Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."

Kuna watu wenye wivu, wanataka kujenga chuki dhidi ya kabila la Wasukuma kwa kuibua neno "Sukuma Gang". Hakuna kitu kama hiki!. Ni wivu tuu unawasumbua!
P
 
Wanabodi,

This is fact!. Jee udini huu ni dhana tuu ya udini au ndio ukweli wenyewe?. Na kwenye udini ninauliza akiwa Mkristu ni lazima awe Mkatoliki?.

Rais Nyerere alikuwa Mkristo Mkatoliki, Rais Mkapa alikuwa Mkristo Mkatoliki, na kwasababu rais aliyepo sasa ni Muislam, hii maana yake rais ajaye ni zamu ya Mkristo sasa subirini rais ajaye na muangalie kwa makini atakuwa ni Mkristo wa dhehebu gani, ukifika wakati huo ndipo mtanielewa!.
Nauliza tuu?

Paskali
Kumbe Mayala naye MDINI... Asee
Paskali ni mdini haswa. Ipo comment yake moja kuhusu Uislam ukiiona hutoamini.
Mkuu Chum Kane , na Relief Mirzska, kwanza angalia tarehe ya bandiko.
Jobo hili analijua kuwa 2025 ilikuwa ni zamu ya Muislamu, hivyo Mama kumsingizia Jobo ana homa ya 2025 ni kumuonea!.

Jobo ni mwana CCM mwandamizi, anajua utaratibu wa CCM, rais hapingwi half term, hivyo wana CCM wote wanajua 2025 ni Samia!, kusingizia homa ya 2025 sio kuwatendea haki.
na katika hoja zote ile hoja ya akiwa Mkristu, ni lazima awe Mkatoliki, haijawahi kujibiwa!, kama unadhani huwa inatokea tuu akawa ni Mkatoliki, endelea kuamini hivyo!, Edward Lowassa angekuwa Mkatoliki, ndie angekuwa rais wetu ile 2015!.
P
 
Mkuu Chum Kane , kwanza angalia tarehe ya bandiko.

Kweli ni homa ya uchaguzi 2025.lakini utamaduni au sera ya ccm ni kuwa Rais anatoka bara makamu anatoka zanzibar.Angalia baada ya Mwinyi hakuna mzanzibar aliyekuwa Rais.Kwahiyo hata ingekuwa ni zamu ya muislam bado ccm inataka mgombea huyo atoke bara.pia ukumbuke hata hiyo ya kubadilishana waislam na wakristo hakuna mahala palipoandikwa ni busara tu ya wazee wetu.
 
Mkuu Chum Kane , kwanza angalia tarehe ya bandiko.
Jobo hili analijua kuwa 2025 ilikuwa ni zamu ya Muislamu, hivyo Mama kumsingizia Jobo ana homa ya 2025 ni kumuonea!.

Jobo ni mwana CCM mwandamizi, anajua utaratibu wa CCM, rais hapingwi half term, hivyo wana CCM wote wanajua 2025 ni Samia!, kusingizia homa ya 2025 sio kuwatendea haki.
na katika hoja zote ile hoja ya akiwa Mkristu, ni lazima awe Mkatoliki, haijawahi kujibiwa!, kama unadhani huwa inatokea tuu akawa ni Mkatoliki, endelea kuamini hivyo!, Edward Lowassa angekuwa Mkatoliki, ndie angekuwa rais wetu ile 2015!.
P
Kaka Mkubwa Paskali, andiko lako limeishi kwa miaka mingi likiwa detailed with facts na relevance kwa mambo mengi sana.

Ila jana watu wengi wanajiuliza, kwanini mama alionekana kuwa na hasira sana na Job, kwani Job kawahi kuonesha nia ya 2025, sidhani na hapa nakubaliana nawe.

Pengine tujiulize au tukuulize kaka yetu kwani umekuwa kwenye game ya kuwa political analyst kwa muda wa kutosha; Au Job ni mshenga wa mtu kwa 2025? Huyo "anaeshengewa" ni nani?

Mama SSH, jana pia akafungua mjadala ndani ya mjadala, kuwapiga chini wenye kiu ya "UKULU" 2025, ndio kusema "akila vichwa" tujue hao waliowekwa "pembeni" walikuwa wana "nia"?

