Supastaa Mpya wa Bongo Kuzawadiwa Tsh. Milioni 25

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,324
33,128


3291098.jpg

Masupa Staa wajao wa Bongo Thursday, October 08, 2009 9:29 PM
Mshindi wa shindano la kumtafuta nyota mpya wa Bongo "Bongo Star Search" ataibuka na kitita cha shilingi Milioni 25. Mdhamini mkuu wa shindano la Bongo Star Search, Kampuni ya Vodacom, leo imetangaza zawadi ya washindi watakaoibuka katika kinyanganyiro hicho.

Akitangaza zawadi hizo Meneja wa Udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna alisema kuwa fainali za shindano hilo zitafayika katika ukumbi wa Diamond Jubilee mnamo tarehe 13 mwezi huu.

Katika fainali hizo mshindi wa kwanza ataibuka na zawadi nono ya shilingi Milioni 25, mshindi wa pili atajinyakulia shilingi Milioni 5, mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi Milioni 3 ambazo ni fedha taslimu pamoja na zawadi ya shilingi laki tano kutoka kwa Shear Illusion ambao ni moja ya wadhamini.

Mshindi wa nne ataondoka na shilingi milioni moja na nusu na mshindi wa tano ataondoka na shilingi milioni moja.

Kwa upande wa burudani, safu ya burudani itaongozwa na Shaa, Feisal Ismail, baby Madaha, Abubakar Mzuri na wasanii wengine kibao aliseama Ritta.

Washindi waliofanikiwa kuingia katika tano bora ambao watagombania nafasi ya kuwa supa staa mpya wa Bongo ni Paschal Cassian wa Mwanza, Beatrice William wa mwanza, Peter Maechi toka mkoa wa Kigoma, Jackson George anayewakilisha mkoa wa Tanga na Kelvin Mbati toka Mkoa wa Dar es Salaam.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3291098&&Cat=8
 
Back
Top Bottom