Sumu ya kuua kunguru ni ipi?

Kwa hiyo ukaona uanzishe na Uzi kabisa[emoji1787][emoji1787]
Acha tu yaani hawa wadudu wanafujo sana na wameanza kuwepo hapa kuanzia mwaka jana ila sasa hivi naona kama wanaanza kukosa adabu. Yaani fujo nyingi.
 
Lazima tuwe na mpango wa kutokomeza kunguru weusi tii hawa ni ndege wasio na adabu kwa binadamu tena wanajikuta ma gangster sana
Ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah nimecheka hapo uliposema wanajifanya magangster. Of course hivi vindege vina madharau sana. Nimejiapiza siku nikimkamata mojawapo mzima mzima. Nitachuma bakora nitamtandika huku namsemea maneno yote ya dharau.
 
Nawewe punguza uwoga. Sasa unajifungia ndani kisa kunguru?
 
Ha ha ha ha. Dawa ni moja watege na neti ukiwakamata wapeleke ukawatelekeze huko njombe baridi iwashikishe adabu
 
Sasahivi wamepungua sanaaa, kuna wakati walikuwa kero mpaka kwenye vibanda vya chips wananyakua watu misosi

Ifanyike kampeni tokomeza kama miaka ile ya 2000's

Na ni Mzee Ruksa ndio aliwaleta huko pwani kutoka India
Hawakuletwa na mzee Ruksa kiongozi hawa waliletwa Zanzibar kutoka India miaka ya 70 lengo likiwa kuwatumia kuondoa mizoga maeneo ya ufukweni bila kufahamu madhara yake, basi wakaanza kuzaliana kwa kasi ya ajabu ndio wakaanza kuhamia maeneo mengine ya pwani ya bara kwa ukorofi wao wakaanza kuwashambulia wale kunguru wa asili mpaka wakawatokomeza mbali zaidi na pwani, hawa kunguru aisee ni very aggresive sifa yao kubwa mara zote wao huwa ndio wa kwanza kumuona adui ndio maana ni ngumu sana kumpiga kwa jiwe au manati kwa sababu unapojiandaa kumshambulia yeye anakuwa alishakuona zamaani na ukimtegea mtego au sumu hakikisha hakuoni unavyoweka, akikuona tu hata sogea hilo eneo, kingine wana hasira, kisasi na umoja, ikitokea mmoja kauwawa basi hilo eneo ni balaa, watakusanyika kundi eneo hilo wakipiga kelele za kuomboleza huku wakishambulia kila kinachokatiza kwa siku kadhaa. Kama ulidhani kunguru kumnyea binadamu ni bahati mbaya ulikosea hufanya hivyo kwa makusudi kabisa, ukikaa chini ya mti huwa wanakuja kimya kimya akikudondoshea puu ile unainua macho juu kumtazama utakuta kishatembea kitambo na sio puu tu wakati mwingine huwa ni mifupa au kipande cha mti, kiufupi kunguru weusi ni moja ya ndege wenye itelijensia ya hali juu sana ukilinganisha na ndege wengine.
 
Pole yako na umejichanganya kuwachokoza alshabab. Hilo bifu lao hutaliweza kwani sio la nchi hiyo. Halitaisha utatupa mrejesho hapa.
 
Nawewe punguza uwoga. Sasa unajifungia ndani kisa kunguru?
Bro unaweza kuwa huwajui hao ndio maana unasema hivyo. Hao wakiona umeua watoto wao ugomvi nao hauhishi. Huwa wanakusanyika, piga kelele, donoa na shambulia yule aliyesababisha mauaji yao. Fuatilia kisa chao na mbwa huko India.
 
Kunguru na Kunguni ni sawa??? Au mtoa mada anasumbuliwa na kunguni piaaa[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Huyo Jirani yako hajui hii Mbinu yako ?
 
Muulize muheshimiwa Ali Mwinyi ndio aliyo waleta
Yaani [emoji3062]
 
Mimi nilinunua mtego wa panya naweka kipande cha nyama. Niliwapunguza lakini wanikariri. Kila wakiona waliobaki wanaitana
Nitawachokoza Ili wanisaidie kunikimbiza niwe nakimbia kimbia nafanya mazoezi #kunguru marathon
 
[emoji16][emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…