Cha mwisho, sikuwahi kusikia "serikali ya mpito"; nani alianzisha hii sakata huko kwenye dunia ya politik zetu huku inajulikana kabisa kikatiba likitokea la kutoka kwa #1, #2 ana-take over. Sema hatukuwahi kuwa na hiyo experience kama jirani Kenya, ila hatimaye na sisi March 17 pale Mzena, mzee upepo ulikata na #2 aka-take over.

Pengine kuna siku tuwe na mjadala huru kuhusu marekebisho ya katiba hii au mpya kama itakuwa discretion ya Mkulu SSH, kwanini nchi isubiri siku moja, mbili ili immediate successor ale kiapo? It is obvious in the absence of #1, the 2nd in command ana-take over, kwanini ilichukua siku 2 then ndipo #2 rasmi akavaa viatu vya U-CinC?
 
Pengine tujiulize au tukuulize kaka yetu kwani umekuwa kwenye game ya kuwa political analyst kwa muda wa kutosha; Au Job ni mshenga wa mtu kwa 2025? Huyo "anaeshengewa" ni nani?
Kama JPM angefika 2025, JPM alipanga kumpa Bashiru, huku Kasimu alikuwa amepania kupokea kijiti!.
Hayo mabadiliko, anampumzisha Kasimu!.
P
 
Jee Watanzania hawana kanda zao?. JK Nyerere alitoka kanda ya Ziwa, Mwinyi akatoka Zanzibar, Ben akatoka kanda ya Kusini, JK ametoka kanda ya Mashariki, Kanda ya Kati by now bado haina mtu mwenye caliber na uwezo wa kuwa rais wa JMT kwa sasa (sorry), hivyo kanda zilizobakia ambazo bado hazijatoa rais ni Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini!, hivyo rais wa 2015 lazima atoke ama Kanda ya Ziwa, ama Kanda ya Kaskazini!. Kwa vile Kanda ya Kaskazi inaelezwa kulaaniwa na Nyerere kufuatia kisa cha Mangi Mkuu Thomas Marealle kumkwamisha Nyerere kwa kutaka Kanda hiyo ndio ipewe uhuru kwanza kwa hoja Tanganyika as a whole bado haijawa tayari, hivyo sasa rais wa 2015 lazima atoke Kanda ya Ziwa!.

Paskali

Rejea
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu ...
Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
Hatimaye kile kitendawili cha Mikutano ya hadhara sasa rasmi kimeteguliwa , hii ni baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kutoa Ratiba yake .

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Itifaki wa Chama hicho John Mrema imedai kwamba , Jiji la Mwanza limeteuliwa kuwa la Kwanza kwa Chadema kufanya mkutano wake wa Hadhara , Mkutano huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya Kitaifa ya Mikutano ya hadhara tangu kuvumbuliwa kwa Tanzania utafanyika tarehe 21/01/2023 .

Mungu ibariki Chadema
Kwa kweli nawapongeza sana kuanzia Mwanza, kwasababu sasa hatimaye Chadema imejitambua na kujua kanda determinant za ushindi kwa uchaguzi wa urais Tanzania ni kanda gani, hivyo wameanzia hapa.
Ushauri huu ulitolewa siku nyingi nyuma!. Mwaka 2010 nilipandisha bandiko hili, CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! humo nikasema
Wanabodi,

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa vile CCM imechokwa na imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kuongeza offensive ili kuisindikiza CCM kaburini, kwa kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, kwa kuonyesha Watanzania kuwa mmekomaa na mko tayari kutawala, hivyo Watanzania watawamini watawakabidhi nchi mwaka 2015.

Sehemu muhimu kabisa kwa Chadema to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM imeumia sana kupoteza Kanda ya Ziwa na wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost, hivyo Chadema itumie uwezo wake wote kulinda what it has!.

Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profit making. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji sio wanasiasa wafanyabiashara. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!.
Paskali
Mwaka 2012, nikapandisha uzi huu
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! humo nilisema
Wanabodi,
Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote, all its mighty powers by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na naomba mshishangae, kama ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa hongo kubwa kabisa ya mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Laurent Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais as long as atatoka Kanda ya Ziwa kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!, the end justifies the means.

Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utajitambua kwa kushikilia kwa makini kile kilicho mkononi na kuongeza juhudi za kuimililki kanda ya Ziwa, hivyo vita kuu ya kisiasa nchini Tanzania kuelekea 2015 ni nani ataimiliki Kanda ya Ziwa. Chadema ikifanikiwa, CCM inapigwa chini, ila CCM ikifanikiwa kuikomboa Kanda ya Ziwa, then 2015 ni CCM tena, na kitakacho fuatia kwa CCM ya 2015 ni kuikomboa Kanda ya Kaskazini na kusema ukweli hii ndio itakuwa kazi ngumu kweli kweli, ila kama itatumika ile 'universal language', kuna msemo "hakuna mkate mgumu mbele ya chai", mkate hata uwe mgumu vipi ukiuchovya ndani ya chai, unalainika!

Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za Ukanda, zitajenga chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.

Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.

Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, Kanda yenu ndio imependelewa sana, inaongoza kwa mashule na wasomi, inaongoza kwa mahospitali!, KCMC, Mawenzi, Kibongoto, Mt. Meru, Seliani, Dareda, etc, Inaongoza kwa vivutio vya utalii, Mt. Kilimanjaro, Mt. Meru, Serengeti, Ngorongoro, Seronera, Manyara, Inaongoza kwa barabara za lami hadi vijijini, inaongoza kwa umeme vijijini, inaongoza kwa maendeleo, inaongoza kwa kutoa wanawake wife material, ukioa mchagga umeoa maendeleo, hivyo msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.

Wito Kwa Wa Kanda ya Ziwa.
Tusikubali kutumiwa kama ngazi ya wengine kupandia kisiasa, kwa vile na mimi ni mtu wa Kanda hii na sisi ndio determinant ya nani anashinda na kukikalia kile kiti cha ikulu yetu, tusikubali kuendelea kutumika tuu kama ngazi kwa wengine kupandia, au kuendelea kuwa na upendo wa mshumaa kumulikia wengine huku kwetu kunateketea, Kanda hii ndio Kanda yenye watu wengi, ndio Kanda yenye mijitu yenye nguvu inayokula na kushiba, ndio Kanda tajiri kuliko Kanda zote, ndio yenye madini ya dhahabu na almasi, ndio wenye Ziwa Victoria lenye samaki watamu Sato, tusikubali kutumiwa kama dodoki kuwasafishia wengine au dekio baada ya deki linatupwa kule, sisi tuna kila aina ya utajiri lakini very unfortunately watu wetu ni masikini wa kutupwa!. Angalia wenzetu wa Kaskazini mbona wameweza kulibwaga hili lidubwana na wanapata maendeleo, na sisi tuamue kulibwaga unless kama 2015 atakuwa ni mmoja wetu!.

Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!

Wasalaam.

Paskali
Sasa Chadema ndio wanaamka kujua nguvu ielekezwe wapi, huu ni mwanzo mzuri!, tatizo la tonge hilo, waliolishika tonge mdomoni wanajua, jee watakubali kunyang'anywa tonge mdomoni?
P.
 
Wanabodi,

Wanabodi nauliza, hii sumu ya siasa za udini, ukanda na ukabila are they real au ni dhana tuu?!.

Tushukuru marais wa Tanzania, wote wametoka katika makabila madogo non dormant tribes, siku akiingia rais kutoka haya makabila makubwa, na ikatokea anatokea kwenye hizi dominant tribes na akiwa ni mkabila, kutazuka ukabila wa ajabu, hadi mtashuhudia watu wakihutubia umma kwa lugha za kabila zao ndipo watu humu mtanielewa nilikuwa nazungumzia nini!.

Hii dhambi ya mbegu ya sumu ya siasa za udini, ukabila na ukanda, zimepandwa na CCM, zimelelewa na CCM na hatimaye 2015, CCM isipozikumbatia siasa hizi ili isalimike, then CCM itavuna ilichopanda!.

Jee mbegu hii ya sumu kaipanda nani?, jee tunaweza kuipiga vita kwa kuikataa tuu, (denial) au kwa kuikanusha tuu (negation) or au tunatakiwa kuubali ukweli mchungu na kukabiliana nao (facing the problem), kwa kukubali tuna tatizo la udini na ukabila! .

Nauliza tuu?

Paskali
Sukumagang ni ITIKADI iliyoasisiwa na JPM kwa manufaa ya wasukuma ukiwemo wewe Paskali Njalah Mayala, na kwa faida yako Sukumagang

Wasukuma kama hilo ni tatizo fanyeni kazi ya kulifuta maana hata wewe hujawahi kulishutumu huko nyuma!
Mkuu MTK , angalia tuu tarehe ya bandiko ujue watu huu udini, ukanda na ukabila, watu tumeanza kuukemea lini.
P
 
Wanabodi,

Swali hili niliwahi kuliuliza huko nyuma, thread iliunganishwa na thread yenye statement ya "tunanyemelewa na udini"!. Ile thread ni ya statement, mimi ni swali, kuwa Jee huu udini, Ukanda na Ukabila unaozungumzwa ni kweli upo na una exist au ni dhana tuu?. Mode ukiona na hii thread bado ina fit kwa swali kuunganishwa na statement, then, unganisha tena!.

