'Multipolar world' haitakuja kwa vikao na 'wishful thinking'

'Multipolar world' haitakuja kwa vikao na 'wishful thinking'

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
65,015
Reaction score
111,415
Kuna mazungumzo mengi sana ya kuondokana na ulimwengu ambao taifa moja lina nguvu na ushawishi mkubwa zaidi duniani(unipolar) kwenda kwenye mfumo ambao mataifa kadhaa yatakuwa na ushawashi na nguvu kubwa duniani(multipolar).

Kihistoria unipolar world haikuja kwa vikao, Marekani au West kwa pamoja kama block haijawa sole superpower wa dunia kwa sababu ya kufanya vikao. West kuwa unipolar superpower ni historia ndefu ya mapinduzi ya kisiasa, kijamii na uchumi ndani West na kuweza kupeleka mambo hayo kote duniani kwa ushawashi na nguvu wakati mwingine.

Leo kuna mataifa wanaitisha vikao vya kujadiliana nao kuwa sehemu ya superpowers. Wanakaa watu ambao hakuna teknolojia za maana zinazovumbuliwa nchini mwao za kuleta maendeleo kwao na kwa wengine duniani wanataka na wao watambulike. Utakuaje superpower power bila teknolojia ya kuwazidi wengine?!

Wanakaa watu ambao siasa zao za ndani sio shirikishi halafu wanataka nao kuwa na ushawashi kwa wengine duniani kama superpower. Unakuaje superpower wakati jinsi unavyoongoza wengine ndani kwako hakuna tofauti kwa ubora na wale wanaokutazama kama mfano?

Wanakaa watu ambao utamaduni wao hauvuki mipaka yao, utamaduni wao ni local lakini wanataka kutambulika kama na wao ni superpowers. Utamaduni ni nyenzo ya ushawashi na kuwavuta watu pamoja zaidi.

Utasikilizwaje kama superpower wakati huna utamaduni wako unique ambao unafurahiwa na kutumiwa kwingine duniani?
 
Hiyo multi polar hatokaa itokee Dunia hii lazima kwenye huu msitu unaitwa Dunia apatikane mbabe mmoja, na mwenye akili ndie atakayetawala Dunia.
Lazima vita zipiganwe iwe kwa software au hardware
Nyakati mpya zinakuja
 
Matatizo ya sasa hayajaletwa na mataifa yanayo-ongelea multipolar world...Shida zote hizi ni jamaa mmoja (USA) anayewaza kuzuia mataifa mengine kwenda na interests zao...Dunia imebadilika...akae kwa kutulia, miaka hii sio 1960's or 70's alipokuwa free kuweka mapinduzi na kuondoa viongozi asiowataka..ubabe huo ulimlipa sana...

Ujinga huo anashindwa sasa, kajaribu Ukraine 2014...matokea yake vita imepiganwa mwaka wa 9 sasa..achilia mbali na SMO ya 2022...maelfu ya wananchi wasio na hatia wamekufa....UJINGA tu huu.....Kila mtu sasa hivi anavimba.....Venezuela kavimba, Iran, India, China, Urusi hata Afrika tumewagomea this time...ohh sijui tuiwekee vikwazo Urusi, mara Zelensky aongee...watu tumewapuuza, tukaendelea na issue zetu ( dharau hii), mpaka wanahangaika kutumatuma viongozi wao kutwa kudhurula Afrika...
Saudi na Iran wameona waendelee na utaratibu wa amani.
Saudia na Yemen...wameweka watulie..
Huko far east wanaongelea kuwa na mbadala wa SWIFT..hapo naongelea Indonesia na wengine....

USA anatapatapa tu...HUWEZI kucontrol dunia katika karne hii....watu wana-access na information, knowledge vibaya mno...

USA atulie tu....awe kama Ujerumani.kimya lakini wako vizuri...kiuchumi, kimaendeleo, kila kitu..hawako kwenye mi-vita -vita....walijifunza na kilichowakuta 1945..
 
Back
Top Bottom