Sumry imeua nane papo hapo

Sumry imeua nane papo hapo

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
6,035
Reaction score
15,064
Wadau, habari zenye uhakika kutoka katavi national park ninathibitisha kuwa basi la summry kutoka mbeya kuelekea mpanda - katavi lilitumbukia kwenye mto maarufu pale mbugani kama shule ya viboko. Mpaka ninavyoandika saa 4.00 asubuhi hii ya ijumaa 5/7/2013 maiti mbili ziko hospital mpanda na maiti sita zimeopolewa toka mtoni. Maiti zaidi zikipatikana tutawajuza. Poleni majeruhi, poleni wafiwa.

Basi lilitumbukia mnamo saa 8: 16 usikudereva alipitia njia illiyokatazwa na serikali so aliiba njia.
Basi lilijaza kupita maelezo, kumbuka ni wakati wa mavuno kwahiyo watu wanasafiri sana,kumbuka hii njia ni summry pekee anayefanya biashara, akija kampuni nyingine anawapiga majuju hadi wanahama.... Wafipa wanajua anachofanya summry.
Mto ambao basi limetumbikia ni maarufu kwa ajali kama hizo.
 
Madereva wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha maafa haya....poleni wafiwa....hizo sababu za majuju hazina msingi kwa wakati huu
 
MUNGU wangu! Mmmmmh!

Wote wale waliopatwa na msiba Mwenyenzi MUNGU awape nguvu!
 
kumbuka hii njia ni summry pekee anayefanya biashara, akija kampuni nyingine anawapiga majuju hadi wanahama.... Wafipa wanajua anachofanya summry.
Mabasi hayaendi hiyo njia, badala ya kujiuliza kwa nini tupate majibu yenye mantiki, tunarahisisha kufikiri, tunasema Summry anawapiga juju competitors wake, unaona tulivyo na akili za samaki na kwa nini tutaendelea kufa njiani kwa kudumbukiza mabasi kwenye mito? Sasa tusemeje, competitors wa Summry wamepata mganga mkali zaidi?

Anyhow, I guess kazi ya Mungu haina makosa, amewapenda zaidi!
 
Poleni sana majeruhi wote.
Poleni sana wafiwa wote
R.I.P. waliotangulia mbele za haki.
 
wadau, habari zenye uhakika kutoka katavi national park ninathibitisha kuwa basi la summry kutoka mbeya kuelekea mpanda - katavi lilitumbukia kwenye mto maarufu pale mbugani kama shule ya viboko. Mpaka ninavyoandika saa 4.00 asubuhi hii ya ijumaa 5/7/2013 maiti mbili ziko hospital mpanda na maiti sita zimeopolewa toka mtoni. Maiti zaidi zikipatikana tutawajuza. Poleni majeruhi, poleni wafiwa.

Basi lilitumbukia mnamo saa 8: 16 usiku
dereva alipitia njia illiyokatazwa na serikali so aliiba njia.

Basi lilijaza kupita maelezo, kumbuka ni wakati wa mavuno kwahiyo watu wanasafiri sana
kumbuka hii njia ni summry pekee anayefanya biashara, akija kampuni nyingine anawapiga majuju hadi wanahama.... Wafipa wanajua anachofanya summry.
Mto ambao basi limetumbikia ni maarufu kwa ajali kama hizo.

apo kwenye blue,dereva kama mzima inafaa awajibishwe kwanza bus aziruhusiw kutembea mpaka muda huo,pia alipita njia isiyo rasmi kwa sababu alijua amevunja sheria,pia abiria ni wapumbavu kwa kuruhusu dereva avunje sheria na wao wakikenua meno,mwisho mungu awalaze pema pepon marehemu wote na majeruhi wapone haraka.hii siyo mipango ya mungu ni ya dereva na abiria
 
pole kwa wafiwa. majeruhi Mungu awaponye upesi.
 
Walikuwa wanatafuta nini saa 8:16 za usiku?
Ukiwaambia wamekufa kijinga utakuwa huwatendei haki?Mambo mengine ni kumsingizia Mungu tu eti kuwa ni mpango wake,hapo huo ni mpango wa dereva na abiria wake,waache kucheza tena na maisha ya watu.
 
Poleni sana majeruhi wote.
Poleni sana wafiwa wote
R.I.P. waliotangulia mbele za haki.
Amen
 
Nakumbuka summry nyingine imeua juzi kati apa njia ya dodoma..poleni.
 
Mabasi hayaendi hiyo njia, badala ya kujiuliza kwa nini tupate majibu yenye mantiki, tunarahisisha kufikiri, tunasema Summry anawapiga juju competitors wake, unaona tulivyo na akili za samaki na kwa nini tutaendelea kufa njiani kwa kudumbukiza mabasi kwenye mito? Sasa tusemeje, competitors wa Summry wamepata mganga mkali zaidi?

Anyhow, I guess kazi ya Mungu haina makosa, amewapenda zaidi!

Umefikiria vyema ndugu! hakuna cha juju wala nini ...summry inamuhusu sana huyu jamaa (wapigeni tu, maana tumechoka sasa!)
 
Poleni majeruhi
RIP Marehemu wote
Poleni wahanga wote wa hiyo ajali
 
Walikuwa wanatafuta nini saa 8:16 za usiku?
Ukiwaambia wamekufa kijinga utakuwa huwatendei haki?Mambo mengine ni kumsingizia Mungu tu eti kuwa ni mpango wake,hapo huo ni mpango wa dereva na abiria wake,waache kucheza tena na maisha ya watu.

Nafikiri hujawahi fika mkoa huo na hata miundo mbinu ya huko hauifahamu. Jinsi miundo mbinu ilivyo mibovu possible walitoka Sumbawanga asubuhi wakijua watawahi fika. Je kama walifika mbugani usiku wangelala wapi? kosa hapo ni la dreva kupita njia isiyoruhusiwa.
 
... RIP marehemu wote, na poleni wafiwa wote!

Watanzania tunajua kuongea sana tu, Na porojo kwa wingi' lakini kwenye MATENDO NI SIFURU.
 
Back
Top Bottom