Sungusungu wanaolinda mitaa Wana Elimu ya ulinzi?

Sungusungu wanaolinda mitaa Wana Elimu ya ulinzi?

Husika na mada tajwa hapo juu.
Ndugu wana Jf je hawa ndugu zetu sungusungu wana elimu ya ulinzi wa mitaa na usalama wa mali za raia.

Je, uwepo wao unatambulika kikatiba?

Naomba kuwasilisha ili tuweze kulijadili.

Karibu sana.
Walinde tu, huo ndio ulinzi shirikishi.
 
Husika na mada tajwa hapo juu.
Ndugu wana Jf je hawa ndugu zetu sungusungu wana elimu ya ulinzi wa mitaa na usalama wa mali za raia.

Je, uwepo wao unatambulika kikatiba?

Naomba kuwasilisha ili tuweze kulijadili.

Karibu sana.
Nadhani hawana, japo hawalalamikiwi Sana nawananchi Kama wale walinzi wenye elimu rasmi.
 
Katiba imeeleza kwamba suala la ulinzi na usalama ni JUKUMU la kila mtanzania.
Pia Sera ya taifa inaeleza hivyohivyo kwahiyo Polisi wametumia kichaka hicho kujifichia inawezekana labda kutokana na uchache wao vifaa vyao duni na kutelelekezwa Kwa kutopewa vitendea KAZI vya kisasa pamoja na Elimu kuntu ya kukabiliana na uhalifu.

Serikali kuona eneo hili si kipau mbele mfano ingewekeza kuwe na CCTV, MAGARI,MAFUTA FORENSIC SCIENCE NK wananchi/ sungusungu wangeachwa wafanye uzalishaji mwingine ili kuongeza tija.
 
Huwa wanaendaga vikozi vyao vidogodogo huko polisi...obay nk

Sahvi kuna maeneo mengine watu
Wameweka mpaka barriers

Ova
 
Hakuna elimu yoyte sungusungu lakin pia swala la sungusungu halipo kisheria kwa sasa lilifutwa miaka ya 1992-1994

Na hii ni baada ya sungusungu wengi kuwa chanzo cha matatizo kwenye Jamii Zao.
 
Zingatia "mamlaka ya serikali za mtaa" wana mamlaka ya kuweka sungusungu wenye uzoefu ili kulinda eneo lao. Nijibu swali, hawana elimu ya ulinzi ila ni uzoefu. Ila kutana nao ili uwajue zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi umenusurika kukamuliwa mbupu na panya road sungusungu tukakuokoa, leo unaulizia elimu yetu!!
 
Back
Top Bottom