Paskali.

Wanabodi nauliza, hii sumu ya siasa za udini, ukanda na ukabila are they real au ni dhana tuu?!.

Jee Watanzania si wana dini zao?, jee kuna ubishi kuwa alipoanza rais Mkristu, Mkatoliki, JK Nyerere, alipoondoka Mwinyi aliingia tuu by a mare chance?, no!. Miongoni mwa sababu za Mwinyi kuingia ni pamoja na dini yake!, this is a fact!. Alipoondoka Mwinyi si aliingia Ben?, inamaana aliingia tuu merely by chance and by chance akawa ni Mkiristu Mkatoliki? na alipotoka JK nae akaingia by mere chance, and just by chance tuu JK akawa ni Mwislam?.

Tutake tusitake, japo haijaandikwa popote wala haijapangwa popote na yeyote lakini kwenye urais wa JMT kuna kupokezana silently hata kama kunaonekana kama ni by chance tuy, then jee tuendelee ku play by chance?. Kwenye uchaguzi uliopita kuna vyama vilipata kura nyingi maeneo ya dini fulani, and this is a fact!. Kuna taasisi na makundi ya watu wali waendorse wagombea fulani kutokana na dini zao!. This is fact!. Jee udini huu ni dhana tuu ya udini au ndio ukweli wenyewe?. Na kwenye udini ninauliza akiwa Mkristu ni lazima awe Mkatoliki?.

Rais Nyerere alikuwa Mkristo Mkatoliki, Rais Mkapa alikuwa Mkristo Mkatoliki, na kwasababu rais aliyepo sasa ni Muislam, hii maana yake rais ajaye ni zamu ya Mkristo sasa subirini rais ajaye na muangalie kwa makini atakuwa ni Mkristo wa dhehebu gani, ukifika wakati huo ndipo mtanielewa!.

Jee Watanzania hawana makabila yao?, Lazima tukubali tukatae, Tanzania tuna makabila makubwa, dominant tribes ambayo yana dominates. na makabila madogo, non dominate tribes. Kati ya haya dominant tribes lazima tukubali kuna baadhi yake wana ukabila wa kutisha!, kuna baadhi yake wana nyodo za ajabu!, kwani iliwahi kutamkwa au kuandikwa popote kuwa watu wamakabila fulani sio hawafai kuchukua urais wa nchi hii, bali hawawezi kupewa kwa sababu matokeo tunayajua!, hivi tuu walivyo na hizo nafasi kubwa kubwa walizo nazo sasa tayari ni miungu watu, wakiukwaa urais si ndio wataota pembe kabisa?!.

Ni general unwritten public opinion kuwa rais wa nchi hii asitokee kwenye hizi dorminant tribes!. Kuna wagombea fulani walinyimwa kura maeneo fulani kwa kuitwa wakuja!. Kuna mikoa fulani mgombea ambaye sio mzawa huitwa "kyasaka" na wanakuambia kabila letu kamwe haliwezi kumchagua "kyasaka"!. Jee huu soi ukabila?. Huu ukabila ni dhana tuu ya ukabila au ndio ukweli wenyewe kuwa kuna ukabila wa kichini chini kwenye siasa kwenye baadhi ya maeneo?.

Tushukuru marais wa Tanzania, wote wametoka katika makabila madogo non dormant tribes, siku akiingia rais kutoka haya makabila makubwa, na ikatokea anatokea kwenye hizi dominant tribes na akiwa ni mkabila, kutazuka ukabila wa ajabu, hadi mtashuhudia watu wakihutubia umma kwa lugha za kabila zao ndipo watu humu mtanielewa nilikuwa nazungumzia nini!.

