washa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2007
- 626
- 370
Ni kweli kuwa tunalo tatizo la udini na ukabila kwa kiasi fulani. Tatizo hili linakuzwa sana baada ya ccm na serikali yake kulitumia katika kuwagawa raia wake ili watawalike kwa urahisi. Kama mtakumbuka kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 kumekuwa na kauli nyingi za dini fulani kukiponda chama fulani cha upinzani kuwa ni chama cha kidini, wakafadhili taasisi moja ya kidini kutoa kauli za kidini na kibaguzi (mtakumbuka yaliyomkuta mkuu wa wilaya na kilemba chake walichodai eti ni cha kidini)
Kwetu sisi wakazi wa uswahilini tumekuwa tukiishi bila ya kuwa na hisia za tofauti zetu katika imani za kidini, mlakini mwenye nyumb (JK) alipoulizwa kuhusu changamoto za uchaguzi alidai kuwa kuna tatizo kubwa sana la udini.
Kama serikali inashabikia udini huu, basi ni hatari sana huko tuendako