Sumry imeua nane papo hapo

Sumry imeua nane papo hapo

Poleni wafiwa, Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, amen
 
Ni Sumry tena kama kama ndani mwez ana ajali mbili. SUMATRA wapo 2 kufungia dar express lakini hii haitafungiwa . Mungu awape nafuu majeruhi ila sitaki kusikia kazi ya Mungu haina makosa kwenye hili coz n uzembe wa wachache asihusishwe Mungu hapa.
 
Again!!!!!!!!!!!! Sumry kila siku? poleni sana majeruhi, na mliopoteza wapendwa wenu. mungu awatie nguvu sana
 
Poleni sana wafiwa na Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu. Pia tumwombe Mwenyezi Mungu awaponye haraka majeruhi wapate kurudi katika ujenzi wa Taifa. Hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya dereva wa basi hilo kama hajafa.
 
aisee inasikitisha sana
ajali nyingi ni uzembe wa madereva
Inabidi sana suala la madereva liangaliwe upya
wawe wamepitia chuo cha mafunzo pale mabibo.
 
Aliyepiga JUJU ni mwana JF aliyeweka picha ya Basi la AIR MSAE,kwani liliua kwa kutumbukia mtoni.Tulikua tumesahau siku nyingi hii Ajali,sasa ameweka hiyo post Smry nayo Imetumbukia na kuua.Huyo atuambie alikua anamaanisha nini.9Tehetehe!)
Halafu hawa wenye mabasi wakiwa wanakaribia kutoa mabasi mapya huwa yale ya zamani yanapata ajali na kuua.Hii makitu sijui iko vipi.
 
Madereva wazingatie sheria za usalama barabarani ili kuepusha maafa haya....poleni wafiwa....hizo sababu za majuju hazina msingi kwa wakati huu

Wamiliki wa hayo mabasi nao waache kugeuza vifo vya watu kutajirikia
 
Walikuwa wanatafuta nini saa 8:16 za usiku?
Ukiwaambia wamekufa kijinga utakuwa huwatendei haki?Mambo mengine ni kumsingizia Mungu tu eti kuwa ni mpango wake,hapo huo ni mpango wa dereva na abiria wake,waache kucheza tena na maisha ya watu.

Yumkini watu huwa hatusomi wala kuslkiliza redio. Kikosi cha usalama barabara walisha pitisha sheria kwamba magari yaruhusiwe kusafiri mwisho saa 6 usiku. Ila walitoa angalizo iwapo gari la abiaria litafika eneo ambapo ni mjini na dereva akaona kwamba hawez kufiika kwenye mji mwingine kabla ya saa sita basi basi hilo lilale katika mji lililopo.

Mara nyingi sana abiria kutoa Mbeya kwenda Arusha huwa wanafika arusha saa 4 ama 5 lakini zamani walikuwa wanalala njiani same ama moshi mjini. sijui eneo ambalo basi hilo limepita ila naona kosa kubwa zaid liko kwa dereva ambaye amepita njia iliyokatazwa na polis wa usalama barabarani.
 
Majeruhi mwingine mmoja amefariki, hivyo kufanya idadi ya vifo kufikia 9. Dereva wa gari kakimbia na majeruhi ni 50.
 
Haya mabus yatatumalza mwee..Mungu awaponye walioumia n awapumzishe salama waliofariki
 
Nafikiri hujawahi fika mkoa huo na hata miundo mbinu ya huko hauifahamu. Jinsi miundo mbinu ilivyo mibovu possible walitoka Sumbawanga asubuhi wakijua watawahi fika. Je kama walifika mbugani usiku wangelala wapi? kosa hapo ni la dreva kupita njia isiyoruhusiwa.

Sumbawanga na Mpanda hivi sasa sio mbali sana kiasi cha gari kufika muda huo endapo lilitoka asubuhi Sumbawanga. Siku hizi kuna basi linalotoka Mbeya kwenda Mpanda mojamoja na huwa linapita Sumbawanga mchana. Huenda hili lilipita Sumbawanga jioni sana.
 
Sumbawanga na Mpanda hivi sasa sio mbali sana kiasi cha gari kufika muda huo endapo lilitoka asubuhi Sumbawanga. Siku hizi kuna basi linalotoka Mbeya kwenda Mpanda mojamoja na huwa linapita Sumbawanga mchana. Huenda hili lilipita Sumbawanga jioni sana.

hili litakuwa limetokea Mbeya,thats why likapita hiyo mida!!!!
 
hili litakuwa limetokea Mbeya,thats why likapita hiyo mida!!!!

acha kutetea upuuzi mkuu,hivi saa 8 ya usiku mnaenda wapi na basi?kwanini msipaki hata kabla ya saa 5 kama mnaona hampo ktk mazingra ya kuimaliza mbuga mapema?UKIAMUMUA KU-TAKE RISK,KUBALIANA NA MATOKEO YAKE YANAYOWEZA KUJITOKEZA,(kwamfano,ukitembea na mwanafunzi,kubaliana na kifungo cha 30yrs ukikamatwa)HAKUNA KUMSINGIZIA MUNGU KWA LOLOTE HAPO
 
SUMRY kila siku ajali!Sumatra mnamuogopa pinda na kada wake wa ccm?Yanatumaliza haya ma bus
 
1010833_532559233460635_1509365397_n.jpg
Ajali yenyewe hiyo hapo....
 
Back
Top Bottom