Jee Watanzania hawana kanda zao?. JK Nyerere alitoka kanda ya Ziwa, Mwinyi akatoka Zanzibar, Ben akatoka kanda ya Kusini, JK ametoka kanda ya Mashariki, Kanda ya Kati by now bado haina mtu mwenye caliber na uwezo wa kuwa rais wa JMT kwa sasa (sorry), hivyo kanda zilizobakia ambazo bado hazijatoa rais ni Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini!, hivyo rais wa 2015 lazima atoke ama Kanda ya Ziwa, ama Kanda ya Kaskazini!. Kwa vile Kanda ya Kaskazi inaelezwa kulaaniwa na Nyerere kufuatia kisa cha Mangi Mkuu Thomas Marealle kumkwamisha Nyerere kwa kutaka Kanda hiyo ndio ipewe uhuru kwanza kwa hoja Tanganyika as a whole bado haijawa tayari, hivyo sasa rais wa 2015 lazima atoke Kanda ya Ziwa!.

Kwa vile 2015 kwa sasa bado ni mbali, hivyo endeleeni kudhani kuwa hii ni dhana tuu, ila hili litakapo tokea, rais wa 2015 akatoka kanda ya Ziwa, ndipo mtanielewa, nazungumzia nini!. Huu ndio ukweli wenyewe, hivyo in future, watu wa Kaskazini wasiendelee kupoteza muda wao kuuwazia urais, unless kama ni kwa kujifurahisha tuu!. Huu ni ukanda!.

Juzi nilipandisha hii thread iliyosema Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
nilishambuliwa sana kwa siasa za ukanda ila this is a fact!. Nikasisitiza CCM haina namna yoyote ya kujiokoa ili ipendeke na kutoa angalizo kuwa majaaliwa ya CCM kuendelea kutawala nchi hii, yanashikiliwa na Kanda ya Ziwa, hivyo nikasema kama ikitokea na Kanda ya Ziwa wakaichoka CCM kama walivyochoka Kanda ya Kaskazini, 2015 CCM inapigwa chini, kichwa chini miguu juu huku mnashuhudia bila kuamini macho yenu wala masikio yenu!.

Hii dhambi ya mbegu ya sumu ya siasa za udini, ukabila na ukanda, zimepandwa na CCM, zimelelewa na CCM na hatimaye 2015, CCM isipozikumbatia siasa hizi ili isalimike, then CCM itavuna ilichopanda!.

Jee mbegu hii ya sumu kaipanda nani?, jee tunaweza kuipiga vita kwa kuikataa tuu, (denial) au kwa kuikanusha tuu (negation) or au tunatakiwa kuubali ukweli mchungu na kukabiliana nao (facing the problem), kwa kukubali tuna tatizo la udini na ukabila! .

Nauliza tuu?

Paskali

Rejea
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu ...
Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
Paskali,
Naomba unifahamishe ikiwa unafahamu.
Tatizo la udini limeanza lini Tanganyika?

Watu gani walioanzisha udini?
Mkuu Maalim Mohamed Said,
Udini Tanzania ulianzishwa na Wakoloni na missionary maeneo yenye mazao ya biashara ndio walijenga makanisa na Shule za misheni, ni watu wa makabila ya maeneo yenye mazao ya biashara ndio walikuwa na uwezo wa kiuchumi kuwalipia watoto wao karo, hivyo wale wa dini nyingine wao walijenga tuu madras.

Uzuri wa Shule za misheni, hawakuwabagua Waislamu, hivyo kuna kundi kubwa la wasomi wa Kiislamu kabla ya uhuru wameokolewa na hizi Shule za Mission.

Tulipopata uhuru, tukajikuta kazi zote za maana za wazungu zinashikwa na Wakristo ubaguzi wa Wabenzi na Makabwela ukaanza.

Mwalimu Nyerere akatangaza elimu bure ili kila Mtanzania apate fursa sawa, ndipo akagundua akili za makabila wanaokula vizuri sio sawa na akili za baadhi ya maeneo, watoto wanaopasi kwenda sekondari ni wa makabila yale yale. Hivyo aka introduce affirmative action kwa baadhi ya maeneo ili Watanzania wote waelimike.

Tukaachana na mitihani ya cambridge tukaanzisha Baraza letu la Mitihani, kisha akaweka different cut of points za ufaulu, ili Watanzania wote wapate fursa sawa.

Ili ndugu zetu Waislamu nao wapate fursa kama za Mission, Mwalimu akaivunja EAMWS
kwa kosa la kuwadumaza na kuwadunisha Waislamu kwa kuitegemea elimu ya madras pekee na kuanzisha kitu kizuri Bakwata ikaanzisha mashule ya Ilim Duniya na kuwaendeleza Waislamu kielimu.

