Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni Dhana Tuu?."

Ni kweli kuwa tunalo tatizo la udini na ukabila kwa kiasi fulani. Tatizo hili linakuzwa sana baada ya ccm na serikali yake kulitumia katika kuwagawa raia wake ili watawalike kwa urahisi. Kama mtakumbuka kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 kumekuwa na kauli nyingi za dini fulani kukiponda chama fulani cha upinzani kuwa ni chama cha kidini, wakafadhili taasisi moja ya kidini kutoa kauli za kidini na kibaguzi (mtakumbuka yaliyomkuta mkuu wa wilaya na kilemba chake walichodai eti ni cha kidini)
Kwetu sisi wakazi wa uswahilini tumekuwa tukiishi bila ya kuwa na hisia za tofauti zetu katika imani za kidini, mlakini mwenye nyumb (JK) alipoulizwa kuhusu changamoto za uchaguzi alidai kuwa kuna tatizo kubwa sana la udini.
Kama serikali inashabikia udini huu, basi ni hatari sana huko tuendako
 
Wanabodi, nauliza, hii sumu ya siasa za udini, ukabila na ukanda are they real au ni dhana tuu?!.

Hii dhambi ya mbegu ya sumu ya siasa za udini, ukabila na ukanda, zimepandwa na CCM, zimelelewa na CCM na hatimaye 2015, CCM itavuna ilichopanda!.

Jee mbegu hii ya sumu kaipanda nani?, jee tunaweza kuipiga vita kwa kuikanusha tuu (denial) au tunatakiwa kuubali ukweli mchungu na kukabiliana nao (facing the problem)!.

Nauliza tuu?

Pasco
Mwanzo nilidhani mavuno yangeanza kupatikana 2015!, I was wrong!. Hiki tunachoshuhudia ni mavuno tuu ya awali, msimu wa mavuno halisi bado!. Serikali ya CCM, ndio imeulea udini kwa kutochukua hatua stahiki tangu awali, sasa has to face the facts!. Tangu hotuba ile ya Mwalimu Nyerere kuhusu "nyufa", hakuna kilichofanyika, sasa ni kazi ya kujenga ukuta!.

Kwa vile sasa haya yametokea, huu sio wakati muafaka wa kumtafuta mchawi kwa kuendelea kulaumu tuu, bali tushauri nini cha kufanya kutuondoa hapa tulipofika na a way forward ili yasitokee tena!.

Poleni wote walioguswa!.

Mungu Ibariki Tanzania!.

Pasco.
Pasco.
 
Ni kweli kuwa tunalo tatizo la udini na ukabila kwa kiasi fulani. Tatizo hili linakuzwa sana baada ya ccm na serikali yake kulitumia katika kuwagawa raia wake ili watawalike kwa urahisi. Kama mtakumbuka kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 kumekuwa na kauli nyingi za dini fulani kukiponda chama fulani cha upinzani kuwa ni chama cha kidini, wakafadhili taasisi moja ya kidini kutoa kauli za kidini na kibaguzi (mtakumbuka yaliyomkuta mkuu wa wilaya na kilemba chake walichodai eti ni cha kidini)
Kwetu sisi wakazi wa uswahilini tumekuwa tukiishi bila ya kuwa na hisia za tofauti zetu katika imani za kidini, mlakini mwenye nyumb (JK) alipoulizwa kuhusu changamoto za uchaguzi alidai kuwa kuna tatizo kubwa sana la udini.
Kama serikali inashabikia udini huu, basi ni hatari sana huko tuendako

Hivi mtu akigundua tatizo na kusema bila ya kumumunya maneno kuwa kuna tatizo fulani. Je huko ndo kushabikia?
 
Mkuu kama umesoma raia mwema la leo ni wazi kuwa kama taifa tumefikia pabaya.Hatuwezi kupata viongozi waliobora kwa kubalance dini.Nimefedheheshwa sana na jinsi mwandishi alivyojaribu kupandikisha mbegu ya udini. kwa mfano
Summaye na Zitto
Pinda na Malima
 
Maintarahamwe hawakulitegemea kabisa hili la CUF na CHADEMA kushirikiana kiasi hiki, hili linawanyima usingizi kupita kiasi.

Ni kufuatia kilichoitwa chama cha waislam (cuf) kuungana na kile cha wakristo (chadema) + nccr & nld (wapagani) Ni shida
 
Kamanda BAK ni kweli kabisa hili la chadema kushirikiana na CUF magamba hayakutegemea kabisa...sasa maintarahamwe akina mwigulu yanahaha
 
CCM walianza na propaganda za ukabila zikashindikana. Wakaja na mbinu za ukanda zikachuja. Wakaibuka na singo ya udini haikulipa. Wakaparamia mazingaombwe ya ugaidi yakawarudi. Wakaibuka na kitisho cha kuingia msituni, kikagota. Sasa wamekuja na katiba ya kitapeli, lakini ndio kwanza katiba yenyewe imekuwa chachu ya kwaunganisha wapinzani!
 
Sasa ikiwa wakristo na waislam wameungana basis ni ushindi. Maana >90% ya watanzania ni waislam na wakristo. Plus 10% ya wapagani ushindi ni wakishindo
 
Ccm na Shetani ni ndugu wa damu kabisa. Siku zote shetani akishindwa huwa akubali na lazima atafute mbinu nyingine ili aendeleze uchafu wake, hivyo hivyo ccm baada ya kushindwa vibaya kwa propaganda zake za Udini,Ukanda,Ukabila na hili la katiba ya sita ya Chenge. Sizani kama ccm itanyamaza na badala yake ni lazima akatafute uwaribifu mwingine na kuuleta kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom