Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,724
- 729,891
Makengeza ni aina ya ulemavu wa macho ambao mwenye hilo tatizo akitaka kuangalia mbele ni lazima ageuke kidogo kushoto ama kulia ndio anaweza kuona anachotaka kuona
Kwenye mikabala ya kugundisha kuna gundi za aina mbalimbali
-superglue hii ni gundi hatari sana na ikikamata mahali haiachii katu na hukamata haraka sana chini ya sekunde 59
-OKO ni aina ya gundi ya kuzibia pancha, gundi hii hukaa ndani ya tairi ikisubiri pancha na ikitokea OKO haraka sana hufanya yake kabla upepo haujavuja hivyo kuokoa muda usumbufu na pesa
- A-B glue unachanganya kemikali mbili tofauti, nayo ni kali sana
Hii ni mifano michache tu ya gundi zinazofanya kazi moja lakini katika mahitaji tofauti
Serikali ya awamu ya tano imeingia na mfumo mpya! Kutovumilia ujinga wowote ule hasa kwenye utendaji na majukumu... Tumeshuhudia watu wazito hasa wakichukuliwa hatua kali bila kupepesa macho.....napongeza sana hili kuna watu walikuwa ni untouchables! Hawagusiki
Lakini sifa hii imetiwa doa kisiki kimoja kidogo sana! Mpaka najiuliza hiki ni kisiki kweli ama ni mwamba mkubwa uliojitokeza juu kama kisiki?
Kigugumizi hiki cha kumwajibisha huyu mtu aliyethibitika kuwa na makosa mengi mkubwa kinatoka wapi? Yani kwa huyu mtu macho yanapata ulemavu wa makengeza ghafla? Kwamba kumwangalia mpaka ugeuze shingo kama kuku?
Tuhuma hizi za kumiliki mali inayozidi kipato chake
Tuhuma za kughushi jina
Kusafiri nje ya nchi kwa mapumziko na kutalii (wengine wameadhibiwa vikali kwenye hili
Tuhuma za kuwa na mahusiano na mtuhumiwa wa dawa za kulevya
Nk nk
Nimekaa najiuliza huyu kabandikwa na gundi gani hiyo Mpaka iwe ngumu namna hii kumng'oa? Katumia super glue OKO ama A-B glue kubandikwa hapo alipo?