Lakini licha ya Bakwata kuanzisha mazushule bado Shule za Mission ziliendelea kuongoza kwa kufaulisha Div 1 zikiongozana wakati Shule za Kiislamu zikivuta mkia kwa zero kuongozana hivyo idadi ya Waislamu wanaojiunga vyuo vikuu bado ikawa ndogo.

Hivyo zikitangazwa nafasi za ajira, wenye sifa wengi wanakuwa ni watu wa dini moja hivyo Waislamu kujiona kama wanakuwa marginalised!.

Mimi niliwahi kuuliza humu Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.

Ingefanywa sensa ya dini za vibaka walioko magerezani, wale wadada wanaofanya ile biashara, wanawake wanaoolewa na kuwa ma golikipa, au idadi kubwa ya watu wanaoishi kwenye umasikini uliotopea, mngeshangaa!.

Ukiondoa mwanzilishi huyo wa udini ambae ni mkoloni, Waislamu waliendelea kujibagua na mpaka kesho bado wanajibagua.

Hata kwenye vyombo vya ulinzi na kazi za ukakamavu niliwahi pia kuuliza humu Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?

Mwalimu Nyerere alikemea sana ubaguzi wowote, mfano ngoja tusubirie akiishamalizana na the Sukuma Gang, tuone nani wanafuatia!.
Pasco
 
Wanabodi,

Wanabodi nauliza, hii sumu ya siasa za udini, ukanda na ukabila are they real au ni dhana tuu?!.

Jee Watanzania hawana makabila yao?, Lazima tukubali tukatae, Tanzania tuna makabila makubwa, dominant tribes ambayo yana dominates. na makabila madogo, non dominate tribes. Kati ya haya dominant tribes lazima tukubali kuna baadhi yake wana ukabila wa kutisha!, kuna baadhi yake wana nyodo za ajabu!, kwani iliwahi kutamkwa au kuandikwa popote kuwa watu wamakabila fulani sio hawafai kuchukua urais wa nchi hii, bali hawawezi kupewa kwa sababu matokeo tunayajua!, hivi tuu walivyo na hizo nafasi kubwa kubwa walizo nazo sasa tayari ni miungu watu, wakiukwaa urais si ndio wataota pembe kabisa?!.

Ni general unwritten public opinion kuwa rais wa nchi hii asitokee kwenye hizi dorminant tribes!. Kuna wagombea fulani walinyimwa kura maeneo fulani kwa kuitwa wakuja!. Kuna mikoa fulani mgombea ambaye sio mzawa huitwa "kyasaka" na wanakuambia kabila letu kamwe haliwezi kumchagua "kyasaka"!. Jee huu soi ukabila?. Huu ukabila ni dhana tuu ya ukabila au ndio ukweli wenyewe kuwa kuna ukabila wa kichini chini kwenye siasa kwenye baadhi ya maeneo?.

Tushukuru marais wa Tanzania, wote wametoka katika makabila madogo non dormant tribes, siku akiingia rais kutoka haya makabila makubwa, na ikatokea anatokea kwenye hizi dominant tribes na akiwa ni mkabila, kutazuka ukabila wa ajabu, hadi mtashuhudia watu wakihutubia umma kwa lugha za kabila zao ndipo watu humu mtanielewa nilikuwa nazungumzia nini!.

Jee Watanzania hawana kanda zao?. JK Nyerere alitoka kanda ya Ziwa, Mwinyi akatoka Zanzibar, Ben akatoka kanda ya Kusini, JK ametoka kanda ya Mashariki, Kanda ya Kati by now bado haina mtu mwenye caliber na uwezo wa kuwa rais wa JMT kwa sasa (sorry), hivyo kanda zilizobakia ambazo bado hazijatoa rais ni Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini!, hivyo rais wa 2015 lazima atoke ama Kanda ya Ziwa, ama Kanda ya Kaskazini!. Kwa vile Kanda ya Kaskazi inaelezwa kulaaniwa na Nyerere kufuatia kisa cha Mangi Mkuu Thomas Marealle kumkwamisha Nyerere kwa kutaka Kanda hiyo ndio ipewe uhuru kwanza kwa hoja Tanganyika as a whole bado haijawa tayari, hivyo sasa rais wa 2015 lazima atoke Kanda ya Ziwa!.

