua watoto wa uswazi milango shuka hutabisha vipi hodi nawe bubu!!
Hivi jamani mnakumbuka issue ya Muumini Mwijuma aka kocha wa Dunia na kisa chake cha kuondoka tamtam? Issue kubwa ilikuwa ni u-celeb wa Muumini. Yeye hoja yake ilikuwa anataka uongozi wa tamtam chini ya Mama Asha Baraka umpatie gari na nyumba yenye hadhi inayoendana na jina lake kwenye jamii.
Alilalamika kwamba haiwezekani yeye kila siku anavyoenda kwenye mazoezi na show za hapa mjini apande madaladala, hii kwake ilikuwa inamshushia hadhi kwenye jamii.
Mfano mwingine ni wasanii wa bongo fleva na waigizaji ambao wakipigiwa simu na vituo vya TV kwamba wanawafuata kwa ajiri ya interviews, basi wasanii hao uomba/uazima magari na nyumba za watu wengine ili angalau waonekane wako juu kimaisha.
Binafsi kuna mwigizaji mmoja kila jumamosi anakuja kuazima gari yangu aende nayo kwenye tamasha la wasanii pale Leaders Club, nikimwambia panda daladala anasema eti ooh yeye kioo cha jamii hawezi panda daladala magazeti yatapata headlines!!
Wadau mnafikiri hawa vijana wanafanya hivi ili iweje?