Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,422
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema kwamba ikiwa rushwa itazidi ndani ya chama chake chama cha CCM, atajiondoa kutoka chama hicho. Haikuweza kufahamika mara moja kama atahamia chama gani lakini kuna tetesi kwamba huenda akahamia CHADEMA.
 
Yaaani habari hii kwako umuhimu ni atakakoenda badala ya uzito wa hiyo "rushwa"?????!!!!

Nchi rahisi sana kuwa kiongozi hii
 
Rushwa izidi hapa iweje? Huyu nae ni mnafiki tu abaki huko huko na rushwa zao
 
Yaaani habari hii kwako umuhimu ni atakakoenda badala ya uzito wa hiyo "rushwa"?????!!!!

Nchi rahisi sana kuwa kiongozi hii

Hayo ni maoni yako binafsi. Hakuna mahali popote nilipodai hivyo.
 
Kauli kama hii kutolewa na Sumaye ni kujishushia heshima tu.

Angekaa kimya akisubiria parapanda lilie basi.

Kama CDM watampokea na kumpa vyeo nao watakuwa mazuzu tu.

He's a loser.
 
Huyu nae hajielewi, unapimaje hicho kiwango cha rushwa ili ujue kimezidi? yaani hata kwa rushwa inayoendelea si tu ndani ya ccm lakini hata katika serikali ya ccm, yeye bado anaona haijazdi, hii inadhihirisha nae ni mla rushwa
 
Ni huyu huyu aliyesema wafanyabiashara wanaotaka mambo yao yanyooke wajiunge CCM au ni Sumaye mwingine. Akiwa Waziri Mkuu alifanya kila linalowezekana kuwabana wafanyabiashara wanounga mkono upinzani na wapo waliopoteza mali zao kwa kuunga mkono upinzani. Dhambi hii itamtafuna maisha yake yote, hata huku kutapatapa ni sehemu ya malipo. Jitu kama hili unalipokea vizuri baada ya wiki unalifukuza.
 
mbona tayari rushwa ilishazidi CCM au anataka IZIDI kiasi gani ndipo ajiondoe? huyu naye ni mchumia tumbo tu!

Haya hukuyaona mwanzo ila anapotaka kuhamia????!!!!!
Tuna shida kubwa ya wanachi kuliko Viongozi
 
Kwahiyo anakiri kwamba rushwa ipo huko aliko. Ila anangoja izidi mpaka kiwango anachokiona yeye ndio aondoke!
 
mzee boya kweli hivi nani kamwambia kuwa anafaa kuwa Rais hii nchi inawazee wengine wa ajabu kweli.
 

mzee nadhani angegombea baraza la wazee wa kimburu pengine angeshinda.
 
Wamejionea jinsi CDM ilivyojipanga kupiga rushwa.Kwa sasa CDM yatosha.Sumaye Kagundua kuwa kako sea njia, rudi kwa Yesu utaokoka kupitia CDM
 
SUMAE hana mvuto tena,apumzike amefaidi sana,enzi zake vyombo vya habari havikuwa Huru,BUNGE halikuwa live,walikuwa wanafanya watakavyo.
 
Mkuu Tipau, asante kwa taarifa hii!. Huyu naye?!, eti kama rushwa itazidi?!. Ndani ya CCM, anataka rushwa izidi mara ngapi zaidi ya hii rushwa iliyopo?!. Sumaye anataka ikizidi kufikia kiwango gani?, hapo ilipo ndani ya CCM, rushwa imeisha zidi hadi kufurika kitambo!, sasa huyu anayeulizia kama rushwa ikizidi, anaulizia CCM ipi?!.

Sumaye aseme tuu, baada ya UKAWA kukosa mgombea mmoja wa 2015, wamemuomba yeye agombee and in principle atakuwa kakubali, sasa anatafuta pa kutokea CCM, ili aeleweke na jamii imuelewe!. Tena namshauri afanye hivyo mapema, kabla jamaa zake hawajabadili ile sheria ya viongozi wakuu wastaafu na kuongeza kipengele "kiongozi mkuu mstaafu atalipwa mafao na marupurupu stahiki" only if hatajishughulisha na siasa basada ya kustaafu!" kwani kuendelea kujishughulisha na siasa nayo ni ajira!.

Hajajifunza tuu kwa wenzake!, Mwalimu Nyerere Foundation, Benjamin Mkapa/IOTF, sasa JMK Foundation/WAMA on the making, na yeye aunde NG'0 yake!, hive ile HOPE FOUNDATION imeishia wapi?!.

Thanks.
Pasco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…