Kwa vile 2015 kwa sasa bado ni mbali, hivyo endeleeni kudhani kuwa hii ni dhana tuu, ila hili litakapo tokea, rais wa 2015 akatoka kanda ya Ziwa, ndipo mtanielewa, nazungumzia nini!. Huu ndio ukweli wenyewe, hivyo in future, watu wa Kaskazini wasiendelee kupoteza muda wao kuuwazia urais, unless kama ni kwa kujifurahisha tuu!. Huu ni ukanda!.

nilishambuliwa sana kwa siasa za ukanda ila this is a fact!. Nikasisitiza CCM haina namna yoyote ya kujiokoa ili ipendeke na kutoa angalizo kuwa majaaliwa ya CCM kuendelea kutawala nchi hii, yanashikiliwa na Kanda ya Ziwa, hivyo nikasema kama ikitokea na Kanda ya Ziwa wakaichoka CCM kama walivyochoka Kanda ya Kaskazini, 2015 CCM inapigwa chini, kichwa chini miguu juu huku mnashuhudia bila kuamini macho yenu wala masikio yenu!.

Paskali
Mwl Nyerere, ila leo kunakitu. Jambo hili la ukabila Mwl alikemea sana; dalili au viashiria vyake, hongera Mwl. Leo hii tena baada ya miaka mingi kuna hisia za viongozi kutaka kupanda mbegu za ukabila. Tunaona kanda ya Wasukuma inaonesha bila wao, CCM itashindwa; viongozi wanahonga vyeo Wasukuma ili waichague CCM, jamani!

Uteuzi wa Biteko Doto, juzi uteuzi wa Makonda kisa ili Wasukuma wajue kuwa wao bado miamba hii kweli kwa Watanzania ni dhana mpya ili kujenga element za ukabila. Tunajifunza, Mwl alichaguliwa na Watanzania akiwa anatokea kwenye kabila dogo sana, Wazanaki; pia Mkapa kwa Wa Makua na Kikwete Wakwele. Hatujawahi taifa hili kuwaogopa Wasukuma.

Ikitokea Watanzania wakajua hili, ukabila uko njiani; kesho Wanyakyusa wataanza nao kuogopwa. Niliombee taifa letu, sisi tayari tumeshaunganishwa, hatuna ukabila.
Usiwe na wasiwasi kabisa na Wasukuma Tuhuma za Ukabila: Wasukuma si Miongoni mwa Makabila yenye Ukabila, tatizo ndio walio wengi!
P
 
Wanabodi,

Kwa vile 2015 kwa sasa bado ni mbali, hivyo endeleeni kudhani kuwa hii ni dhana tuu, ila hili litakapo tokea, rais wa 2015 akatoka kanda ya Ziwa, ndipo mtanielewa, nazungumzia nini!. Huu ndio ukweli wenyewe, hivyo in future, watu wa Kaskazini wasiendelee kupoteza muda wao kuuwazia urais, unless kama ni kwa kujifurahisha tuu!. Huu ni ukanda!.

Juzi nilipandisha hii thread iliyosema Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!
nilishambuliwa sana kwa siasa za ukanda ila this is a fact!. Nikasisitiza CCM haina namna yoyote ya kujiokoa ili ipendeke na kukubalika, natoa angalizo kuwa majaaliwa ya CCM kuendelea kutawala nchi hii, yanashikiliwa na Kanda ya Ziwa, hivyo nikasema kama ikitokea na Kanda ya Ziwa wakaichoka CCM kama walivyochoka Kanda ya Kaskazini, 2015 CCM inapigwa chini, kichwa chini miguu juu huku mnashuhudia bila kuamini macho yenu wala masikio yenu!.

Paskali
Wasiwasi wangu Kanda ya Ziwa ndio watakuwa wanaamua Nani awe Rais wa JMT kuanzia kwenye NEC ya CCM
Mkuu Yohana Mbatizaji, johnthebaptist , usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu Kanda ya Ziwa, ni Kanda determinant kwa sababu ndio inapiga kura inayoitwa a decisive votes kutokana na hii ndio Kanda kubwa zaidi na yenye idadi kubwa ya wapiga kura.

Hili la ukanda angalia sisi hili tuliliona lini Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?." na tukashauri nini!.

Saa hizi ndio wenzetu mnaliona, na baada ya Samia, akiisha ingia mwingine, ndio lile jingine la akiwa Mkristo ni lazima awe... ndilo nalo mtaliona!.

P
 
Mkuu Yohana Mbatizaji, @johnthebaptist , usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu Kanda ya Ziwa, ni Kanda determinant kwa sababu ndio inapiga kura inayoitwa a decisive votes kutokana na hii ndio Kanda kubwa zaidi na yenye idadi kubwa ya wapiga kura.
Hizi ni myth tu...

Wanaoamua nani awe Rais ni Ccm, hizo kura zenu ni kiini macho tu.
 
Hizi ni myth tu...

Wanaoamua nani awe Rais ni Ccm, hizo kura zenu ni kiini macho tu.
This is where you go wrong, na hili ndilo kosa kubwa la upinzani wa Tanzania, kudhani adui yao mkubwa ni CCM!. Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ..., numbers don't lie
Wanabodi,

14. Voting statistics

Tanzania: 2010 Presidential election results
Updated January 2010

The United Republic of Tanzania elections for parliament and the presidency were held on 31 October 2010.

Voting statistics
Registered Voters 20 137 303
Total votes 8 626 283
% Turnout 42.84
Valid votes 8 398 394
Spoilt votes 227 889
% Spoilt votes 2.64

Table source
Commonwealth 2010, 31.

Results
Candidate Party Votes % Vote
Jakaya Kikwete Chama Cha Mapinduzi (CCM) 5 276 827 62.83
WP Slaa Chama Cha Demokiasia na Maendeleo (CHADEMA) 2 271 941 27.05
Ibrahim Lipumba Civic United Front (CUF) 695 667 8.28
Peter Mziray Kuga Progressive Party of Tanzania (PPT-MAENDELEO) 96 933 1.15
Rungwe Hashim Spunda National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi) 26 388 0.31
Muttamwega Bhatt Mgaywa Tanzania Labour Party (TLP) 17 462 0.21
Yahmi Nassoro Dovutwa United People's Democratic Party (UPDP) 13 176 0.16
Total
8 398 394 99.99

Table source
Commonwealth 2010, 31.

References
COMMONWEALTH 2010 Report of the Commonwealth Observer Group: Tanzania General Elections 31 October 2010.

15. Kwa mujibu wa data hizo, JK amechaguliwa kura milioni 5 tuu kati ya watu milioni 40!. Waliojiandikisha ni milioni 20, lakini waliopiga kura ni milioni 8 tuu!, hii inamaanisha kuna watu milioni 12, ambao walijiandikisha lakini hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwemo wale waliokata tamaa na kuona kupiga kura ni wastage of time, hata upige vipi kura, matokeo ni yale yale lazima CCM ishinde, hivyo kuliko kupoteza muda wakaachana kabisa na kupiga kura!

16. Suppose 2015, Watanzania tutakuwa Milioni 50 wenye sifa za kupiga kura ni milioni 35, hawa wote wakihamasishwa kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura, mgombea wa CCM atajipatia kura zao zile milioni 6 za wanachama wao kwa mujibu wa tovuti ya CCM, halafu hizo kura milioni 29 zimuangukie mgombea wa upinzani, hata NEC ya CCM, wachakachue vipi, there will be no way out!, hivyo adui yetu mkubwa sio CCM, bali ni Watanzania wanaipigia kura CCM!.

17. Sasa ili kuwafikia Watanzania wote na kuwaamsha waliolala, Chadema haiwezi kuwafikia Watanzania wote kwa kutegemea mikutano ya hadhara na mass media za wengine. Chadema lazima wawe na mass media yake ambayo ita propagate the message of changing the mindset ya Watanzania. Chadema wana all the resource kumiliki media yake lakini very unfortunately they are myopic, hawana vision ya kuona mbali kuangalia nje ya box and see a bigger picture. Hawajui kupanga priorities zao. Bei ya gari moja tuu la M4C linatosha kununua transmitter ya Digital ya redio na TV. Chadema bila media yake, ni kutwanga maji kwenye kinu, CCM ina media yake na TV yake TBCCM, radio zake na magazeti yake, Chadema bila media yake, ikulu wataendelea kuisikia tuu kwenye bomba, 2015 ni CCM tena! .

Wasalaam.

Paskali
P
 
Hizo kura ni kiini macho tu, demokrasia bandia hiyo..
Siasa sio imani kama dini, ukiishaamua kuamini ni demokrasia bandia hata nikikuwekea numbers don't lie, bado huamini. Siasa sio imani , siasa ni sayansi ya siasa, and numbers don't lie!.
P
 
Back
Top Bottom